FAIDA ZA NDIMU KWA AFYA YA MWILI WA BINADAMU.
Fahamu kwanza Ndimu na limao zina utofauti katika virutubisho .. japo baadhi vinafanana.
Faida za Ndimu
1.Ndimu husafisha damu na kuondoa tatizo la homa.
2.Ndimu huondoa gesi tumboni kwa wenye matatizo ya tumbo kujaa gesi.
3.Ndimu husaidia kuondoa sumu mwilini.
4.Ndimu huondoa tatizo la allergy (Mchafuko wa damu).
5.Ndimu ukikamulia kwenye chai ya rangi huzuia sumu ya majani ya viwandani yasikudhuru.
6.Ndimu inaondoa kipara kwa wenye matatizo ya nywele kunyonyoka. Matumizi chukua maji ya ndimu changanya na mafuta ya zaituni kidogo kisha pakaa kichwani kaa muda wa masaa mawili kisha osha kichwa chako kwa maji ya kawaida. Tiba hii itakusaidia kukuza nywele zako kwa wale wenye tatizo la nywele kunyonyoka zitakuwa nyingi fanya hivyo kwa muda wa siku saba(7)
7.Ndimu inatibu kifua na mafua matumizi changanya maji ya ndimu na maji ya vuguvugu... kunywa mara nyingi.
8.Ndimu huondoa harufu mbaya kinywani (mdomoni)
.. kwa sababu inasaidia kuua bakteria wabaya wa mdomoni wanaosababisha mdomo kunuka.
Matumizi tumia maji ya ndimu kwa kusuktua na kupigia mswaki asubui na jioni kwa muda wa siku 21 tatizo litaisha.
9.Ndimu inapunguza maumivu kama mtu amechomwa na msumari au vitu vyenye ncha kali au kujikata,, Kamua ndimu pakaa sehemu yenye tatizo tiba hii itakusaidia kidonda kipone kwa haraka.
10.Pia Ndimu ni nzuri kuitumia pale umalizapo kunyolewa haina haja ya kutumia spirit.
Ndimu ni nzuri itakusaidia kuondoa kuondoa Vipele, Mba, na magonjwa yote ya ngozi.
No comments:
Post a Comment