Na Brighton Masalu.
WEMA  Isaac Sepetu (pichani), mwenye kibendi cha miezi miwili kasoro  alichopachikwa na ‘kidume’ Naseeb Abdul Jumaa ‘Diamond’, amegeuka kero  kwa baadhi ya mastaa Bongo hasa wa kike kutokana na kutema mate ovyo,  kujichetua na kuinadi mimba yake kupita maelezo.
Akizungumza na  The Biggest IQ Paper, Ijumaa Wikienda ndani ya Viwanja vya Leaders Club,  Kinondoni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita, Wema  alisema kuwa kinachosababisha awe kero ni dalili za wazi za mjamzito  alizonazo ikiwemo kutema mate ovyo, kubagua vyakula na kudeka  kupitiliza.
Alifunguka: “Wanasema nawakera, lakini nahisi wananionea gere na mimba yangu. Mimi sina chuki na mtu yeyote na naomba…
Na Brighton Masalu.
WEMA  Isaac Sepetu (pichani), mwenye kibendi cha miezi miwili kasoro  alichopachikwa na ‘kidume’ Naseeb Abdul Jumaa ‘Diamond’, amegeuka kero  kwa baadhi ya mastaa Bongo hasa wa kike kutokana na kutema mate ovyo,  kujichetua na kuinadi mimba yake kupita maelezo.
Akizungumza na  The Biggest IQ Paper, Ijumaa Wikienda ndani ya Viwanja vya Leaders Club,  Kinondoni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita, Wema  alisema kuwa kinachosababisha awe kero ni dalili za wazi za mjamzito  alizonazo ikiwemo kutema mate ovyo, kubagua vyakula na kudeka  kupitiliza.
Alifunguka: “Wanasema nawakera, lakini nahisi  wananionea gere na mimba yangu. Mimi sina chuki na mtu yeyote na naomba  wanivumilie.”
No comments:
Post a Comment