Mshituko! Katika hali isiyotarajiwa, mwanamuziki Judith Daines Wambura Mbibo a.k.a Lady Jaydee au Jide, (pichani) amewahuzunisha mashabiki wake baada ya kuonesha picha ya jeneza lake litakavyokuwa siku akiaga dunia.
LIWE NA RANGI ZA ZAMBARAU NA NYEUPE
Kupitia ‘blogu’ yake, Jide alitundika picha mbili za jeneza lenye rangi za zambarau na nyeupe, akiambatanisha na maelezo kuwa yuko mbioni kuwadondoshea simulizi kamili ya tukio hilo litakavyokuwa kupitia wimbo wake mpya.
Risasi Jumamosi liliinyaka ishu hiyo sekunde chache baada ya Jide kufanya tukio hilo Februari Mosi, mwaka huu, saa 8: 10 mchana.
SIMULIZI KAMILI INAKUJA
Pamoja na picha hizo, Jide aliandika: “Siku ikifika langu liwe la rangi hii, halafu simulizi kamili ya story nzima kuwa nataka iweje, ziko kwenye wimbo wangu mpya.
“Mpaka kuhusu nani awepo na nani asiwepo na nini kifanyike, nani achukue nini na nani afanye nini, stay tuned.”
MASHABIKI WAJAWA MAJONZI
Muda mfupi baada ya tukio hilo, ndani ya mtandao huo kulikuwa kama msiba ambapo mashabiki wake walipata nafasi ya kuweka maoni yao wakionesha kuhuzunishwa na kitendo hicho.
Baadhi ya mashabiki walikwenda mbali zaidi wakieleza waziwazi kuchukizwa na jambo hilo alilolifanya staa wao wanayempenda.
“Da’ Jide mi’ siku zote huwa napenda kutembelea blog yako na huwa nachingia sana bila kujitambulisha kwa kuwa wewe ni mtu ninayekutegemea katika maisha yangu.
“Wewe ni kama kioo changu, ila hili uliloandika kwa kweli halijanibariki, limenihuzunisha na kunisikitisha sana.
“Najua sote tupo njia hiyo, lakini kwa nini leo umeamua kutuandikia hivyo? Naomba mipango ya shetani ishindwe! Mungu wetu ni mwaminifu sana na nakutabiria utaishi miaka mingi hadi ufikiwe hiyo rangi haitakuwepo. Uwe na amani dada,” ilisomeka sehemu ya maoni hayo iliyoungwa mkono na mashabiki wake wengi waliojawa na simanzi.
KWANI JIDE YUKO WAPI?
Hivi karibuni Jide anayejipanga kuachia albamu yake ya tano inayoitwa Ya Tano aliripotiwa kuwa nchini Ufaransa ambapo amekuwa akionekana kwenye picha akiwa sehemu tofauti nchini humo.
NI MJAMZITO?
Bado mitandao mingi Bongo imekuwa ikidai kuwa pamoja na kuwa masomoni Ufaransa, lakini ana kila dalili za kuwa na kibendi, jambo ambalo yeye au mumewe Gardner G. Habbash ‘Kaputeini’, hawajawahi kulithibitisha.
No comments:
Post a Comment