Rais wa zamani wa Marekani, Bill Clinton amemtetea vikali mgombea urais wa chama cha Democrats nchini Marekani Barack Obama.
Katika hotuba iliyochukua muda wa dakika 50
katika kongamano la chama hicho linalofanyika mjini Charlotte, North
Carolina, Clinton alikosoa sera za uchumi za chama pinzani cha
Republican.Rais Obama atamenyana na mgombea wa chama cha Republican Mitt Romney katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Novemba.
Hotuba ya Clinton ni dalili ya kuimarika kwa uhusiano kati yake na Obama na pia kama juhudi za kupiga jeki mvuto wa obama miongoni mwa wazungu wanaofanya kazi.
Kura za maoni zinaonyesha kuwa wapiga kura wa chama hicho wamekuwa waangalifu sana kuhusu sera za Obama lakini Clinton ana rekodi nzuri ya kuwashawishi watu kumuunga mkono Obama.
Clinton aliambia wafuasi wa chama '' Amueni nchi mnayotaka kuishi. Ikiwa mnataka viongozi wasio wajali basi pigieni kura chama cha Republican. Mkitaka nchi yenye nafasi nyingi na ambayo majukumu yanagawanywa, basi sote tuko pamoja. Lazima mumpigie kura Barack Obama na makamu wake Joe Biden."
Bwana Clinton alikosoa vikali chama cha republican kwa kuzuia juhudi za uchepuzi wa uchumi na badala yake kujihusisha na mijadala kuhusu sera.
Kura za maoni zinaonyesha Barack Obama akiongoza kwa asilimia 47 huku mpinzani wake Mit Romney akimfuata kwa asilimia arobaini na sita.
No comments:
Post a Comment