Taifa Stars yakosa mechi ya kujipima nguvu; kuiva morocco wiki ijayo:
Shirikisho la Soka nchini (TFF) limeshindwa kuipatia timu ya Taifa ya Tanzania mechi ya kirafiki ili kuiandaa kwa mchuano wa marudiano na timu ya Morocco. Timu ya Taifa ilikuwa inahitaji kucheza mechi ya kirafiki japo moja kabla ya kurudiana na Morocco Oktoba 8, 2011. Mashindano haya ni ya kutafuta tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Mataifa ya Africa (Africon 2012) ambayo yatakapofanyika ndio yataamua ni nchi gani za Afrika zitaenda kucheza kwenye mashindano ya Kombe la Duniani mwaka 2014.
Kutokana na tamko hilo hapo jana kwamba TFF imekosa mechi ya kirafiki ambayo ingeweza kupima uwezo wa vijana hao kabla ya kusafiri kwenda huko Morocco hivyo timu hiyo itaenda huko ikiwa haijajipima uwezo wake wala kufanya masahihisho muhimu kabla ya mechi hiyo nzito.
Mechi hii dhidi ya Morocco itakuwa inafuatia mechi ya kundi D. Mechi iliyotangulia (katika makundi) ilikuwa ni kati ya Taifa Starts na Algeria ambapo zilitoka sare ya kufungana bao 1-1 kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar.
Kundi D la mashindano hayo linahusisha timu za Algeria, Morocco, Tanzania na Jamhuri ya Africa ya Kati (Central Africa Rep). Kila Timu imeshacheza mechi tano mpaka sasa huku Morocco ikiwa kileleni kwa pointi 8 na magoli 4, nafasi ya pili ikishikwa na Jamhuri ya Kati ikiwa na pointi 8 na magoli 2, Tanzania Imeshika Nafasi ya tatu kwa pointi 5 na ikidaiwa Bao 1 na Algeria ikishika Mkia na imepata pointi 5 na deni la magoli 5.
Mechi hii dhidi ya Morocco inaweza kuwa Ngumu zaidi kwa timu yetu ya Taifa kwa kuwa Morocco ni timu kongwe sana na yenye uzoefu mkubwa katika Michuano hii. Lakini kuna matumaini makubwa sana kwa timu yetu ambayo kwa siku za karibuni imekuwa na maendeleo mazuri. Endapo Tanzania itaishinda Morocco ugenini basi itajiweka katika mazingira mazuri ya kusonga mbele na hatimaye kucheza katika fainali hizo za Africon.
Mechi Iliyopita ilimailizika Tanzania Ikifungwa bao 1-0 Mounir El Hamdaoui akipata Goli la ushindi kwa Morocco na lilitengenezwa na Mchezaji wa Arsenal Marouane Chamakh. Video – Tanzania 0-1 Morocco
Tanzania Imecheza Mechi 5, imeshinda 1, Sare 2 na imefungwa mechi 2.
Morocco wamecheza Mechi 5, wamechinda 2, sare 2 na Wamefungwa 1.
Tunategemea Kuona utendaji mzuri kutoka kwa washezaji kama Mbwana Samatta, Henry Joseph, Nahodha Nsajigwa, Nizar Khalfan, Mrisho Ngassa na kadhalika Katika mechi hiyo dhidi ya Morocco.
Kikosi Cha Morocco Kilicho Itwa:
Makipa – Nadir Lamyaghri, Ahmed Mohamadina, Issam Badda.
Mabeki – Abdelhamid El Kaoutari, Michael Chretien Basser, Mehdi Manatia, Jamal Alioui, Badr El Kaddouri, Ayoub El Khaliqi, Rachid Soulaimani, Moustapha Lamrani.
Viungo - Adel Taarabt, Houssine Kharja (Captain), Younès Belhanda, Mohammed Berrabeh, Mohammed Chihani, Karim El Ahmadi, Oussama
Washambuliaji - Marouane Chamakh, Youssouf Hadji, Youssef El- Arabi na Mounir El Hamdaoui.
Kikosi Cha Taifa Stars Kilichoitwa:
Makipa - Shabani Dihile (JKT Ruvu Stars), Juma Kaseja (Simba) na Shabani Kado (Yanga).
Mabeki – Shadrack Nsajigwa Captain (Yanga), Erasto Nyoni (Azam), Idrissa Rajab (Sofapaka, Kenya) na Amir Maftah (Simba), Aggrey Morris (Azam), Juma Nyoso
(Simba) na Victor Costa (Simba).
Viungo – Henry Joseph (Kongsvinger IL, Norway), Nurdin Bakari (Yanga), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar) na Jabir Aziz (Azam), Nizar Khalfan (Vancouver Whitecaps,
Canada), Mrisho Ngassa (Azam) na Ramadhan Chombo (Azam).
Washambuliaji - Abdi Kassim (DT Long An, Vietnam), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC), Dan Mrwanda (DT Long An, Vietnam), Athuman Machupa (Vasalund IF, Sweden), John Bocco (Azam) na Hussein Javu (Mtibwa Sugar).
Mechi hii itakayochezwa wiki ijayo kwenye mji wa Marrakech – Morocco.
**Hivi sasa, Tanzania imeshika nafasi ya 126 katika ‘FIFA/Coca Cola Rankings‘ na Morocco ikiwepo katika nafasi ya 59 duniani
No comments:
Post a Comment