Robin van Persie akiwa na tuzo yake ya mtu wa kwanza kufikisha magoli 20.
MCHAWI wa soka wa timu ya Arsenal ya Uingereza, Robin van Persie, jana alitunukiwa tuzo ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga magoli 20 katika ligi kuu ya Uingereza msimu huu unaoendelea.
Van Perseie ambaye ndiye kepteni wa Arsenal alizawadiwa tuzo hiyo huko London Colney, kufuatia timu yake kuifunga Blackburn magoli 7-1 kwenye Uwanja wa Emirates, Jumamosi ambapo alifunga magoli matatu na kufikisha magoli 22 katika mechi 24 ilizocheza timu hiyo.
Mchezaji huyo pia alikuwa wa kwanza kufikisha magoli 10 ambapo alifikisha idadi hiyo alipofunga magoli matatu ambapo timu yake iliishinda Chelsea kwa magoli 5-1 kwenye dimba la Stamford Bridge mwezi Oktoba mwaka jana.
Magoli 22 ya Van Persie yameweka pengo la magoli sita kati yake na Demba Ba wa Newcastle United, na pengo la magoli saba kati yake na Sergio Aguero wa Manchester City na Wayne Rooney wa Manchester United.
No comments:
Post a Comment