Waziri Mkuu Mstaafu Bw. Frederick
Sumaye akimsisitiza jambo Bw.Martin Sanya mara baada ya kumkabidhi tunzo
pamoja na kitita cha shilingi Mil 3.8 ya mwamuzi bora wa ligi kuu ya
Vodacom 2011/2012, Anaeshuhudia kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na
Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Bw. Kelvin Twisa.
Waziri Mkuu Mstaafu Bw.Frederick
Sumaye katikati akishuhudia Mh.Mbunge wa Tabora mjini ambae ni
Mwenyekiti wa Simba Sports Club Elden Rage akipongezwa na Mkuu wa
kitengo cha Masoko na Mawasiliano Bw.Kelvin Twisa mara baada ya kupokea
tunzo ya golikipa bora kwa niaba ya Juma Kaseja,wakati wa hafla ya kutoa
tunzo kwa msimu ulioisha wa ligi kuu ya Vodacom.
Waziri Mkuu Mstaafu Bw.Frederick Sumaye akiongea wakati wa hafla ya kutoa tunzo kwa msimu ulioisha wa ligi kuu ya Vodacom.
Meneja Mahusiano ya nje wa Vodacom
Tanzania Bw.Salum Mwalim (kushoto) na Meneja Mahusiano wa kampuni hiyo
Matina Nkurlu wakifuatilia hotuba ya Waziri Mkuu Mstaafu Bw. Frederick
Sumaye ambae alikuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya kutoa tunzo kwa msimu
ulioisha wa ligi kuu ya Vodacom.
Waziri Mkuu Mstaafu Bw.Frederick
Sumaye akimpongeza Msemaji msaidizi wa Azam FC Jaffer Iddi Maganga
alipoenda kupokea tunzo ya vijana kwa niaba ya Rashid Mandawa wa Coastal
Union wakati wa hafla ya kutoa tunzo kwa msimu ulioisha wa ligi kuu ya
Vodacom,iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania katika Hoteli ya Dobble Tree,
anaeshuhudia kulia ni Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa
Vodacom Bw.Kelvin Twisa.
Waziri Mkuu Mstaafu Bw.Frederick
Sumaye katikati akishuhudia Mwenyekiti wa Azam FC Mohamed Said
akipongezwa na Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano Bw.Kelvin Twisa
mara baada ya kupokea tunzo ya mfungaji bora na timu ya nidhamu na
kocha bora kwa niaba ya klabu yake wakati wa hafla ya kutoa tunzo kwa
msimu ulioisha wa ligi kuu ya Vodacom, iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania
katika hoteli ya Dobble Tree jijini Dar e Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu Bw.Frederick
Sumaye akimkabidhi hundi yenye thamani ya shilingi Milioni kumi na tano
na laki tano Katibu wa Yanga Bw.Selestini Msigwa wakati wa hafla ya
kutoa tunzo kwa msimu ulioisha wa ligi kuu ya Vodacom, iliyoandaliwa na
Vodacom Tanzania katika hoteli ya Dobble Tree jijini Dar e
Salaam,anaeshudia katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano
wa Vodacom Tanzania Bw.Kelvin Twisa.
Waziri Mkuu Mstaafu Bw.Frederick
Sumaye kushoto akishuhudia Mwenyekiti wa Azam FC Mohamed Said
akipongezwa na Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano Bw.Kelvin Twisa
mara baada ya kupokea hundi yenye thamani ya shilingi Milioni ishirini
na mbili kwa kuibuka washindi wa pili katika msimu 2011/2012 wa ligi kuu
ya Vodacom wakati wa hafla ya kutoa tunzo kwa msimu ulioisha wa ligi
kuu ya Vodacom,iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania katika hoteli ya Dobble
Tree jijini Dar e Salaam.
Waziri
Mkuu Mstaafu Bw.Frederick Sumaye kushoto akimkabidhi hundi yenye
thamani ya shilingi milioni hamsini Mh.Mbunge wa Tabora mjini ambae ni
Mwenyekiti wa Simba Sports Club wakati wa hafla ya kutoa tunzo kwa msimu
ulioisha wa ligi kuu ya Vodacom,katikati ni Mkuu wa kitengo cha Masoko
na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Bw.Kelvin Twisa.
Waziri Mkuu Mstaafu Bw.Frederick
Sumaye akipiga picha ya ukumbusho na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom
Tanzania wakati wa hafla ya kutoa tunzo kwa msimu ulioisha wa ligi kuu
ya Vodacom.Iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania katika hoteli ya Dobble
Tree Jijini Dar e Salaam.
