My Web

Emmanuel

CONTACT

Tuesday, July 31, 2012

ZOEZI LA KUANDIKISHA VITAMBULISHO VYA TAIFA LINA KASORO LUKUKI



Mkurugenzi wa NIDA, Dickson Mwaimu.
KWANZA tumshukuru Mungu kwa kutuweka hai leo na kubwa zaidi kwa kutuwezesha kukutana katika safu hii kwa mara nyingine tena, hakika Mungu anastahili kuabudiwa.
Baada ya kusema hayo leo nitazungumzia zoezi la uandikishaji wa vitambulisho vya taifa.
Kusema kweli zipo dalili lukuki hivi sasa zinazoonyesha kwamba zoezi hilo la kuandikisha wananchi ili wapewe vitambulisho vya uraia, halitafanikiwa, labda itokee miujiza.
Kwa kusema kweli zoezi limeanza vibaya, na inaonesha waandaaji, Mamlaka ya Vitambulisho (Nida) hawakujiandaa vya kutosha na pia hawakuwaandaa raia kuitikia wito wa kujitokeza kujiandikisha.
Babu zetu walisema ‘Siku njema huonekana asubuhi,’ lakini kwa Nida, sivyo maana shughuli yao ‘asubuhi’ yaani siku za kwanza za zoezi hilo mambo ni shaghalabaghala na wamesababisha wananchi kushindwa kujiandikisha na badala yake kusumbuka.
Nikiwa raia ninayeipenda nchi hii nafikiri nina wajibu wa kuonyesha upungufu na kufichua uozo unaoweza kukwamisha zoezi hilo muhimu lenye manufaa kwa taifa na ustawi wa watu wake.
Yapo matatizo makubwa yanayokwamisha zoezi hilo na tatizo kubwa lipo serikali kuu, haionyeshi dalili zozote za kufahamu nini kinaendelea katika mchakato mzima wa mpango huo.
Zoezi hilo nyeti linaonekana kuachwa katika mikono na mamlaka za chini za serikali za mitaa ambazo kwa kweli hazina uwezo wala nyenzo za kulifanikisha.
Kutokana na hilo wananchi wamekuwa wakiteseka na kupoteza muda mwingi kwenye foleni na wengine kushindwa kujiandikisha licha ya kutumia muda mwingi wakiwa kwenye foleni.
Katika baadhi ya sehemu taratibu zenye mkanganyiko zinatawala wakati wa kujiandikisha.
Kama hiyo haitoshi, Mamlaka ya Vitambulisho (Nida) imeonyesha udhaifu mkubwa kwa kushindwa kufahamu kuwa, ilipaswa kwanza kuendesha programu kubwa ya uhamasishaji kwa kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi kupitia vyombo vya habari.
Lakini pia waandikishaji wote walipaswa kupewa mafunzo stahiki ili kuepusha makosa na ubabaishaji ambao wananchi wanaushuhudia sehemu mbalimbali za nchi.
Uwezo wa waandikishaji wengi umeonekana kuwa chini ya kiwango na imegundulika kwamba wengi wao hawana elimu ya kutosha, matokeo yake ni kukosea majina ya wananchi wanaokwenda kujiandikisha.
Kutokana na hilo ni wazi kwamba siku ya kutolewa vitambulisho hivyo ikifika vinaweza kuwa na majina yaliyokosewa, hivyo kusababisha usumbufu mkubwa na lawama kwa serikali.
Lakini pia kuna taarifa kuwa katika baadhi ya sehemu kuna idadi kubwa ya wananchi ambao wamegundulika kutojua kusoma wala kuandika na kufanya zoezi hilo kuwa gumu.
Kutokana na usimamizi usioridhisha wa Nido, wananchi wameonekana kutokuwa na uelewa wa taarifa gani wanazotakiwa kuwa nazo katika ujazaji wa fomu, kwani baadhi ya waandikishaji wamekuwa wakiwataka walete rundo la vitambulisho.
Mchanganyiko huo wa masharti ya utambulisho uko wazi kwani katika sehemu nyingine wametakiwa kuonyesha kitambulisho kimoja tu.
Wananchi pia wamekuwa wakilalamikia kasi ndogo ya uandikishaji ambayo imesababisha misururu mirefu katika vituo vya uandikishaji kiasi cha watu kushindwa kujiandikisha.
Mbaya zaidi hakuna utaratibu wowote wa kuwahudumia watu wenye ulemavu, wajawazito au wenye watoto wadogo na wazee au vikongwe. Nimeshuhudia mateso makubwa kwa watu hao kutokana na idadi ndogo ya waandikishaji katika vituo vya kujiandikisha.
Nido imewaruhusu wajumbe wa mashina ya chama tawala kuwajazia fomu za utambulisho wananchi wanaoishi katika maeneo yao ili waweze kuorodheshwa na serikali za mitaa na hatimaye kupewa vitambulisho vya uraia.
Utaratibu huo tayari umelalamikiwa na raia wa vyama vingine vya siasa kwani wanadai kuwa wajumbe hao wametumia nafasi hiyo kuwahamasisha wanachama wa chama chao kujiandikisha kwa wingi ili washinde katika chaguzi zijazo.
Ni vigumu kuelewa kwa nini serikali kuu na Nido hazikuona umuhimu wa kuhakikisha kwamba vifaa kama karatasi, kalamu, huduma za kupiga picha na kurudufu zinapatikana bila malipo kama ilivyokuwa wakati wa kujiandikisha kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa 2010.
Matokeo yake kuna baadhi ya wananchi wanaofika kujiandikisha wanalalamika kwamba sehemu fulani hapa nchini wanadaiwa rushwa kwa kisingizio cha serikali kutoweka vifaa hivyo na huduma nyingine.
Kutokana na mlolongo wa changamoto hizo nasema kuwa zoezi hilo limekwenda ndivyosivyo na naamini siyo wananchi wote wataweza kulipa fedha hizo, hawa wakulima na watoto wao na wengine wanaweza kuacha kwenda kujiandikisha.
Ipo haja basi Nida kuongeza muda na elimu kwa waandikishaji ili kusudio la serikali kuandikisha raia wote ili wapatiwe vitambulisho vya taifa linafanikiwa, vinginevyo tutakuwa tunapoteza muda na fedha bure.
Namuomba Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mizengo Pinda na timu yake kuyaangalia haya na kuyasafanyia kazi.

