Rais wa Malawi, Bingu wa Mutharika enzi za uhai wake.
RAIS wa Malawi, Bingu wa Mutharika, amefariki baada ya shambulio la moyo, vyanzo vya hospitali na serikali ya nchi hiyo vilisema.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 78 alikimbizwa hospitali ya Lilongwe siku ya Alhamisi baada ya kuanguka na alitangazwa kuwa amefariki baada ya kufikishwa hapo. Vyombo vya habari vya serikali vilisema alikuwa amepelekwa Afrika Kusini kwa matibabu japokuwa hakuweza kufahamika mara moja kabla ya hapo alikuwa wapi.
Wananchi wengi wa Malawi wamekuwa wakiulaumu utawala wa kiongozi huyo ambaye aliwahi kuwa mchumi wa Benki ya Dunia kwa matatizo ya kiuchumi ambayo yameikumba nchi hiyo.
“Tunajua amekufa na bahati mbaya amefia katika hospitali moja ndogo, miongoni mwa hospitali ambazo alikuwa hazijali, kwani zilikuwa hazina madawa ama umeme,” alisema Chimwemwe Phiri, mfanyabiashara wa mjini Lilongwe mmoja wa wananchi wengi waliofurahia kifo chake.
Katiba ya nchi hiyo inasema Makamu wa Rais, Joyce Banda, atakuwa mkuu wa nchi hiyo japokuwa alifukuzwa katika chama tawala cha DPP cha Mutharika mwaka 2010 kuhusiana na suala la kuchukua madaraka pindi rais anapofariki au kutoweza kuendelea kutawala.
CHANZO: REUTERS
No comments:
Post a Comment