My Web

Emmanuel

CONTACT

Sunday, April 19, 2020

Maombi ya Asubuhi

Maombi ya asubuhi na faida zake

Ndege na wanyama huamka asubuhi na mapema wakimsifu Mungu. Watumishi wa Mungu wengi Walikua wakiamka asubuhi na kuomba. Baadhi yao ni Ibrahim,Daudi alipenda kuamka asubuhi na kuomba, katika Zaburi 88:13 LAKINI MIMI NIMEKULILIA WEWE, BWANA NA ASUBUHI MAOMBI YANGU YATAKUWASILIA na Zaburi 57:8, AMKA UTUKUFU WANGU, AMKA KINANDA NA KINUBI, NITAAMKA ALFAJIRI, maombi ya asubuhi kwa Daudi yalimfanya kuwa mshindi, Mungu aliupenda moyo wa Daudi.

Yakobo alipopigana na malaika akamwambia sitakuacha mpaka utakaponibariki, ilikua alfajiri na mapema! Matendo 16:25 Paulo na Sila waliomba alfajiri mapema sana, milango ya gereza ikafunguka, Yoshua alipenda kuamka alfajiri, na hata Yesu mwenyewe aliamka asubuhi na kuomba na kuna wakati aliwakuta wanafunzi wake wamelala akawauliza hamkuweza kukesha nami hata saa moja? Pia Mungu alipokua akiwatuma watumishi wake aliwatuma alfajiri na mapema, Yeremia 25:4 NAYE BWANA AMETUMA KWENU WATUMISHI WAKE WOTE, HAO MANABII, AKIAMKA MAPEMA NA KUWATUMA….. na Joshua 6:12 Yoshua akaondoka asubuhi na mapema, nao makuhani wakalichukua sanduku la Bwana.

Unapoanza kuomba asubuhi unamtangizia shetani kwamba mnaanza vita kwamba uko tayari kwa mapambano,unamtangazia adui yako, ugonjwa wako, tatizo lako kwamba kuanzia sasa hakupati maana umejitoa kupanga maombi yako kwa Mungu Zaburi 5:3 BWANA ASUBUHI UTASIKIA SAUTI YANGU, ASUBUHI NITAKUPANGIA DUA YANGU NA KUTAZAMIA.

Ningependa ufahamu faida za maombi ya alfajiri

1.UTAVIKWA NGUVU ZA MUNGU Kutoka 16:7 Na asubuhi ndipo mtakapouona Utukufu wa Bwana, kwa kuwa yeye asikia manung’uniko yenu mliyomnung’unikia Bwana.

2.HUTAINGILIWA NGUVU ZA GIZA, maana umefunikwa na nguvu za Mungu, mapepo, magonjwa, havina uwezo kuingia kwenye maisha yako, vifungo vyote vya shetani, nira zake, mizigo yake vitaharibiwa na kuwekwa huru Mathayo 11:28 NJOONI KWANGU, NINYI NYOTE MSUMBUKAO NA WENYE KULEMEWA NA MIZIGO NAMI, NAMI NITAWAPUMZISHA. ISAYA 10:27 TENA ITAKUA KATIKA SIKU HIYO MZIGO WAKE UTAONDOKA BEGANI MWAKO, NA NIRA YA SHINGONI MWAKO, NAYO NIRA ITAHARIBIWA, KWA SABABU YA KUTIWA MAFUTA,

3.UTAKUA MBALI NA MAONEVU, SHETANI NA MALAIKA ZAKE, Zaburi 105:14-15 Hakumwacha mtu awaonee, hata wafalme wake aliwakemea kwa ajili yao, akisema, msiwaguse masihi wangu, wala msiwadhuru nabii zangu. Mungu anatuita masihi

4.TUKIAMKA ASUBUHI TUNAVIKWA HAKI ISAYA 54:14-17, Utathibitika katika haki ….kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa, na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utahukumu kuwa mkosa, huu ndio urithi wa watumishi wa Bwana, na Haki yao inayotoka kwangu mimi, Asema BWANA

5.KUINULIWA KUTOKA MAVUMBINI HADI UTUKUFU Zaburi 113:7-9 Humwinua mnyonge kutoka mavumbini, 1 Sam 2:7-8 …..humwinua mnyonge kutoka mavumbuni, humpandisha mhitaji kutoka jaani…

6.UNAKUA NA BIDII KATIKA KAZI ZAKO, mtu anayeomba asubuhi na mapema ana bidii kwa kazi yake, anafanikiwa kimwili na nyumba yake wanafanikiwa. Kuamka asubuhi ni kuwa shahidi mwaminifu wa Yesu Waebrania 10:38 LAKINI MWENYE HAKI WANGU ATAISHI KWA IMANI, NAYE AKISITASITA, ROHO YANGU HAINA FURAHA NAYE, Waebrania 11:6 LAKINI PASIPO IMANI HAIWEZEKANI KUMPENDEZA, KWA MAANA MTU AMWENDEAYE MUNGU LAZIMA AAMINI KWAMBA YEYE YUKO, NA KWAMBA HUWAPA THAWABU WAMTAFUTAO

7.UTAKUA HAI, MWENYE KUKUA KIROHO. Kilicho hai kinaongezeka na kukomaa ili mtu akue anahitaji chakula ndio NENO la Mungu ambapo UNACHANUA, Mark 4:1-20, Hosea 14:5 NITAKUWA KAMA UMANDE WA ISRAELI,NAYE ATACHANUA MAUA KAMA NYIRORO, NA KUIENEZA MIZIZI YAKE KAMA LEBANONI

8.UTAZAA MATUNDA, hivyo hutakatwa na kutupwa motoni John 15:1-6, Luka 3:9 NA SASA HIVI SHOKA LIMEKWISHA KUWEKWA PENYE MASHINA YA MITI; BASI KILA MTI USIOZAA MATUNDA MAZURI HUKATWA NA KUTUPWA MOTONI. Matawi yanayozaa yanasafishwa matawi yasiyozaa yanakatwa, Mtu kama ulikua na tabia haubadiliki, ukiaomba asubuhi, hofu ya Mungu itakaa ndani yako na hutatenda dhambi tena, mfano kama ulikua na tabia ya kutukana kinywa chako kinakamatwa! (haongei lugha chafu) UTUKUFU WA MUNGU UNAKUFUNIKA

*ASUBUHI NJEMA,SIKU NJEMA*

No comments:

Post a Comment

New