MWANDISHI WETU
WAZIRI Mkuu mstaafu Frederick Sumaye
ameeleza kusikitishwa kwake na kupoteza umaarufu wa soka la Tanzania kwa
sasa ukilinganisha na miaka ya 1970.
Sumaye alisema hayo juzi
katika hoteli ya Double Tree By Hilton ya jijini Dar es Salaam katika
hafla ya kuwatunuku washindi mbalimbali waliofanya vema kwenye ligi kuu
ya Vodacom msimu wa 2011/2012.
Alisema hali hiyo inatokana na timu vilabu
nguli vya Simba na Yanga kubweteka kwa moja kuifunga nyenzake na kujiona
zimefika peponi kitu ambacho si dalili nzuri katika maendeleo ya soka.
“Simba kuifunga Yanga au Yanga kuifunga
Simba si kigezo kizuri cha kujiona ni timu nzuri, timu inatakiwa
iangalie ushindani kimataifa …ndiyo maana hata wakipangiwa timu kutoka
Misri, Ivory Coast n.k mnaingiwa na hofu kubwa,”alisema.
“zamani vilabu vya nje vilikuwa vikipangwa
na timu za Tanzania zinatetemeka lakini sisi sasa…kama tunataka kurudi
katika heshima yetu ya zamani tujipange kimataifa, “aliongeza Sumaye.
Aidha, Sumaye alisikitishwa na migogoro
katika vilabu na kusema inachangia pia kudidimiza soka hivyo amewataka
viongozi kuhakikisha wanafanya kazi kwa ushirikiano sambamba na
kuvihudumia ipasavyo vilabu vyao.
Sumaye ambaye ni mpenzi mkubwa wa mabingwa
wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba, alitumia fursa hiyo kuwaasa
mashabiki na wanachama wa timu za Simba na Yanga kuzomeana uwanja pindi
moja ya timu inapokuwa uwanjani.
“Muwe wapinzani katika michezo lakini si
uhasama, lazima tuwe na urafiki baina yetu na kuonyesha uzalendo zaidi
kwa Simba kuishangilia Yanga ikicheza na timu ya nje au Yanga
kuishangili Simba ikicheza na timu ya nje,”aliongeza.
Sumaye pia alitumia nafasi hiyo kuwapongeza
washindi wote na kuwataka kutovimbishwa vichwa na zawadi hizo badala
yake wazitumie kama kichocheo cha kujibiidiisha zaidi.
Awali Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa
Vodacom Kelvin Twisa alisema kampuni yake imetoa zaidi ya shilingi
milioni 113 kama zawadi za washindi hao na hivyo kufanya mwaka huu zwadi
kuongezeka tofauti na mwaka jana zilikuwa shilingi milioni 90.8.
“Tunajivunia kuwa wadhamini wa ligi kuu
bara ambapo vipaji vingi vimeonekana na viwango vya kuvutia pia katika
mechi zote na ndio maana hii leo tupo katika kutoa zawadi kwa
washindi,”alisema.
Katika halfa hiyo, ilitambulishwa tuzo mpya
inayohusisha wachezaji vijana waliofanya vema kwenye timu hizo ambapo
waliotwaa ni pamoja na Rashid Mandawa (Coastal Union), Hassan Dilunga
(Ruvu Shooting) na Frank Damayo aliyekuwa anaichezea JKT Ruvu na sasa
amesajiliwa Yanga ambapo kila mmoja alizawadiwa shilingi milioni moja.
Azam Fc ilifanikiwa kuongoza kwa kutwaa
tuzo tano ikiwemo ile ya nafasi ya pili iliyowapatia sh.mil.22, timu
yenye nidhamu (mil.7.8), kocha bora-Stewart Hall (mil.3.8), mfungaji
bora- John Bocco (mil.3.9) na mchezaji bora- Aggrey Morris (mil.3.3).
Aidha mabingwa Simba walitwaa mil.50, huku
kipa wake Juma Kaseja alitwaa tuzo ya kipa bora na kuzawadiwa Mil.3.3,
wakati Yanga ilizawadiwa mil.15 kwa kushika nafasi ya tatu na Martin
Sanya alitwaa tuzo ya mwamuzi bora na kuzawadiwa mil.3.8.
