My Web

Emmanuel

CONTACT

Tuesday, February 28, 2012

Hatimae Noti ya Sh 500 kubadilishwa kuwa katika sarafu



BENKI Kuu ya Tanzania (BoT), imeanza mchakato wa kufanyia mabadiliko ya noti mpya ya Sh500, ili iwe ya sarafu baada ya kujiridhisha kuwa inachakaa kwa haraka zaidi.

Akizungumza na gazeti hili jana kwa njia ya simu kutoka Arusha, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndulu, alisema mchakato kuifanyia mabadiliko na noti hiyo ili iwe katika sarafu, inazingatia ukweli kwamba fedha iliyoko katika mzunguko mkubwa katika jamii.

Profesa Ndulu alisema noti ya Sh500 inatumika kwa kiasi kikubwa na wananchi wengi, jambo linalosababisha kuchakaa haraka kabla ya wakati uliopangwa.

“Tunafanya mchakato wa mabadiliko ya noti hizi zinazochakaa kwa haraka kwa sababu zenyewe zinatumika zaidi,” alisema Profesa Ndulu.

Alisema hatua hiyo haitaathiri mzunguko wa fedha na kwamba sarafu ya Sh500 itakapoanza kutumika, noti hiyo itaondoka polepole.

Alisema sarafu hiyo ya Sh 500 itaanza kupatikana katika kipindi kifupi kijacho na kuwawezesha wananchi kuitumia.
“Watanzania wasishituke mabadiliko hayo ya noti za Sh500 kwenda sarafu maana hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kwa watoa chenji,”alisema.

No comments:

Post a Comment

New