*Tuombe Sala/ Dua*
Mwenyezi *Mungu* mwenye wingi wa rehma tunashukuru leo tarehe 18/4/2020 siku ya Jumamosi kwa ulinzi wako uliotupatia usiku mzima, tumeamka salama tukiwa na afya njema kabisa lakini tukiwa bado na hofu kubwa ya Coronavirus Covid - 19 juu yetu sisi. Ni siku ya pili leo hii tunaendelea kukuomba na kukunyenyekea Mwenyezi *Mungu* utuondolee gonjwa hili linalowanyima watu wengi usingizi.
Mwenyezi *Mungu* maambukizi ya ugonjwa huu pamoja na vifo vinaongezeka kwa kasi kubwa ya kutosha na inayotupa mashaka kiasi kwamba hatujui kesho yetu itakuwaje, sisi waja wako tunakuomba wewe Mwenyezi *Mungu* mwenye uwezo pekee wakuumaliza ugonjwa huu. Tiba yake mpaka sasa haijapatikana zaidi ya watu kuelezana bila uhakika kwamba sijui dawa ni kitunguu swaum, tangawizi na limao zinasidia kuua hao vijidudu vya Coronavirus Covid - 19, tunaamka huku tukiwa na mashaka mioyoni mwetu tukijiuliza leo nitaimaliza salama kutokana na mihangaiko yetu ya kutafuta ridhki, tunaomba kwako Mwenyezi *Mungu* tena na tena na kila wakati tunaomba utuondolee ugonjwa huu Mwenyezi *Mungu*, tunaomba ukatende miujiza kwa madaktari, wauguzi na wasaidizi wote na ukawalinde wakati wa kuwahudumia wahanga wa ugonjwa huu, wakawe majasiri, wakaweke uzalendo mbele, wakawatibu wagonjwa bila ya woga lakini ukawalinde pia kwani nao wana familia zao wameziacha nyumbani huku zikiwategemea. Tunawaombea wale ambao wameshatangulia mbele za haki uwapunguzie adhabu ya kaburi na wale wanaougua wakapate kupona na kurejea kwenye hali zao kiafya kama kawaida.
Mwenyezi *Mungu* tunaomba kutubu dhambi zetu, tunaomba utusamehe Mwenyezi *Mungu*, tunaomba huruma yako kwetu Mwenyezi *Mungu*, tunataka kuziacha dhambi zetu.
Nchi nzima ya Tanzania na hata Dunua nzima leo hii na siku zijazo hatutachoka kuendelea kukuomba Mwenyezi *Mungu* kutuondolea na kutuhepusha na magonjwa yanayokosa tiba na hata yale yenye tiba.
Ewe Mwenyezi *Mungu* tunaomba tusaidie.
*Amen 🙏🏾 Amiin 🤲🏾*
No comments:
Post a Comment