Kufuatia ushauri wa waziri mkuu
Mizengo Kayanza Pinda wa kuziomba bank zipunguze kiwango cha riba kwa
wakulima, kuna swali limeulizwa kua vipi bank za kiIslam zinaweza
kuwasaidia wakulima? Swali hilo limejibiwa kama ifuatavyo. Ni kweli
kwamba katika gazeti la Mwananchi la tarehe 16/5/2012 kulikuwa na makala
iliyonakili ushauri wa Waziri Mkuu wa Tanzania Mh Mizengo Kayanza Pinda
akizishauri bank zitoe mikopo yenye riba nafuu kwa wakulima. Alizitaja
changamoto ambazo zinawakabili wakulima kwa kusema ‘"Wakulima
wadogowadogo wanashindwa kupata mikopo ya kutosha kwa sababu benki za
biashara zinawatoza riba kubwa na kuhitaji dhamana (collateral) alisema
Mh Pinda. Mh Pinda aliyasema hayo jijini Dar es Salaam katika hotuba
iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,
Shamsi Vuai Nahodha wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Chama cha Kilimo
Vijijini Afrika (Afraca).
Tukianzia na tataizo la riba (interest) na ambalo bank za kawaida
zinatofautiana na bank za kiIslam, ni dhahiri kua riba ktk mazingira
yake yote ni kikwazo kikubwa cha maendeleo. Matatizo ya riba
yalishaelezwa na bado yanaendelea kuelezewa, na kuthibitishwa na
wataalam wengi wa kiuchumi duniani, kwa mfano hivi karibuni mkuu wa
shirika la fedha la kimataifa International Monetary Fund (IMF)
Christine Lagarde aliishauri serikali ya Uingereza kupunguza kiwango
cha riba mpaka ifikie sifuri, alinukuliwa akisema “BRITAIN should
consider cutting the interest rate to ZERO if the economy continues to
struggle, the International Monetary Fund believes”).The Sun 23 may 2012.
Maneno ya Miss Lagarde yaliungwa mkono na wanauchumi wengi kwa kesema
“Cutting rates from 0.5 per cent won’t be the solution on its own, but
would send out the right signal.”
Kwa upande wa bank za kiIslam, tungezishauri zijitokeze
kuwafahamisha wananchi na wadau mbali mbali kua ziko njia mbali mbali
zinazoweza kutumiwa kuepuka riba, na wakati huo huo kuleta ufanisi
katika nyanja mbali mbali za kiuchumi, jamii na kadhalika. Ukweli ni
kwamba bank za kiIslam zina uwezo wa kuwasaidia wakulima kwa kutumia
mifumo ya uchumi ambayo inakubalika kisheria kama vile murabaha,
mudarabah, muzaarah, musaqaat na nyinginezo ambazo zimeelezewa kwa
ufasaha kwenye www.ijuebankiyakiislam@blogspot.com.
Tukitolea mfano kwa kutumia mfumo wa murabaha, bank inaweza
kuwapatia wakulima vifaa na mahitaji mbali mbali kwa masharti ya
kulipa hapo baadae pamoja na faida. Murabaha maana yake ni bank au
mwenye uwezo, kumnunulia asie na uwezo kitu fulani kwa masharti amlipe
kwa faida maalum hapo baadae, kwa mfano bank inaweza kuwanunulia
wakulima vifaa mbali mbali vya kilimo kama vile matrector, mbegu na
mbolea, kisha ikawauzia kwa faida maalum kwa masharti walipe hapo
baadae. hapa inaonekana wazi kabisa kua murabaha unaweza kuwasaidia
wakulima wakaweza kujikomboa na kujitegemea hapo baadae.
Wasi wasi mwengine ni ule unaohusiana na dhamana (collateral)
kutoka kwa wakulima kutokana na uhakika kwamba wakulima wengi hawana
mali ambazo wanaweza kuzitumia kama dhamana ili bank ziweze kuwapa
mikopo. Hilo nalo linaufumbuzi wake, kwa mfano bank za kiislsm inaweza
ikatumia kitu kinachojuikana kama‘group-based lending approach
capitalising on peer monitoring and guarantee mechanism’ ambayo ni
utaratibu wa kufanya biashara kwa vikundi ambayo hiyo inaweza kuwa
mbadala wa dhamana kwa mtu mmoja mmoja.
Ushauri kwa serikali ya Tanzania
Kwa upande wa serikali, tunapenda kuishauri ibadilishe njia
(approach) katika kilimo na wakulima kwa kuweka mipango madhubuti ya
mabaliko katika maeneo mengi ya vijijini kwa kujenga miundominu. Ni
ukweli usiopingika kua wakazi wengi wa vijijini wanapoteza haki zao za
msingi kama vile elimu bora, matibabu ya uhakika, na kadhalika.