Monday, July 30, 2012

MAANDALIZI YA WIZARA KUSHIRIKI KATIKA MAONYESHO YA NANENANE DODOMA YAMEKAMILIKA


Wizara ya Maliasili na Utalii itashiriki katika maeonyesho ya Nanenane ambayo yatafanyika kitaifa katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma tangu tarehe 1 Agosti 2012. Kama kawaida Wizara imeandaa banda moja kubwa ambalo italitumia pamoja na Mashirika, Wakala, Taasisi zake na wadau wa Wanyamapori, Misitu, Nyuki Malikale na Utalii.
Maandalizi ya banda la Wizara ya Maasili na Utalii ambalo lina sehemu kuu tano yamekamilika. Sehemu hizo tano ni:
(i) banda kuu ambapo maelezo yatatolewa na machapisho kugawiwa kwa wageni,
(ii) Bustani ya miti;
(iii) Shamba la Nyuki;
(iv) Wanyamapori hai;
(v) Mashindano ya ufugaji Bora wa nyuki bora.
Katika sehemu ya Wanyamapori hai kutakuwa na aina 20 za wanyama. Leo jioni tarehe 29/7/2012 Wanyama watakaowekwa kwenye mabanda maalum yaliyoandaliwa tayari kwa maonyesho ni Simba, Chui, Tumbili, Kobe, Kanu, Fisi madoa, Fisi Mraba, Sokwe Mtu na Chatu. Wanyama wengine na ndege watawasili leo usiku tayari kuwekwa kwenye mabanda yao kesho.
Aidha katika banda la Maliasili kutakuwa na maonyesho ya asali kitaifa ambayo yameandaliwa na Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) kwa njia ya ushindani. Katika mashindano hayo wafugaji wa nyuki walitembelewa na wataalam katika sehemu wanakofugia na kushindanishwa kwa kuzingatia ufanisi katika ufugaji na utunzaji bora wa mazao ya nyuki hususan asali. Washindi watapewa zawadi na Mgeni Rasmi siku ya kilele cha maonyesho haya ya Nanenane tarehe 8/8/2012.
Kauli mbiu ya Nanenane mwaka huu ni: “Kilimo Kwanza: Zalisha kisayansi na kitekenolojia kukidhi mahitaji ya ongezeko la mahitaji ya watu”.
Kutokana na kauli mbiu hiyo Wizara itawelimisha wananchi kuhusu uhusiano wa shughuli za Maliasili na Utalii na “Kilimo Kwanza”. Kwa mfano wananchi wataombwa kuhifadhi misitu na kupanda miti kwa kuwa misitu inachangia katika kuleta mvua inayofanikisha kilimo. Vilevile vyanzo vya mito inayofanikisha kilimo cha umwagiliaji ni katika misitu.
Aidha wanyamapori hufanikisha utalii ambao huchangia asilimia 26 ya pato la fedha za kigeni nchini. Fedha hizo za kigeni zinatumika katika kununulia zana za kilimo, kama vile matrekta. Pia biashara ya mazao ya Maliasili huleta maduhuli ambayo yanapelekwa Hazina na hatimaye kutumika katika kufanikisha kilimo, kama vile kununua pembejeo.
Wananchi wanaoishi katika mkoa wa Dodoma na mikoa ya jirani wanakaribishwa kutembelea banda la Maliasili katika maonyesho ya Nanenane Dodoma ili wapate utaalam wa kushiriki katika shughuli za kuhifadhi na kuendeleza Maliasili kwa manufa yao.
[MWISHO]George Matiko
MSEMAJI
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
Tarehe 29 Julai 2012

