Kamanda wa polisi katika mkoa wa kipolisi wa Kinondoni Charles Kenyela ametoa kauli ya mwisho baada ya taarifa kuenea jana wakati wa msiba wa Kanumba kupitia sms, facebook & twitter kwamba kuna watu wamepoteza maisha baada ya kuzimia kwenye msiba huo.
Kenyela amesema “huo ni uvumi tu baada ya watu kuona watu wengi wakidondoka, sasa kwa imani zao wakadhani kwamba wamefariki lakini ukweli ni kwamba wengi walipewa msaada hapohapo na watu wa RedCross na wengine walipata nafuu wakiwa njiani kupelekwa hospitali, waliofikishwa hospitali walikua 10, mmoja alipelekwa Muhimbili na kuruhusiwa baadae na wengine tisa walipelekwa Mwananyamala na wameruhusiwa tayari”
“Mpaka sasa hivi hakuna taarifa yeyote ya mtu kufariki au kupata matatizo yoyote hata ya kuibiwa, hakuna… japo watu walikua wengi zaidi ya mategemeo na kwa umati huo pengine ulikua unafaa kutengewa eneo kubwa labda uwanja wa taifa, ndio maana ule msongamano ulichangia watu kuzimia kwa kupata mshituko na hata joto lenyewe lilichangia sana” – Kamanda Kenyela.
Katika sentensi nyingine Kamanda Kenyela amesema ni ngumu kukisia idadi ya waliofika kwenye viwanja vya leaders kumuaga Kanumba ila ni zaidi ya watu elfu ishirini na tano, huku akithibitisha kwamba wengi walikosa nafasi na kuamua kuondoka kwenye eneo hilo.
Kutokana na watu kuwa wengi na time kusogea, ilitangazwa na MC kwamba watakao husika kuuaga mwili wa Kanumba ni baadhi ya viongozi wa serikali waliokuwepo akiwemo Makamu wa Rais pamoja na Familia ya Marehemu tu, wananchi wengine waliambiwa wajipange kwenye barabara ya Tunisia na gari hilo litapita wataona jeneza la Kanumba
No comments:
Post a Comment