PINDA ATAKA WANA CCM KUWANYIMA KURA WANAOTUMIA PESA KUOMBA NAFASI
WAZIRI mkuu Mizengo Pinda ataka wana CCM wanaotumia nguvu ya pesa kusaka uongozi ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kutoapewa nafasi wanazoomba kama njia ya kukijenga chama chenye viongozi waadilifu .
Pinda ambaye ni mlezi wa CCM mkoa wa Iringa ametoa kauli hiyo leo wakati akiwahutubia wana CCM na wakereketwa na CCM na wananchi wa jimbo la Iringa mjini katika kumtano wake wa hadhara katika viwanja vya Kihesa mjini hapa .
Akiwa jimbo la Iringa mjini Pinda amepata mapokezi makubwa kutoka kwa wana CCM na vyama vingine ambao walifika kumsikiliza tofauti na ilivyotegemewa kuwa kutokana na jimbo hilo kuwa ni ngome ya Chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema) yawezekana Pinda angeambulia patupu katika mkutano wake huo.
Kwani alisema kuwa rushwa ndogo ndogo ndani ya CCM ndizo ambazo zimeendelea kukifanya chama hicho kuyumba siku hadi siku na hivyo kudai kuwa uchaguzi wa mwaka huu ni muhimu kwa chama hicho kurekebisha makosa hayo ili kiwe na nguvu zaidi katika kujipanga .
Alisema ndani ya CCM kuna makundi ya baadhi ya wanachama yanazidi kujengeka ambayo pamoja na kutofaa kuchaguliwa kuwa viongozi hawataki kuambiwa hawafai.
Alisema kuwa Kiongozi safi hawezi kupatikana kwa kutoa rushwa tena inayodhalilisha utu wa wana CCM rushwa ya kati ya Sh 1000, Sh 500 na kutaka wana CCM kuchangua viongozi wenye sifa safi wasio tumia pesa kuwanunua
Pinda aliwataka wanachama wa chama hicho kuwaadhibu kwa kuwanyima kura wale wanatumia fedha kununua uongozi.
Akiwashukuru wananchi wa mjini Iringa waliojitokeza kumpokea na kumsikiliza Waziri Mkuu, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) anayewakilisha mkoa wa Iringa Profesa Peter Msolla alikumbusha makosa yaliyofanywa na chama hicho mjini Iringa hadi yakasababisha jimbo la Iringa Mjini lichukuliwe na Chadema.
“Tunafahamu tulipojikwaa mpaka tukapoteza jimbo hili, hata hivyo tunawahakikishieni tunazidi kujipanga kwa nguvu zetu zote kulirudisha mikononi wa CCM ili mkoa wa Iringa uendelee kuhesabika kama ngome kuu ya CCM,” alisema.
No comments:
Post a Comment