BARAZA LA VIJANA CHADEMA(BAVICHA) LAWATAKA VIJANA KUSHIRIKI KUTOA MAONI YA KATIBA MPYA


Wakazi wa Iringa wakiwasikilizaviongozi wa BAVICHA 
katika uwanja wa Mwembetogwa



AIRTEL SASA KUTUMA PESA BURE KUPITIA AIRTEL MONEY


Wateja wa Airtel sasa kutuma pesa Bure kupitia Airtel money

·Kupata huduma ya Airtel money sasa piga *150*60# Bure

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeendelea kuboresha huduma ya Airtel money kwa kurahisisha upatikanaji wa muongozo (menu) kwa kupiga *150*60# Bure pamoja na kuzindua promosheni kabambe itakayowawezesha wateja wa Airtel nchi nzima kutuma pesa Bure.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema” Airtel tunaendelea kutoa uhuru kwa wateja kupata huduma zetu kirahisi zaidi nchini kote, kuanzia sasa mteja akipiga *150*60# anapelekwa moja kwa moja kwenye orodha yake ya huduma na kuweza kuchagua anachohitaji kufanya ikiwa ni pamoja na kuongeza salio, kufanya malipo, kutoa pesa na mengine mengi
tumefanya hivi hii ili kumwezesha mteja mwenye simu yeyote kupata huduma za kibenki na kuondoa changamoto zozote zitakazojitokeza, sasa mteja ana uhuru wa kuchagua kutumia njia ya awali ambayo ni kwenda moja kwa moja kwenye muongozo wa simu yake na kupata orodha (Menu) ya Airtel au kupiga namba *150*60# na kuunganishwa moja kwa moja
vilevile tunayofuraha kuzindua ofa kabambe kwa wateja wetu nchini zima ambapo kutuma au kupokea pesa chini ya kiwango cha 100,000 ni BURE na mteja atakaponunua LUKU kupitia Airtel money ni BURE (hakuna viwango vya miamala vitakavyotozwa). Tunawajulisha wateja wetu wote na wakala wetu waliosambaa nchi zima kutumia huduma hii iliyorahisi ni rahisi aliongeza” Mmbando.
Airtel ni mtandao ulioenea nchini na unatoa huduma za kifedha za Airtel money yenye mawakala zaidi ya 10,000 waliosambaa maeneo mbalimbali mjini na vijijini kwa dhamira ya kupunguza changamoto ya upatikanaji wa huduma za kifedha na kusaidia wateja wetu kuokoa muda kwenda mbali kupata huduma za kibenki.
Kupitia Airtel money mteja anaweza kupata huduma mbalimbali ikiwemo: kupokea pesa, kulipa bill kama DSTV, LUKU na DAWASCO, USA visa , kununua salio na huduma nyingine nyingi

Thursday, July 26, 2012

Kundi la watu wanaodhaniwa majambazi wamevamia baa ya Chonya

Kundi la watu wanaodhaniwa majambazi wamevamia baa ya Chonya eneo la
River Side jijini DSM, leo asubuhi na kupora fedha.

