Hotuba ya bwana harusi wetu
MC: Na sasa tupate maneno machache kutoka kwa bwana Harusi
BWANAHARUSI: Asante MC, kwanza naomba nimshukuru Mungu kwa kumuumba mke wangu, kwa hilo Mungu uko juu. Pili nimshukuru baba mwenye nyumba wangu kwa kukubali niwe na deni la kodi ili kufanikisha harusi hii. Naomba nitoe shukrani kwa bosi wangu kwa kunipa likizo fupi ili nikamilishe shughuli hii. Naishukuru kamati yangu ya harusi kwa kuwezesha kukusanya fedha zilizofanikisha harusi hii, nimshukuru mke wa kaka yangu kwa kutuazima gauni la harusi, na kaka yangu kwa suti hii niliyovaa. Natoa shukrani kwa mtengeneza keki, nitairudisha keki kwako kesho kama tulivyokubaliana. Nawashukuru wazazi wangu kwa kuja na kikundi cha ngoma toka kijijini, kweli kimeziba pengo la burudani katika harusi hii. Naishukuru kamati ya wazee wa kanisa kwa kufanikisha kumshawishi mke wangu aolewe na mimi, niwape aksante kwa akina mama jirani kwa kuja na vyakula toka makwao ili kufanikisha harusi hii, na vijana kwa kuja na pombe za halali na haramu mradi harusi hii ni furaha tupu. MC wewe ni rafiki yangu nashukuru kwa kukubali tulipane kidogokidogo aksante sanaaaaa
BWANAHARUSI: Asante MC, kwanza naomba nimshukuru Mungu kwa kumuumba mke wangu, kwa hilo Mungu uko juu. Pili nimshukuru baba mwenye nyumba wangu kwa kukubali niwe na deni la kodi ili kufanikisha harusi hii. Naomba nitoe shukrani kwa bosi wangu kwa kunipa likizo fupi ili nikamilishe shughuli hii. Naishukuru kamati yangu ya harusi kwa kuwezesha kukusanya fedha zilizofanikisha harusi hii, nimshukuru mke wa kaka yangu kwa kutuazima gauni la harusi, na kaka yangu kwa suti hii niliyovaa. Natoa shukrani kwa mtengeneza keki, nitairudisha keki kwako kesho kama tulivyokubaliana. Nawashukuru wazazi wangu kwa kuja na kikundi cha ngoma toka kijijini, kweli kimeziba pengo la burudani katika harusi hii. Naishukuru kamati ya wazee wa kanisa kwa kufanikisha kumshawishi mke wangu aolewe na mimi, niwape aksante kwa akina mama jirani kwa kuja na vyakula toka makwao ili kufanikisha harusi hii, na vijana kwa kuja na pombe za halali na haramu mradi harusi hii ni furaha tupu. MC wewe ni rafiki yangu nashukuru kwa kukubali tulipane kidogokidogo aksante sanaaaaa
Mpaka chupi imekonda
Binti alifariki kwa ukimwi. Nyanya yake akawa anakusanya nguo zake ndipo alipokumbana na G String ya marehemu
BIBI: Sasa nimeamini ugonjwa huu mbaya, umekondesha mpaka chupiMi sina bahati kama mke wangu
Walevi watatu walikutana baa;
Mlevi 1: Hii baa nzuri lakini sio kama ya mtaani kwetu. Pale
kwetu kuna baa ya Kimaro ukinunua chupa mbili , Kimaro mwenyewe
anakunulia moja nyingine
MLEVI 2: Mtaani kwetu kuna baa ya Gano, hapo ukinunua moja na Gano anakunulia ya pili
MLEVI 3: Mtaani kwetu ndio
kiboko, kuna baa ya Mzee Komba ukifika akikuchagua, anakununulia bia
mpaka ulewe kisha anakupeleka kwenye gesti yake anakupa mtu wa kulala
nae
MLEVI 1: Hapo kiboko, we umeshawahi kuchaguliwa?
MLEVI 3: Bado mi sina bahati sana, lakini mke wangu kisha chaguliwa mara 2 wiki hii peke yake.Aise ufunguo sio wenyewe
Jamaa alikuwa na safari
ya miezi kadhaa, kwa wivu wake akamtengenezea mke wake chupi ya chuma. Siku
alipokuwa anaondoka akamuita rafiki yake mpenzi;
JAMAA: Aise wewe ndiye
rafiki yangu mpenzi mi nasafiri, nimemtengenezea mke wangu chupi ya chuma yenye
kufuli, ili wahuni wasije wakamshawishi kunisaliti, sasa naona ufunguo naweza
kuupoteza hivyo naomba wewe ukae nao mpaka nirudi.
RAFIKI: Nashukuru kwa
imani kubwa uliyonayo juu yangu rafiki, nitakutunzia vema mali zako..........
Mume akaelekea kwenye kituo cha basi, kabla hajafika rafiki yake akamuwahi huku
akipumua kwa shida na kutokwa jasho baada ya mbio ndefu.
RAFIKI: Aise samahani,
inaonekana umekosea umeniachia funguo sio
Nyani na mjusi walikuwa kijiweni wanavuta bangi......
Siku
moja Nyani alikuwa kakaa kijiweni anavuta bangi. Mjusi akaja akampa
'Hi', akaomjoin na kuomba puff, nyani akamuonya kuwa ile bangi kali ni
kipisi cha kutoka Makete. Mjusi akapokea wakaanza kuvuta kwa raha zao.
