Mwalimu wa warembo wa shindano la kumsaka Miss Sinza 2012, 
Mwajabu Juma, akitoa maelekezo kwa warembo hao wakati wa mazoezi yao ya 
mwisho kujiandaa na shindano hilo litakalofanyika kesho katika Ukumbi wa
 Mawela Social, karibu na Vatcan Hoteli, Sinza. Shindano hilo 
litasindikizwa na burudani kabambe na shoo ya kufa mtu kutoka kwa Bendi 
ya African Stars, watakaokuwa wakitambulisha pia baadhi ya nyimbo zao 
mpya kwa mara ya kwanza, pamoja na msanii wa Vichekesho kutoka kundi la 
Ze Commedy linalorusha michezo yake kupitia Televisheni ya Chanel 5, 
Masawe Mtata, ambaye pia atakuwa akitambulisha video ya wimbo wake mpya 
uitwao Uongo Kweli.
 Warembo hao wakiwa katika mazoezi yao ya pamoja ya shoo ya 
ufunguzi, jana jioni ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mwisho kuelekea 
shindano lao litakalofanyika kesho kwenye Ukumbi wa Mawela Social, 
karibu na Vatcan Hotel.
 Warembo hao wakiwa katika mazoezi yao ya pamoja ya shoo ya 
ufunguzi, jana jioni ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mwisho kuelekea 
shindano lao litakalofanyika kesho kwenye Ukumbi wa Mawela Social, 
karibu na Vatcan Hotel.
 Warembo hao wakiwa katika mazoezi yao ya pamoja ya shoo ya 
ufunguzi, jana jioni ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mwisho kuelekea 
shindano lao litakalofanyika kesho kwenye Ukumbi wa Mawela Social, 
karibu na Vatcan Hotel.

Warembo hao wakipozi kwa picha ya pamoja baada ya kumaliza mazoezi yao.
MASHINDANO ya kumsaka mrembo bora waKitongoji cha Sinza, Redds Miss
 Sinza 2012 yatafanyika kesho (Ijumaa) kwenye ukumbi wa Mawela Social 
Hall (Ten Star Lounge) uliopo karibu na hoteli ya Vatican City.
Mashindano hayo yatashirikisha jumla ya warembo 14 wanaowania taji 
la kituo hicho pamoja na kuiwakilisha kitongoji cha Sinza kwenye 
mashindano ya Kanda ya Kinondoni na baadaye Miss Tanzania.
Mbali ya taji (crown) na nafasi ya kuiwakilisha Sinza katika 
Mashindano ya Kanda ya Kinondoni, pia mshindi wa kwanza katika shindano 
hilo atajinyakulia kitita cha sh. 500,000/=  katika mashindano hayo 
yatakayopambwa na bendi ya African Stars “Twanga Pepeta International’ 
ambao watakuwa wakitambulisha baadhi ya nyimbo zao mpya na Msanii wa 
vichekesho wa kundi la Ze Comedy la Chanel 5, Masawe Mtata, atakayekuwa 
akitambulisha video na wimbo wake mpya wa Uongo Kweli.
Akizungumza na mtandao huu, Mratibu wa mashindano hayo kutoka 
kampuni ya Calapy Entertainment, Majuto Omary, alizitaja zawadi nyingine
 kuwa ni shs 400,000 kwa mshindi wa pili, sh. 300,000 kwa mshindi wa 
tatu . Mshindi wa nne na wa tano watapata sh. 150,000 kila mmoja na 
waliobaki watapata sh. 100,000 kila mmoja kama kifuta jasho.
Aidha Majuto, aliongeza kuwa mbali ya kutembea jukwaani kwa 
‘catwalk’ kwa warembo hao, pia kutakuwa na shindano la kusaka vipaji 
ambapo warembo watachuana  ili kumpata Mafoto Miss Talent Sinza 2012, 
ambapo mshindi atapata sh. 50,000 kutoka mtandao wa sufianimafoto.blogspot.com.
“Maandalizi yamekamilika na viingilio vitakuwa ni sh. 10,000 kwa 
viti vya kawaida na sh. 25,000 kwa vitu Maalum (VIP), tumeandaa shoo 
fupi na ya aina yake ili baadaye mashabiki wa fani ya urembo wa 
kitongoji cha Sinza wapate fursa ya kusugua kisigino na bendi ya Twanga 
Pepeta,” alisema Majuto.
Majuto aliwataja Warembo wanaowania taji hilo kuwa ni pamoja 
na Mariam Miraji, Naima Mohamed, Lulu Ambonela, Maria John, Judith 
Sangu, Eva Mushi, Vailet John na  Esther Mussa.
Warembo wengine ni Christina Samwel, Nahma Said, Aisha Ramadhan, Nancy Musharuzi, Brigitter Alfred na Merina Mushi.
Shindano hilo limedhaminiwa na Redds Premium Cold, Dodoma Wine, Gland Villa Hotel, Clouds FM, mtandao wasufianimafoto.blogspot.com, Brake Point, Fredito Entertainment, Screen Masters,  Lady Pepeta na flexi.





No comments:
Post a Comment