Ukiangalia umuhimu na mchango wa mkulima katika mataifa yanayoendelea
utakuta kwamba wakazi hawa wanatakiwa wapatiwe mahitaji muhimu kama vile
barabara safi, vituo vya elimu, afya na miondombinu mengine. Kwa kua
wakazi wengi wa vijijini ni wakulima, serikali pia inatakiwa iweke
mipango madhubuti ya kuinua kilimo kwa kuwapatia wakazi hawa
wataalam,ujuzi na mahitaji mengine.
Pamoja na mambo mengine hotuba yake Mh waziri mkuu iliziasa bank
kuwafikia wananchi huko vijijini, hili ni suala muhimu kwani mabank
mengi yamejikita sana mijini na kuwasahau kwa kiasi kikubwa wakazi wa
vijijini. Wataalamu wengi wa kiuchumi wanadai kwamba suala la faida kwa
mabank ndio sababu ya mabank haya kutokupeleka huduma vijijini, suala
hili limesababisha wakazi wengi wa vijijini kukosa huduma za kibank
mpaka waende mijini kitu ambacho kinawagharimu sana. Kwa upande mwengine
uchunguzi wa mambo unaonyesha kua wakazi wengi wa vijijini hawana bank
accounts, kitu ambacho kimesababisha ugumu sana kwa wakazi hao kuaminika
kupata hata hiyo mikopo yenye riba nafuu. Kwa haya machache tunadhani
yatasaidia lakin kama kutakua na swali lolote basi usisite kuwasiliana
nasi.
Kuna ndugu yetu ameuliza swali lifuatalo
Asilimia 95 ya wafanyabiashara wa
kiIslam hapa TZ wanakopa pesa za riba kutokana na kutokuwepo na taasisi
za fedha za kiIslam kuwakopesha, nini hukmu yao ktk nchi hizi ambazo
bank za kiIslam hazipo.
Limejibiwa kama ifuatavvyo
Riba ktk mazingira yote imekatazwa ktk sheria ya kiIslam kwa aina zake zote ikiwemo kukopa ambako kuna riba(Quran 03:130; Deuteronomy 23:19 ; Bible, Matthew 05:17). Sio hivyo tu, Mwenye ezzi Mungu ametangaza vita kwa wale wote watakaofanya matendo ambayo riba itahusika kwa njia moja au nyingine. Rudia blog www.ijuebankyakiisam.blogspot.com kwa maelezo zaidi kuhusu madhara ya riba ktk sehemu ya maswali na majibu kuna article kwa anuani ‘contemporary world without interest’.
Kuhusu kutokuwepo kwa taasisi za fedha za kukopesha bila riba Tanzania, uhakika ni kwamba bank za kiIslam zimeanza kuenea kwa kasi Tanzania ikiwemo Amana bank ambayo ni full Islamic bank na nyingine kama vile NBC ambazo zina Islamic window. Inawezekana kwamba huduma kama za mikopo ya pesa bado hazipo, kama hiyo ndio kesi, basi riba ktk mikopo itabaki kua ni haramu lakin kuna huduma nyingine ktk hizo bank za kiIslam ambazo ni halali na mteja anaweza akatumia huduma hizo badala ya mkopo wa riba. Kwa mfano anaweza kufanya kitu kinachojulikana kama murabaha, mudarabah, musharaka na nyinginezo ambazo zimeelezewa kwa ufasaha kwenye blog iliyotajwa hapo juu.
Kitu kingine cha kuzingatia ni kwamba mtu kufanya biashara kama hiyo ambayo atahitaji kuchukua mkopo wa riba, sio kitu cha lazima ambacho asipofanya hivyo atapoteza maisha, kwahiyo, sio ktk dharura zilizoruhusiwa kisheria ya kiIslam ambazo mtu anaweza kufanya jambo la haramu. Ambalo linashauriwa kwa bank za kiIslam ni kujitahidi kuhakikisha kua huduma hizo zinapatikana hata kama ni ktk wakati wa baadae, kwa kua mahitaji ya huduma hizo yanazidi kuongezeka. Mpaka bank za kiIslam zitakapoanza kutoa huduma hizo mikopo hiyo ya riba itabaki kua ni haram ktk sheria ya kiIslam. Nadhani kwa haya machache yanajibu swali lako na kama utahitaji maelezo zaid basi usisite kutuandikia.

Shukran.
No comments:
Post a Comment