Lulu akiwa na mama yake, Bi. Lucresia Karugila.
Na Rhobi Chacha
NYOTA wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ (pichani chini),  amefunguka na kuweka wazi kwamba anajutia maisha yake ya nyuma, hasa  kitendo cha kuwa anamtoroka mama yake usiku na kwenda kufanya starehe na  kumuomba msamaha, aya zinazofuata zinaweka wazi ishu nzima.
Akizungumza na mwandishi wetu jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki  iliyopita, Lulu alisema kuwa kila akikumbuka vitendo hivyo anaumia sana  kwa vile amebaini alikuwa akimkosea mama yake.
Alisema ameamua kumwomba msamaha mama yake na anaamini atasamehewa kwa sababu siku zote mama atabaki kuwa mama.
“Kiukweli kutoka moyoni ninalazimika  kumwomba msamaha mama yangu mzazi kutokana na makosa niliyokuwa nikimfanyia hapo awali.
“Hakuna kitu kinachoniumiza kama kitendo cha kumtoroka usiku na kwenda  kwenye starehe. Mama popote ulipo naomba msamaha, mimi mwanao  nilikukosea sana,” alisema Lulu.
Hata hivyo, Lulu alisema kwamba kwa umri alionao sasa (miaka 18), mama yake anamwamini ipasavyo kwa kila anachokifanya.
Mwaka jana, Lulu mbali na skendo nyingine kwenye vyombo vya habari, pia   alivuma sana kutokana na tabia yake ya kupatikana kwenye kumbi za  sterehe akiwa na umri wa miaka 17.
No comments:
Post a Comment