PICHA za Bi Harusi mtarajiwa ambaye ni modo sexy Bongo, Jacqueline  Patrick ‘Jack’ hivi karibuni zimenaswa akiwa katika mapozi ya kimahaba  na mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Martin.
Picha hizo ambazo zipo kwenye mtandao zinawaonesha wawili hao  wakijiachia kwenye Ufukwe wa Mbalamwezi uliopo Mikocheni jijini Dar es  Salaam, mazingira yaliyosababisha baadhi ya watu kuhoji juu ya ukaribu  wao huo.
“Mh! Huyu si ndiyo anatarajiwa kuolewa hivi karibuni? Sasa huyu mwanaume  ni nani tena, au ndiyo mchumba wake?” alihoji mdau mmoja baada ya  kuziona picha hizo.
Katika kujua uhusiano uliopo kati ya wawili hao, mwandishi wetu  alimtafuta Jack kupitia simu yake ya mkononi lakini hakuweza kupatikana  mara moja.
Martin alipopatikana alisema: “Picha hizo tulizipiga siku tuliyokuwa  tunaandaa matangazo flani hivi, ila hazina maana yoyote mbaya, Jack ni  mshikaji wangu wa kawaida tu.”
Jack ambaye ni Miss Ilala namba 3, 2005 anatarajiwa kuolewa hivi karibuni ambapo vikao vya harusi vimeshaanza.
No comments:
Post a Comment