Shirika la kutetea haki za
watoto Save the Children, limekusanya maelezo ya kutisha na kuogofya
kuhusu visa vinavyowakumba watoto katika vita vinavyoendelea nchini
Syria.
Shirika hilo limekusanya ushahidi kutoka kwa watoto waliotoroka vita na ambao wameelezea dhulma na mateso waliyokumbana nayo.Shirika hilo linasema kuwa limehoji mtoto mwenye umri wa miaka 15, aliyechomwa kwa sigara,wakati alipokuwa amefungwa katika iliyokuwa shule yake.
Mtoto mwingine alizungumzia kupigwa na umeme huku akiishi katika chumba kimoja na maiti.
Ingawa shirika hilo halikutoa taarifa rasmi kuhusu nani aliyetenda mateso hayo, limeisisitizia Umoja wa Mataifa kuchukua hatua dhidi ya wanaotenda dhulma hizo.
No comments:
Post a Comment