Chadema imeibuka kidedea baada ya ya mgombea wake Bw. Joshua Nassari kushinda kiti cha ubunge wa jimbo la Arumeru Mashariki kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika jana. Msimamizi wa Uchaguzi huo Bw Trasence Kagenzi amemtangaza rasmi mgombea wa Chadema Bw. Nassari kuwa mshindi kwa kumshinda mpinzani wake mkubwa, Sioi Sumari wa CCM.
Kwa mujibu wa msimamizi wa uchaguzi huo, jumla ya watu 120,000 walijiandikisha kupiga kura. Jumla ya waliojitokeza kupiga kura ni 60,038. Jumla ya kura zilizoharibika ni 661. Nassari Joshua amepata jumla ya kura 32,972 akifuatiwa na mpinzani wake mkuu Bw. Sioi Sumari wa CCM aliyepata kura 26,757.
Wagombea wengine wamepata kura kama ifuatavyo. Mazengo Adam (AFP) 139, Charles Msuya (UDP) 18, mgombea wa TLP 18, Kirita Shauri Moyo (SAU) 22, Hamisi Kiemi (NRA) 35, na Mohammed (DP) 77.
Katibu wa Chadema Dr Wiilibrord Slaa amewashukuru wana Arumeru Mashariki kwa imani yao kwa Chdema hasa kwa kijana Joshua Nassari. Akiandika kwenye mtandao wa Facebook, Dr Slaa amesema: " Ushindi wao ni ushindi wetu sote. HONGERA SANA JOSHUA. Mungu mbariki JOSHUA, Mungu ibariki Tanzania."
Naye naibu Katibu wa Chadema ambaye pia ni mbunge wa Ubungo amewapongeza wananchi wa Arumeru Mashariki kwa kudhihirisha kuwa uongo, ufisadi na usanii hauwezi kushinda ukweli, uadilifu na umakini। Akiandika kwenye mtandao wa Facebook, Mh Mnyika amewashukuru wana Arumeru kwa kuunganisha nguvu ya umma na Wana Chadema wote waliongoza mapambano mpaka kupata ushindi. Pia amewashukuru kwa kuongezea Chadema nguvu ya kuwawakilisha bungeni kwa sasa, na kuongeza kuwa ushindi huu ni ishara ya ushindi wa 2015.
No comments:
Post a Comment