Ligi kuu ya Vodacom msimu wa 2011/2012
ilianza kutimua vumbi Agosti 20,2011 na kumalizikia Mei 6, 2012 na
kuvishirikisha vilabu 14 vikiwemo Simba, Yanga, Azam Fc, African Lyon,
Kagera Sugar, Mtibwa Sugara, Toto Africans, Moro United, JKT Ruvu, Ruvu
Shooting, Coastal Union, Polisi Dodoma na Oljoro JKT.
|
Mgeni rasmi, Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye kushoto akiwa na Meneja Masoko wa Vodacom Kevin Twisa 'Kifaa' |
|
Katikati
ni Sumaye, kulia Twisa na kuhsoto Mwenyekiti wa Simba SC, Alhaj Ismail
Aden Rage Mbunge wa Tabora Mjini (CCM) na mmiliki wa kituo cha Redio
cha Voice Of Tabora |
|
Ofisa Habari wa TFF, Boniphace Wambura kulia |
|
Katibu wa Simba SC, Evodius Mtawala kushoto na rafiki zake |
|
Twisa akihutubia |
|
Mwenyekiki wa Simba, Rage kulia, Mwenyekiti wa Azam, Mzee Mohamed Said katikati na Katibu Mkuu wa Yanga, Celestine Mwesigwa |
|
Waziri Mkuu wa zamani, kipenzi cha Watanzania, Sumaye |
|
Msaidizi wa Sumaye, Chombo kulia akizungumza na bosi wake |
|
Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah kulia, katikati Twisa wakiwa na Sumaye |
|
Wadau, Dina Ismail kushoto na Mohamed Mharizo |
|
Warembo wa Vodacom |
|
Maswahiba
wa miaka nenda, rudi, Grace Hoka, Mhariri wa BINGWA na Dina Ismail, wa
dinaismail.blogspot.com ambaye pia ni Mwandashi wa Habari za Michezo
Mwandamizi wa gazeti la Tanzania Daima |
|
Twisa kulia na Sumaye |
|
Rage na Sumaye wakiteta |
|
Sumaye |
|
Sumaye |
|
Sumaye |
|
Sumaye |
|
BIN ZUBEIRY |
|
Mzee Said kulia, Mwesigwa na Jaffar Iddi, Msemaji wa Azam |
|
Vimwana wa Vodacom na mataji, tuzo mbalimbali walizokabidhiwa washindi |
|
Refa bora, Martine Sanya kulia akipokea tuzo yake kutoka kwa Mh Sumaye. Kushoto ni Twisa |
|
Rage amkimpokelea tuzo Kaseja |
|
Mzee Said akipokea tuzo |
|
Mwesigwa akipokea hundi ya Yanga |
|
Mzee Said akipokea tuzo ya Azam FC |
|
Rage akipokea hundi ya Simba SC |
|
Angetile akipongezana na Mh Sumaye |
|
Wadau wa Yanga, katika picha ya pamoja na Mh Sumaye |
|
Wadau wa Simba SC katika picha ya pamoja na Mh Sumaye |
|
Angetile kulia na kushoto Wambura katika picha ya pamoja na Sumaye |
|
Frank damayo |
|
Mlimbwende |
|
Damayo akipokea tuzo yake |
|
Damayo akichukua msosi |
|
Mh Mbunge na kiungo wa zamani wa Simba SC, Rage 'akifakamia' |
JUMA
Kaseja, kipa wa Simba SC usiku huu ameibuka kipa bora wa Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara na kujinyakulia kitita cha Sh. Milioni 3.3 kutoka
kwa wadhamini Vodacom.
Katika
hafla ya kukabidhi tuzo za washindi wa Ligi Kuu ya Vodacom
zilizofanyika kwenye hoteli ya Double Tree By Hilton, Masaki, Dar es
Salaam, beki wa Azam FC, Aggrey Morris alishinda tuzo ya Mchezaji Bora
wa msimu wa Ligi Kuu.
Aidha,
Azam FC washindi wa pili wa Ligi Kuu walitwaa pia tuzo za timu yenye
nidhamu, wakati kocha waom, Stewart Hall kutoka Uingereza, aliibuka
kocha bora, mshambuliaji wake John Bocco ‘Adebayor’ aliibuka mfungaji
bora.
Katibu
Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Angetile Osiah pia
alitambulisha tuzo maalum kwa wachezaji chipukizi waliopandishwa kutoka
timu za vijana na kufanya vizuri katika timu za wakubwa.
Katika
tuzo hizo, kiungo mpya wa Yanga, Frank Damayo sambamba na Rashid
Mandawa wa Coastal Union na Hassan Dilunga wa Ruvu Shooting, kila mmoja
alitwaa Sh. Milioni 1.
Katika
hafla hiyo, ambayo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu wa zamani, Frederick
Sumaye, mwamuzi Martin Sanya alishinda tuzo ya refa bora, wakati bingwa
Simba alizawadiwa Milioni 50, mshindi wa pili Azam Milioni 22 na Yanga
aliyekuwa wa tatu Milioni 15.5.
No comments:
Post a Comment