Idadi ya watu wanaokimbilia kwenye kambi ya wakimbizi
 ya Dadaab imeongezeka na kufikia watu laki nne na elfu sitini na tano. 
Mashirika yanayotoa misaada yameonya kuwa kati ya idadi hiyo, takriban 
watu laki moja na elfu thalathini watakosa makaazi hivi karibuni na 
kuishi katika mazingira magumu ndani ya hema zisizoweza kuhimili dhoruba
 ya upepo na mvua.
                     
Msemaji wa shirika la Oxfam ameiambia BBC kuwa wakimbizi waliowasili kambini hivi karibuni hawana vifaa vyovyote, ila wanategemea mifuko ya plastiki na karatasi za maboksi na matawi ya miti.
                     
Mashirika yameonya kuwa kuanzia mwezi septemba 
kutakuwa na upungufu wa maji na vyoo halikadhalika huduma za afya. Kwa 
wakati huu wahudumu wa afya wamezidiwa na idadi kubwa ya watu -mfano 
uliopo wa vituo viwili vya afya katika kambi ya Hagadera inayohudumia 
wakimbizi 78,000.
Wakati vyombo vya habari vikizingatia kuwa kiwango cha wakimbizi wanaoingia kambini kinaliongana na mchango wa pesa zilizochangishwa, mtazamo umegeuka na wahisani kubadili maoni yao kuelekea kwingine kama janga la ukame uliolikumba eneo la Sahel.
Msemaji wa shirika la Oxfam ameiambia BBC kuwa wakimbizi waliowasili kambini hivi karibuni hawana vifaa vyovyote, ila wanategemea mifuko ya plastiki na karatasi za maboksi na matawi ya miti.
Kambi imefurika wakimbizi
Wakati vyombo vya habari vikizingatia kuwa kiwango cha wakimbizi wanaoingia kambini kinaliongana na mchango wa pesa zilizochangishwa, mtazamo umegeuka na wahisani kubadili maoni yao kuelekea kwingine kama janga la ukame uliolikumba eneo la Sahel.
No comments:
Post a Comment