Birthday ya Spika wa Bunge Anne Makinda

 Spika wa Bunge Anne Makinda akikata keki tayari katika 
Birthday yake jana mjini Dodoma.
Bi Lina Kitosi akimlisha Mhe. Spika keki kwa niaba ya wafanyakazi wa Bunge wakati wa 
Birthday yake ya 63 iliyofanyika jana mjini Dodoma.
Ni Birthday ya 63 ya Mhe. Spika Anne Makinda na hii 
ilikuwa keki ya Birthday.
 Spika Anne Makinda akipokea keki kutoka kwa mmoja 
wa wafanyakazi wa Bunge.

Walichosema wabunge katika Tamasha la Kigoma



 Walichosema wabunge katika Tamasha la Kigoma All Stars-Leka Dutigite, Lake Tanganyika Stadium, Kigoma

Video ya kwanza : Mhe. Joshua Nassari -Mbunge wa Arumeru Mashariki
Video: Zitto

Wednesday, July 25, 2012

HOSPTALI YA AICC KUENDESHA KAMPENI YA KUPIMA KISUKARI BURE


 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Hosptali ya AICC kuendesha kampeni ya kupima kisukari bure
24-07/2012
Arusha, Tanzania

Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha kupitia hospitali yake ya AICC kitaendesha kampeni ya kupima kisukari bure kwa wakazi wa Arusha ili kusaidia wananchi kutambua kama wana ugonjwa wa kisukari au wapo katika hatari ya kuugua ugonjwa huo.
Kampeni hiyo itafanyika kesho (terehe 26-07-2012) katika hopitali ya AICC iliyopo jijini Arusha ambapo madaktari wa hospitali ya AICC kwa kushirikiana na madaktari wa wanaohudhuria mkutano wa Shirikisho la Madaktari wa Kimataifa pamoja na madaktari kutoka Chama cha Ugonjwa wa Kisukari Tanzania wataendesha zoezi la upimaji huo.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa AICC, Bwana Elishilia Kaaya, amesema kuwa mbali na kupima kisukari, madaktari hao pia watatoa ushauri wa namna bora ya kuishi na jinsi ya kuzuia madhara ya kisukari kwa wale watakao kuwa wamekutwa na ugonjwa huo.
 “Hospitali ya AICC inatambua umuhimu wa afya za wakazi wa Arusha na Watanzania kwa ujumla na ndio maana tumeona ni vema kufanya kampeni hii ya kupima kisukari. Napenda kutumia fursa hii kuwaalika wakazi wote wa Arusha na vitongoji nyake kufika kwa wingi kwani mbali na kupima pia itatolewa elimu na ushauri kutoka kwa wataalamu hao.” alieleza Kaaya.
Kwa mujibu Mkurugenzi Mwendeshaji, upimaji huo utaenda sambamba na mkutano wa kwanza wa Shirikisho la Madaktari wa Kisukari wa Kimataifa ambao kwa mara ya kwanza unafanyika hapa nchini. Mkutano huo utafanyika katika kituo cha AICC ambapo madaktari wanaohudhuria mkutano huo na wale kutoka Chama cha Ugonjwa wa Kisukari Tanzania watatoa huduma ya upimaji katika zoezi hilo.
“Tunaamini baada ya kampeni hii wananchi watakuwa wamepata ufahamu juu ya hali ya afya zao na kutumia vema ushauri wa madaktari kwa ajili ya kujikinga na kuzua athari za ugonjwa huo”, alielezea Kaaya.
Mbali na kuendesha kampeni hii, hospitali ya AICC imeanzisha kitengo maalumu cha kisukari ambapo kila wiki madaktari hutoa huduma za matibabu na ushauri kwa wagonjwa wa kisukri.
Ugonjwa wa kisukari umekuwa ukiongezeka kwa kasi duniani ambapo taarifa za Shirika la Afrya Duniani (WHO) zinaonesha kuwa hadi kufikia mwaka 2011 watu milioni 366 walikuwa wanaugua ugonjwa wa kisukari na mwaka 2030 idadi inakadiriwa kufika milioni 552. Barani Afrika watu milioni 14 na nusu wanaugua ugonjwa huo huku idadi ikitarajiwa kufika milioni 28 mwaka 2030 ikiwa ni ongezeko la asilimia 90.

