Katibu mkuu wa
Umoja wa mataifa, Ban Ki Moon ameandaa mkutano maalum mjini New York
kujadili mzozo unaokumba Mali ambako wapiganaji wa kiisilamu wameteka
eneo la Kaskazini mwa nchi hiyo.
Nchi kadhaa za Afrika Magharibi pamoja na
Ufaransa zinataka azimio la Baraza la usalama la umoja wa mataifa,
litakalo wawezesha kuunga mkono hatua za kijeshi dhidi ya kile
wanachokiita magaidi wa Kaskazini mwa Mali.Rais wa Ufaransa, Francois Hollande, aliambia mkutano wa baraza kuu la umoja wa mataifa, Jumanne, kuwa Ufaransa iko tayari kuunga mkono juhudi za kuirejeshea Mali hadhi yake kama nchi huru.
Jeshi la pamoja la nchi za Magharibi mwa Afrika lijulikanalo kama ECOMOG, na ambalo limewahi kuingilia kati mizozo katika baadhi ya nchi za Afrika, linasema kuwa takriban wanajeshi elfu tatu, wana kibarua cha kutwaa eneo la Kaskazini kutoka kwa wapiganaji hao.
Lakini mwandishi wa BBC anasema kuwa viongozi wa Afrika wanatafuta uungwaji mkono kutoka kwa Baraza la usalama la umoja wa mataifa kabla ya kupeleka wanajeshi huko.
No comments:
Post a Comment