Mwanadada Nguyen Thi Phuong alivyokuwa kabla ya kutumia dawa za asili.
Nguyen Thi Phuong alivyo baada ya kutumia dawa za asili.
NGUYEN Thi Phuong ni mwanadada mwenye asili ya Vietnam, ukimuangalia huenda ukadhani ni bibi wa miaka 73 lakini ni binti mdogo mwenye umri wa miaka 26.
Mrembo huyo, aligeuka mzee mwaka 2008 na kwa mujibu wa madaktari, tatizo hilo amelipata baada ya kutumia dawa za asili.
Wakati anakutwa na tatizo hilo, Nguyen alikuwa na umri wa miaka 23. Kipindi hicho alikuwa mrembo mwenye sura ya kuvutia lakini hivi sasa hana raha, kwani sura yake ni ya kikongwe.
Pamoja na madaktari kusema hivyo, Nguyen anaamini kuwa hali aliyonayo imesabishwa na aina ya samaki wa baharini aliokuwa anakula ambao ndiyo wamemsababishia mzio (aleji) mwilini.
Nguyen akiwa na mumewe, Thanh Tuyen.
Mume wa Nguyen, ambaye ni fundi seremala, Thanh Tuyen, alisisitiza kuwa pamoja na mkewe kuzeeka, bado anampenda kama zamani.
Tuyen alisema, kinachomsikitisha ni kwamba yeye na mkewe hawajapata mtoto na kutokana na hali ngumu kiuchumi aliyonayo, hajui kama Nguyen anaweza kupona na kushika ujauzito, kwani hivi sasa ni kama amezeeka.
Kutokana na namna Nguyen alivyoharibika, amekuwa akitembea amevaa kinyago (maski) ili kuficha uso wake.
“Wakati naanza kuumwa nilikuwa najisikia maumivu mwili mzima, pia nilikuwa nawashwa wakati wa kulala,” alisema Nguyen.
Nguyen aliendelea kusema kuwa baada ya maumivu aliamua kutafuta dawa kwenye maduka ya madawa ya kawaida kwa sababu yeye na mume wake hawana uwezo wa kununua dawa zinazofaa kwa sababu ya umaskini.
NI UGONJWA GANI?
Madaktari wanafafanua kuwa ugonjwa alionao Nguyen unaitwa Lipodystrophy ambao husababisha kuyeyuka kwa mafuta ya chini ya ngozi, hivyo kusinyaa na mhusika kuonekana mzee.
Wataalamu hao wamesema kuwa mwili wa Nguyen una kiwango kikubwa sana cha cortisol iliyotokana na mitishamba.
Ugonjwa huo unatajwa kuwapata wanawake wengi ambao wana umri kati ya miaka 20 na 40.
Daktari Vo Thi Bach Suong wa Hospitali ya HCMC, amejitolea kumsaidia Nguyen kwa kumpa matibabu yatakayomuwezesha kupona kabisa.
No comments:
Post a Comment