Wanaharakati nchini
Uingereza wanataka kampuni ya Trafigura kufunguliwa mashtaka kwa hatua
yake ya kutupa taka yenye sumu nchini Ivory Coast mwaka 2006.
Uchunguzi wa miaka mitatu wa mashirika ya
Amnesty International na Greenpeace umeonyesha udhaifu wa serikali za
Magharibi kushindwa kuzuia kumwagwa kwa taka yenye sumu nchini Ivory
Coast mwaka 2006.Watu elfu mia moja walikwenda hospitali kwa matibabu. Wanaharakati hao wanateta kuwa serikali za Uingereza na Uholanzi zimeshindwa kuzuia kumwagwa kwa sumu au kuwawajibisha Trafigura.
Kampuni hiyo imekanusha madai hayo na kusema kuwa ripoti hiyo ina taarifa zisizo za kweli.
Kampuni hiyo ni mojawapo ya kampouni kubwa duniani za usafiri na imekuwa ikijitetea ikisema kuwa taka hiyo haikuwa na na sumu na wala haikuhatarisha maisha ya watu.
Mnamo mwezi agosti mwaka 2006, familia kadhaa mjini Abidjan ziliamka na kukumbana na harufu mbaya yenye mvuke wa sumu.
Taka hizo za kemikali zilikuwa zimeletwa katika eneo hilo kwa meli ya kampuni iliyokuwa imekodiwa na kampuni ya Trafigura na kisha kutupa taka hizo katika eneo lenye taka.
Kampuni hiyo imekana kuwa taka hizo zingeweza kusababisha ugonjwa na kuelezea kuwa ilikuwa imelipa kampuni moja mwenyeji kuweza kutupa taka hiyo kwa njia sawa kisheria.
No comments:
Post a Comment