Bunge la Congress nchini Uruguay limepitisha sheria ya kuhalalisha utoaji mimba katika hali zinazokubalika.
Bunge hilo limepitisha sheria hiyo kufuatia
majadiliano makali yaliyoishia kwa wabunge hao wa Congress kuipitisha
kwa kura 50 dhidi ya 49.Sasa hoja hiyo itawasilishwa katika bunge la juu la Senate ambalo linatazamiwa kuiidhinisha.
Sheria hiyo itawaruhusu wanawake kutoa mimba kabla haijafika wiki 12 ilimradi wamepata ushauri nasaha kutoka kwa madaktari wasiopungua 3 ili kufahamishwa hatari za kuavya mimba.
Mbali na Cuba, Uruguay itakuwa nchi ya kwanza katika ukanda wa Amerika kusini kuruhusu mwanamke yeyote anayetaka kutoa mimba fursa ya kufanya hivyo.
No comments:
Post a Comment