Na Mwandishi Wetu
UTAFITI uliofanywa na Chuo Kikuu cha Tiba cha Johns Hopkins, Marekani, umegundua ukweli kuhusu chanjo ya Ukimwi kuwa matumizi ya dawa za kurefusha maisha (ARV) yanaweza kuwafanya waathirika wa Virusi vya Ukimwi (VVU) kukutana kimwili na wapenzi wao bila kondomu na wasiwaambukize ugonjwa huo.
Aidha, kuna taarifa za kitaalamu kutoka katika chuo hicho zinasema wataalamu hao waliofanya utafiti katika majaribio kwenye sehemu mbalimbali za dunia, wamebaini kuwa mtu ambaye anatumia dawa za kurefusha maisha, anaweza kufanya tendo la ndoa bila ya kutumia kondomu na mtu ambaye hana Ukimwi na asiweze kumuambukiza kwa asilimia 95.
Mkuu wa Mtandao wa Maabara za Kuchunguza VVU katika chuo hicho, Profesa Susan Eshleman, alifafanua kuwa wamebaini dawa za kurefusha maisha (ARV) kwa waathirika wa HIV kama mtumiaji atatumia kikamilifu , zinaweza kutumika kama sehemu ya kuzuia maambukizi kama muathirika atajamiiana bila kutumia kondomu.
“Matokeo haya yameleta mwanga mpya katika sayansi ya kuzuia maambukizi na inawaweka watafiti kwenye mazingira mazuri zaidi ya kupata suluhisho la kukabiliana na maradhi haya,”alisema Profesa Eshleman ambaye hata hivyo aliwashauri waathirika wanaotumia ARV kuendelea kutegemea kondomu kama moja ya njia za kuzuia maambukizo mapya.
No comments:
Post a Comment