HABARI zilizotua Risasi Jumamosi muda mchache kabla gazeti halijakwenda mtamboni zinadai kuwa, staa wa sinema za Kibongo, Steven Kanumba (pichani) anataka kuoa, lakini amechimbwa mkwara na mama yake mzazi kwamba asithubutu kuangukia kwa staa, ‘itamkosti’.
Kwa mujibu wa chanzo, siku za karibuni, staa huyo amekuwa akizungumzia suala la kuoa lakini ugumu upo kwenye masharti ya mama yake.
“Jamaa (Kanumba) kila siku anazungumzia kuoa, lakini anasema ameshaambiwa na mama yake, asije akampelekea hawa mademu mastaa wa Bongo, kwani wana presha,” kilisema chanzo.
Kikaongeza: “Kwa vyovyote vile mama yake atakuwa anataka akaoe kijijini kwao, Shinyanga huko. Sasa unavyomjua Kanumba kweli ataweza kuishi na mwanamke asiyekuwa na jina kubwa?”
Habari hazikuishia hapo, ikadaiwa kuwa mama yake alishamuwekea wazi Kanumba kwamba hakubaliani na mastaa wa kike Bongo kwa kuoa, labda kujirusha tu.
Hata hivyo, inasemekana kuwa Kanumba hajaweka wazi msimamo wake kwa mama yake mzazi.
Baada ya kupata taarifa hizo, Risasi Jumamosi lilimvutia waya Kanumba ili kumuuliza kuhusu madai hayo ambapo alifunguka:
“Sikia, kwa sasa sijafikiria na wala sina mpango wa kufunga ndoa, ila siku itafika nitafunga ndoa kwa mwanamke ambaye atampendeza Mungu, awe staa asiwe staa. Awe tajiri asiwe tajiri ni huyo huyo nitaoa.
“Kuhusu suala la kupangiwa na familia nikaoe kijijini, hilo sikubaliani nalo kwani mimi ndiyo mwenye uamuzi, kwa sababu mke nitaishi naye mimi.”
Alhamisi ya Februari 2, 2012 nyumbani kwa mama yake Kanumba, Temeke, Dar binti mmoja aliyekuwa akitoka nje, aligongana uso na Risasi Jumamosi, mahojiano yakawa hivi:
Risasi: (baada ya salamu) “tuna shida na mama yake Kanumba.”
Binti: “Ametoka.”
Risasi: “Amekwenda wapi?”
Binti: “Sijui alikokwenda wala muda wa kurudi.”
Risasi: “Sisi tunataka kumuuliza ishu ya maana kuhusu mwanaye Kanumba, kwa hiyo tusaidie hata namba yake ya simu.”
Binti: “Sijaishika kichwani.”
Kanumba ameshawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mastaa kadhaa wa Bongo huku ikiaminika kuwa, mmoja wao alitaka kumuoa kama wasingezinguana katikati ya safari yao.
No comments:
Post a Comment