Vodacom Tanzania Yapunguza Gharama za Simu Mwezi Mtukufu wa Ramadhan

  • Ni Ofa mpya ya kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi wa maneno na kutumia intanet kwa shilingi 250 tu kwa siku.
  • Ofa kuanza kila siku saa tano usiku hadi saa moja asubuhi.
  • Kupata ofa hiyo piga *102*250#
-
Dar es Salaam 25th Julai 2012…. 
 Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania, imeanzisha ofya mpya ya mwezi mtukufu wa Ramadhan ambayo itawawezesha wateja wa mtandao huo kupiga simu bila kikomo, kutuma ujumbe mfupi wa maneno na kupata huduma za intanet kwa shilingi 250/= tu kwa siku.
Ofa hiyo mpya itakuwa ni kwa siku saba za wiki kuanzia saa tano usiku hadi saa moja asubuhi katika kipindi chote cha mwezi mtukufu wa Ramadhan. Ili mteja ajiunge na huduma hiyo, atatakiwa kupiga *102*250# ambapo ataweza kupiga simu kutoka Vodacom kwenda Vodacom, kutuma ujumbe mfupi wa maneno kwenda mitandao yote ya simu na kutumia intanet bila kikomo.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bwana Rene Meza alisema kipindi hiki ni maalum kwa waislamu duniani kote kuwa karibu na Mungu pamoja na ndugu, jamaa na marafiki.
“Tumeona vyema tuwapatie njia rahisi ya kuwasiliana na ndugu, jamaa na marafiki kwa unafuu na ambayo wataifurahia tukijua kwamba waislamu walio wengi ni miongoni mwa wateja ambao wametuunga mkono kwa miaka mingi sasa. Tunataka nao wajisikie kuwa sehemu ya familia ya Vodacom katika kipindi hiki cha maombi,” alisema Meza.
Ofa hii imekuja wakati Vodacom Foundation inaendelea na kampeni yake ya Care and Share mkoani Tanga inayolenga kutoa misaada ya kifedha na vifaa mbalimbali kwa watoto yatima katika kipindi cha Mwezi wa Ramadhan.
Kampeni ya Care and Share inaadhimisha miaka mitano tangu kuzinduliwa kwake, huku ikitoa fursa ya kipekee kwa Vodacom Foundation kushughulikia changamoto mbalimbali kwa watoto yatima na vituo vya kulelea watoto yatima.
Kupitia kampeni hiyo, mamia ya watoto yatima wameweza kusaidiwa na maisha yao kuboreshwa, suala ambalo jamii nzima na wateja wa Vodacom wanajivunia.
“Tutaendelea kuwapatia wateja wetu kile wanachostahili kwani bila ya mchango wao Vodacom Tanzania isingekuwa hapa ilipo leo. Nawatakia waislamu wote kheri katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan,” alihitimisha Meza.

Friday, July 20, 2012

PICHA MBALIMBALI ZA AJALI YA MELI





Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,
(wa pili kulia) akiwa na Viongozi Wakuu wa Serikali alipofika katika Ofisi za Shirika 
la Bandari, Malindi Unguja kupata taarifa sahihi ya ajali ya kuzama kwa Meli ya 
MV Sky Get ikitokea Dar es Salaam kuelekea Unguja.








Majeruhi wakipatiwa Mablanketi kwa ajili ya kujihifadhi baada ya kuokolewa 
katika meli ya Star Gate iliozama huko katika bahari ya Chumbe Zanzibar na
 ikiwa na abiria 250.





Majeruhi alieokolewa katika meli ya Star Gate iliozama huko katika 
bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250. 





Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Amer Kificho pamoja na mawaziri 
mbalimbali wakiwa katika Eneo la Bandari wakishuhudia kuletwa kwa 
majeruhi mbalimbali waliookolewa katika meli ya Star Gate iliozama huko 
katika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250





Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akiwa katika Eneo 
la Bandari akishuhudia kuletwa kwa majeruhi mbalimbali waliookolewa katika 
meli ya Star Gate iliozama huko katika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250. 





Wananchi mbalimbali wakishuhudia tukio la kuokolewa watu waliozama 
na meli ya Star Gate huko katika hukokatika bahari ya Chumbe Zanzibar 
na ikiwa na abiria 250. 





Waziri wa Nchi Afisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk 
Mwinyihaji Makame akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari kuhusiana na 
kuzama kwa Meli ya Star Gate hukokatika bahari ya Chumbe Zanzibar na 
ikiwa na abiria 250. 





Askari wa Vikosi mbalimbali wakiwa katika kazi ya Uokozi kwa Abiria 
waliokuwa katika Meli ya Star Gate ambayo iliozama katika ikiwa imebeba 
abiria 250 huko katika bahari ya Chumbe Zanzibar





Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Hamad Masoud Hamad akiwa katika 
hali ya huzuni Baada ya kushiriki katika uokoaji na kuwaona Majeruhi
waliookolewa katika Meli iliozama ya Star Gate wakiteremka hapo Bandarini Zanzibar. 





Abiria aliyookoka katika Meli iliozama ya Star Gate akifarijiwa na Jamaa 
zake Baada ya kuteremka katika Meli iliowaokoa hapo Bandarini





Abiria aliyeokoka kutoka katika meli iliyozama





Abiria waliookolewa kutoka katika meli iliozama ya Star Gate katika 
bahari ya Chumbe Zanzibar 





Watalii na raia wa kigeni pia walikuwemo katika meli iliyozama hawa 
ni baadhi ya waliosalimika











Majeruhi wakiwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja





Majeruhi wa ajali ya Meli wakiwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja 
wakipata huduma baada ya kuokolewa.














Daktari akitowa huduma ya kwanza kwa mmoja wa majeruhi wa boti iliozama





Mmoja wa Majeruhi akipata huduma ya Kwanza baada ya kuokolewa 
akiwa katika bandari ya malindi














Tagi la Shirika la Bandari likiwa katika sehemu ya tukio.





Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu Hamad Masoud akiwa katika 
boti ya Kilimanjaro akiwa sehemu ya Tukio ilipozama boti hiyo maeneo ya Chumbe.








Boti ya Fly ikiondoka katika bandari ya Zanzibar kueleke kutowa 
msada w uokoaji.





Boti iliozama ni kama hii ni ni pacha wake.





Helikopta ya Jeshi la Polisi ikiwa eneo la tukio.





Boti ya KMKM ikiwa katika zoezi la kuokowa majeruhi. 





Baadhi ya Abiria wakiwa katika moja ya chombo cha kuokolea wakielea 
baharini wakisubiri kuokolewa.





Majeruhi wakiwa katika mgongo wa boti hiyo wakisubiri kuokolewa.





Waokoaji wakiokoa moja ya maiti. wakiwa katika boti ya Kilimanjaro. 





Mwokoaji akiwa na mmoja wa maiti wa ajali hiyo.


Picture


Picha kama ilivyochukuliwa na Dkt. Mahamba akiwa kwenye ndege angani 
mara baada ya rubani kuishusha ndege usawa wa futi 2,800. 


Picture




Picture









Hizi ndizo Meli za Mv Skagit ambazo ununuzi wake uliripotiwa kwenye
 vyombo vya habari mwanzoni mwa mwaka 2011 amabo ilidaiwa kuwa
meli hizi zilinunuliwa kutoka Marekani - Washington State na moja ya
kampuni za usafiri kwa Dola laki nne kwa zote mbili ambapo zilitegemewa
kutatoa huduma za usafiri kati ya Zanzibar na Dar.

Boti hizi zilitengenezwa mwaka 1989 na kila moja ina uwezo wa kubeba
abiria 250 ziliwahi kuwekwa kwenye mtandao wa E bay kwa bei ya
Dola laki tatu kila moja lakini hazikupata wateja. Zilipotengenezwa
mwaka 1989 ziligharimu Dola milioni tano.

Picha na maelezo kwa hisani ya Zanzibar Blog.

New