Sikuzani Kibwana akiwa amelazwa nje kupata ubaridi.
Mwanafunzi mwenzake akimsubiri azinduke.
Mandhari ilivyo nje ya chumba cha Intanet.
MWANAFUNZI aliyekuwa kidato cha nne Shule ya Sekondari Morogoro inayomilikiwa na serikali, Sikuzani Kibwana, leo ameanguka ghafla na kupoteza fahamu katika chumba cha Intanet baada ya kusoma matokeo na kujikuta amefanya vibaya kwenye mtihani huo ambapo alioongozana nao wote wakiwa wamefanya vizuri.
Mwandishi wetu alishuhudia tukio hilo kwenye chumba cha Intanet cha Valentenes karibu na Uwanja wa Jamhuri katika Manispaa ya Morogoro ambapo wanafunzi wa shule mbali mbali walikuwa bize kuangalia matokeo ya kidato cha nne mwaka 2011 yaliobandikwa jana kwenye mtandao na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA).
Mwanafunzi huyo alianguka na kupoteza fahamu na kuzua taharuki kubwa kwa watu wote waliokuwemo ndani ya chumba hicho.
Wanafunzi wenzake walimtoa nje ili apigwe ubaridi na kuwapigia simu wazazi wake.
Hadi mtandao huu unaondoka hapo, mwanafunzi huyo alikuwa bado hajazinduka.
No comments:
Post a Comment