Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR –Mageuzi) David Kafulila akichangia bungeni kuhusu namna bora ya ukusanyaji wa mapato kupitia kodi zinazotozwa kwenye makampuni ya simu nchini ili kuongeza mapato ya serikali leo mjini Dodoma.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugay akitoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali zilizowasilishwa na wabunge wakati wa kikao cha tano cha mkutano wa sita leo mjini Dodoma.
Waziri na Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Mponda (kushoto) akizungumza jambo na Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kulia) ndani ya ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma. Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Stephen Wasira (katikati ) na Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama kwenye Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma leo.
Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha Gregory Theu (kushoto) akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika Christopher Chiza (kulia) nje ya ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.
Waziri wa Fedha Mustapha Mkulo (kulia) akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kwa wabunge mara baada ya kumalizika kwa kikao cha tano cha mkutano wa sita leo mjini Dodoma. Kutoka kushoto ni mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe na Davidi Kafulila (wa pili kutoka kushoto) kutoka Kigoma Kusini.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Mwenyekiti wa Kampuni ya MAAT International ya Spain, Bw. Santiago Jimenez Barull kabla ya mazungumzo yao, Ofisini kwake, Bungeni mjini Dodoma leo. Kampuni hiyo inakusudia kuwekeza nchini katika kilimo na madini. Katikati ni Mbunge wa Wawi na mwenyeji wa Mgeni huyo, Mh. Hamad Rashid.
No comments:
Post a Comment