Jopo la mahakama moja ya
Marekani limeamua kuwa kampuni kubwa ya teknolojia ya Korea Kusini,
Samsung, iliiga baadhi ya ufundi mpya wa kampuni ya Marekani ya Apple
kuunda simu zake wenyewe za kisasa za smartphone na kumputa ndogo -
tablet.
Samsung imelalamika kuwa Apple inajaribu kuhodhi soko zima la smartphone, na imesema itakata rufaa.
Zaidi ya nusu ya simu za smartphone zinazouzwa duniani ni ama za Apple au Samsung, na kampuni hizo mbili zinashtakiana katika mahakama ya nchi mbali mbali duniani.
No comments:
Post a Comment