Usonji Ni Nini?
Usonji (Autism) ni tatizo linalotokea katika ukuaji na linaathiri namna mtu anavyohusiana na wengine, katika mawasiliano/lugha, tabia yake na namna anavyouelewa ulimwengu. #Uzi
Hujidhihirisha zaidi mtoto anapofikia umri wa miaka 3. Kisababishi hakijulikani.
Dalili kuu za watu wenye usonji ni:
1.Hawapendi kujihusisha na watu (social interaction)
2.Inakuwa vigumu kuchangamana na watoto wenzake kama wile kwenye michezo, na kuelewa hisia za watu wengine.
3. Tabia ya kurudia rudia vitu (Repetitive behavior).
Namna gani unaweza kumtambua mtu mwenye usonji:
1. Inakuwa vigumu kutazama watu machoni (poor eye contact)
2.Wana tabia ya kukaa wenyewe (kujitenga)
3. Hawapendi mabadiliko
4.Hawawezi kuchezea sauti kabla ya miezi kumi na mbili.
5. Hawawezi kuongea sentensi au kurudia sentensi. baada ya miaka miwili.
6.Wanapoteza uwezo wa kuongea au kujifunza.
7.Huwa na uwezo mkubwa na kukumbuka vitu.
Pia Wanaweza kufanya vizuri shuleni, chuoni, na hata kwenye kazi. Wanaweza kuwa na uwezo maalum kwenye vitu mfano mahesabu, pazzo, au ufundi Fulani. Wanaweza kuwa na matatizo kujifunza kama vile kutoweza kusoma na kuandika.
Kusaidia watoto hawa ni kuwapa huduma ya shule ya awali na elimu maalum mapema.
Mtoto mwenye usonji huwa ni msumbufu sana, ana hasira, muharibifu, mchoyo, mbinafsi, mzito kuelewa, anapenda sana kujiumiza, sio msikivu, anapenda kurukaruka na kufanya vitendo vingine vya kushangaza.
No comments:
Post a Comment