Mjusi akawa hoi kwa stimu akamwambia nyani,'Nasikia koo limekauka ngoja
niende mtoni nikanywe maji'. Mjusi kufika mtoni kwa kuwa alikuwa na
stimu nyingi akatumbukia mtoni. Mamba aliyekuwa pembeni akamwona akawahi
kumuokoa na kumtoa nje ya maji. Mamba akamuuliza mjusi imekuwaje
kutumbukia mtoni kizembe vile, mjusi akajibu, 'Nilikuwa na nyani
tunavuta bangi nikasikia kiu cha ajabu nikajikuta kwenye maji' mamba
akasema, 'Hebu twende kwa huyo nyani'. Wakamkuta nyani ndo anamalizia
kile kipisi hata macho tabu kufungua. Mamba akamuita, 'Oya'. nyani
akafungua macho alipomuona mamba akashtuka sana,'Mshikaji umekunywa maji
debe ngapi umerudi mkubwa hivyo?
Vituko vya kweli vya wavuta bangi
Katika maisha yangu nimekwisha sikia vituko vingi kuhusu bangi.
Nikikumbuka siku ya kwanza nimemuona rafiki yangu akivuta bangi(1968),
jina lake ni Iddi sitataja majina mengine ameshakuwa mtu mzima sasa
ninauhakika anawajukuu wengi tu. Alikuja mahala ambapo tulikuwa
tunafanya mazoezi ya muziki maana naye alikuwa mpiga gitaa mzuri, akatoa
bangi kwenye kibox cha njiti za kibiriti akasokota akavuta, wote
tukimkodolea macho na kusubiri apagawe, hakuna cha ajabu alichofanya ila
tu nakumbuka alikuwa anarudia rudia na kudai sisi sote ni samaki. Mpaka
leo nikikutana nae huwa namtania, 'samaki'. Rafiki yangu mwingine
ambaye ana wadhifa mkubwa serikalini aliwahi kunambia kuwa kuna siku
alivuta bangi akahisi shati lake lina siafu, ilibidi alitoe na kulitupa
pembeni huku akipiga kelele 'siafu siafu'. Kuna Mzee mwingine Richard,
ambaye kwa sasa mawasiliano yetu yamekuwa ni kupitia FB maana miaka
mingi hatujaonana, aliwahi kuwa kituko shuleni baada ya kuvuta bangi
wakati wa mapumziko ya saa 4, enzi hizo akiwa form 2, yeye alihisi
mbingu zinateremka na kuja kumbana, kwa hiyo nae akazidi kutembea huku
akiwa ameinama macho yake juu, akiangalia mbingu ambazo kwake zilikuwa
zinateremka na kukaribia kumbana, watu wote tukimuangalia na kumshangaa.
Sitasahau nilivyocheka kituko cha rafiki yangu marehemu aliyekuwa
mwanamuziki muimbaji, ambaye alinambia yeye na rafiki zake mara nyingi
walikuwa wanazungumza kuwa kuna wauza bangi huchanganya bangi na kinyesi
cha binadamu ili iwe kali zaidi. Sasa siku moja wenzie walipompa kipisi
cha bangi, kilianza kumletea hisa za kufa kufa hivyo akahisi
'wamemchanganyia'. Kadri muda ukivyozidi ndivyo alivyozidi kujisikia
vibaya, ikalazimu akimbilie kwa baba yake huku akilia,'Baba baba
wamenichanganyia'
kuna kali ya ukweli ya muuza vinyago(kaajiriwa)..yeye alikuwa anauza
vinyago vya kawaida vya mpingo..sasa siku moja akavuta bangi kwa mara ya
kwanza tena asubuhi kabla ya kwenda kazini...ila sasa bosi wake jana
yake usiku alileta vinyago kutoka Congo(vya kizamani)ambavyo mara nyingi
hutoa harufu mbaya sana(sijui kwanini)..sasa jamaa asubuhi akiwa
"high"(kwamara ya kwanza) kafungua duka, kasikia harufu mbaya sana, basi
akampigia bosi wake;
Jamaa;bosi huku hali ni mbaya sana
Bosi; kwani kuna tatizo gani?
Jamaa:hawa wanyama wote wamekunya humu dukani yani kunanuka kimba balaa njoo mwenyewe uzoe mavi mimi kazi yako basi...
Jamaa;bosi huku hali ni mbaya sana
Bosi; kwani kuna tatizo gani?
Jamaa:hawa wanyama wote wamekunya humu dukani yani kunanuka kimba balaa njoo mwenyewe uzoe mavi mimi kazi yako basi...
Wamama natoa onyo, punguzeni ufisadi
Ufisadi unatajwa sana
katika mali kama ardhi, na pesa. Utasikia watu wanalalamika ohh Mwenyekiti
anahodhi eneo kubwa sana la ardhi peke yake wakati wengine hawana eneo, au ohh
jamaa anahodhi akaunti kubwa ya vijisenti wakati wananchi wengine wakiwa hawana
hata hela ya kula. Kuna ufisadi ambao uko wazi ila watu wanaukwepa kuupiga
vita.
Sensa ya mara ya mwisho
hapa nchini, ilionyesha wazi kuna
uhaba mkubwa wa wanaume hapa nchini, sasa unakuta wamama wanahodhi mwanaume na
kukataa katakata kushirikiana katika matumizi kwa ushirikiano na wamama wenzie, huu ni ufisadi wa hali ya
juu. Acheni uchoyo, tumieni bidhaa hii adimu kwa ushirikiano, amani na upendo. Nawasilisha hoja
No comments:
Post a Comment