Wana Global naomba kushea na nyinyi stori ya jaribio la utapeli lililonitokea jana tarehe 26/03/2012,
majira ya saa sita na nusu mchana nilipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kwa jina la Patric Makombe ambaye alidai kuwa anafanyakazi shirika la chakula duniani katika kambi moja huko Kigoma. Mtu huyo alilitaja jina langu kwa ufasaha kazi yangu namba ya gari na mtaa ninaoishi.
Mtu huyo alidai kuwa amewahi kufanyakazi katika benki ya NMB Tanga baadae akahamia WFP Kigoma namba ya simu ya mtu huyu ni 0712127749. Alinijulisha kuwa hapo ofisini kwake wanahitaji dawa fulani ya kuhifadhia chakula na kwamba baada ya muda bosi wake atanipigia kwa kuwa kwa wakati ule alikuwa kwenye kikao lakini akaniomba nikubali kushirikana nae kwa kuwa ananifahamu kuwa ni mtu mwaminifu na nisingeweza kuwadhulumu baada ya biashara.
Baada ya masaa matatu hivi alinipigia simu mtu aliyejitambulisha kwa jina la Thomas Michael ambaye alidai kuwa ni coordinator wa WFP Kigoma na alinieleza kuwa anahitaji product inaitwa DAMOLINE LIQUID BEST IN FOOD PAIR 50. Na akaniambia nimtafute mtu anaitwa Dr. Msuya Peter namba ya simu 0656367291 ni muulize wanauzaje pea moja ya hiyo dawa kisha nimjulishe lakini nisimwambie chochote huyo Dr. Msuya kwa kuwa mwaka jana aliwadhulumu walipo fanya dili kama hiyo. Aliendelea kudai kuwa bei nitakayo ambiwa atanielekeza niongeze kiasi fulani kisha bosi wake ambaye ni mzungu atakapokuja kununua nimpige hicho cha juu na hiyo ndio itakuwa faida yetu. Ingawa nilishaanza kustuka lakini nilifanya kama nilivyoelekezwa kumpigia Dr. Msuya naye akanijibu dawa kwa pea moja ni dola 3100 za Marekani ambazo ni karibu ya shilingi za Kitanzania milioni tano. Nilipo mrudishia jibu akasema huyo Mzungu akija ni muuzie dola 4000 na kwamba faida yetu kwa kila pea itakuwa dola 900 sawa na shilingi milioni moja na laki nne hivi. Na kwamba Mzungu atakapokuja atachukuwa pea hamsini. kwa kuwa ilikuwa jioni tulikubaliana tuwasiliane siku inayofuata ili tuanze dili. Usiku huo nilamua kufuatilia kwenye mtandao maana ya hiyo DALOMINE LIQUID. Hamaaad nilipofungua tu nikakutana na ujumbe jihadhari na utapeli huu kwenye blogu mbili tofauti za bongo. Kwa mujibu wa maelezo yao kama ningeenda kwenye dili ningeambiwa na matapeli kuwa niende kwa Dr. Msuya ninunue sample moja ya dawa kisha niende nayo Golden Tulip au uwanja wa ndege kumsubiri bosi wake ambaye angekuwa anatokea Kigoma kisha ningeondoka na mtu mwingine kwenda kuchukua pea 49 zilizobaki pamoja na kulipwa kitita changu kisha tugawane. Kumbuka kuwa kama ningeenda kwa Dr. Msuya ningetakiwa kwenda na dola 3100 ili nipewe hiyo sample na kwa kufanya hivyo ningeenda Golden Tulip kuwatafuta hao waungwana nisingekuta mtu. Baada ya kujua ujanja wao niliwasubiri wanipigie siku iliyofuta na walifanya hivyo majira ya saa nne asubuhi. Niliwaomba wanitumie nauli toka nilipo hadi Dar ili tuendelee na dili ndipo walipostuka na hawajapiga simu tena. Hivyo nawaomba sana wana Global muwatahadahrishe ndugu zetu wote kuhusu utapeli huu mpya. Watu wameibiwa mamilioni ya shilingi mkitaka kuhakikisha fungueni GOOGLE kisha andika DALOMINE LIQUID BEST IN FOOD halafu fuatilia trend za jamaa wa mablog wanavyoshusha hata mwenye blogu mmoja anaitwa Michuzi limemfika jambo hili tahadharini sana ndugu zangu.
No comments:
Post a Comment