My Web

Emmanuel

CONTACT

Thursday, April 12, 2012

George Zimmerman charged with 2nd degree murder - INFOWARS.COM





.

Waombolezaji wa kikundi cha New Black Panthers wakiandamana kupinga kifo cha Trayvon huko Florida.
Thai Nguyen, 31, akishiriki maandamano hayo ya Washington.

Waombolezaji wa kifo cha Trayvon Martin wakiwa na mishumaa huko Sanford, Florida, Machi 25, mwaka huu.

Mtuhumiwa wa mauaji. George Zimmerman katika picha iliyopigwa Julai 2005.

MZUNGU aliyempiga risasi na kumwua kijana mweusi nchini Marekani, amefunguliwa mashitaka ya mauaji kiwango cha pili.

Mwendesha mashitaka wa jimbo la Florida, Angela Corey, amethibitisha kwamba George Zimmerman (28) amefunguliwa mashitaka ya kumwua Trayvon Martin (17).

Corey alisema baada ya mauaji hayo, muuaji alitoroka hadi alipokamatwa baada ya yeye kujipeleka polisi.

Mauaji hayo yameibua malalamikomakubwa nchini Marekani ambapo inadaiwa Trayvon alikuwa hana silaha yoyote wakati anauawa.

Awali, polisi walikataa kumkamata Zimmerman wakisema alikuwa analindwa na sheria ya jimbo hilo (Florida) ambayo inamruhusu mtu kutumia nguvu kujilinda iwapo anaona anatishiwa.

Hata hivyo, malalamiko hayo makubwa kutoka kwa umma – akiwemo Rais Obama wa Marekani – yaliilazimu timu ya Corey kufikiria upya uamuzi huo na kuona kama kulikuwa na kesi ya kujibu katika tukio hilo.

Hukumu kwa kosa la mauaji ya kiwango cha pili ni miaka 22 jela.

Akihojiwa, Zimmerman alisema alimwua kijana huyo ka vile alionekana “kutia mashaka”.

Watetezi wa mtuhumiwa huyo wanasema marehemu ndiye aliyeshambulia kwanza akaivunja pua ya Zimmerman kabla ya kumpiga na kumwangusha chini.

Katika jimbo la Florida, mtu anaruhusiwa “kujitetea” iwapo anaamini anakabiliwa na hatari ya kifo au madhara ya kimwili

No comments:

Post a Comment

New