Kwa takribani muda wa juma moja
sasa kumekuwepo na taarifa katika vyombo vya habari na njia mbalimbali
za upashanaji habari, kuwa kampuni moja ya meli inayodaiwa kutoka Iran,
inayojulikana kwa jina la NITC (National Iranian Tanker Company),
inatumia bendera ya Tanzania, isivyo kihalali na kinyume kabisa na
sheria za nchi na zile za kimataifa, kwa malengo ambayo hayajulikani.
Pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar kutoa taarifa kwenye Baraza la Wawakilishi tarehe 2 Julai 2012
kukanusha taarifa hizo, Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
kinaitaka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia kwa
Waziri wa Mambo ya Nje na Waziri wa Uchukuzi kutoa taarifa kwa umma juu
ya hatua ilizochukua kuchunguza madai hayo.
Aidha, Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania ieleze iwapo utaratibu huo umezingatia kwa ukamilifu United
Nations Convention law of the Sea, kifungu cha 91, Geneva Convention
of Registration kifungu cha 6 na maazimio mengine ya kimataifa kuhusu
usajili wa meli kubwa pamoja na usafirishaji wa mafuta.
Maelezo yaliyotolewa na Serikali ya
Umoja wa Kitaifa Zanzibar inayoongozwa na CCM na CUF yanaibua maswali
kutokana na kampuni ya Philtex ya Dubai inayoelezwa kupewa uwakala na
Mamlaka ya Usafiri wa Baharini- Zanzibar Maritime Authority (ZMA)
kufanya kazi na makampuni mengine hivyo taarifa hizo hazijitoshelezi
katika kuondoa uwezekano kwamba meli za NITC zilipeperusha bendera ya
Tanzania.
Ili kujisafisha juu ya tuhuma hizo
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilipaswa kushirikiana na Serikali ya
Muungano kufanya uchunguzi wa kubaini msingi wa tuhuma hizo na kuchukua
hatua iwapo meli za NITC zilipeperusha bendera ya Tanzania bila
ridhaa ya serikali zote mbili.
Ikumbukwe kwamba hii si mara ya kwanza
kwa baadhi ya maofisa wa ZMA kutuhumiwa kuruhusu vitendo vilivyo
kinyume na sheria kama ilivyojitokeza wakati wa kashfa ya kuzama kwa
meli ya Spice Islender.
Kwa upande mwingine, Serikali ya
Muungano nayo haiwezi kukwepa kuwajibika kwa kuzingatia kuwa kuwa baadhi
ya taarifa hizo katika vyombo vya habari vimewanukuu mawaziri wa
serikali wakionekana kujikanyanga na kujikanganya juu ya suala hili
nyeti la bendera ya taifa, ambayo ni moja ya utambulisho wetu rasmi kama
Watanzania, kutumika kwa malengo yasiyojulikana na kampuni ya nje.
Moja ya vyombo vya habari hapa nchini,
vimewanukuu mawaziri husika, Waziri wa Uchukuzi, Harrison Mwakyembe na
Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Bernard Membe, juu ya
suala hilo.
Wakati Waziri Mwakyembe amenukuliwa
akisema kuwa anazo taarifa za suala hilo, lakini asingeweza kulitolea
kauli mpaka Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi wa Tanzania Zanzibar
azungumze, Waziri Membe yeye mbali ya kukiri kuwa kitendo hicho ni kosa
kisheria, anasema habari hizo zilikuwa za kushtushwa na ngeni kabisa,
huku akisema kuwa vyombo husika vitalichunguza kwa makini.
Ukimya wa serikali yetu ambayo kwa
hakika unatokana na udhaifu wake katika kuchukua maamuzi, sasa
umesababisha kitendo hicho kutafsiriwa kuwa Tanzania inaibeba na
kuisaidia Iran kukwepa vikwazo ambavyo nchi hiyo inatishiwa na mataifa
ya Magharibi, hasa Marekani na Umoja wa Ulaya, kutokana na malumbano ya
muda mrefu ambayo yanatokana na mataifa hayo kutumia mabavu na vitisho
kuzichagulia baadhi ya nchi nyingine duniani, nini cha kufanya na
rasilimali zake mathalani mzozo unaoendelea na Iran kuhusu urutubishaji
wa madini ya urani.
Si nia ya CHADEMA kuingia katika
mgogoro wa Iran na Mataifa ya Magharibi hapa kupitia mjadala wa madai
hayo yaliyoandikwa kwenye vyombo vya habari; lakini CHADEMA kinatoa
tamko kufuatia ukimya na kigugumizi kinachoikumba Serikali ya CCM, kila
inapohitajika kufanya maamuzi ya haraka, hasa kuwalinda watu wake na
hadhi ya utaifa wao na nchi yao ndani na nje ya nchi.
Ni kutokana na udhaifu wa serikali
hii, ambayo umekuwa ukijidhihirisha pia kwa kushindwa kupanga bajeti
inayojitegemea hasa kwa kutumia utajiri mkubwa wa rasilimali ambazo nchi
hii imebarikiwa, hali inayotufanya tuonekane taifa ombaomba na kupoteza
heshima mbele ya mataifa makubwa na madogo, kuwa hatuna uwezo wa akili
kuweza kujitegemea.
Utegemezi huu umefanya baadhi ya raia
wa Nchi nyingine mathalani Mbunge aitwaye Howard Berman wa Bunge la
Marekani, akiwa kama Mwenyekiti wa Kamati ya Masuala ya Nje, kupata
uwezo wa kuandika barua ya dharau na kejeli kwa Rais Jakaya Kikwete, juu
ya suala hilo la Meli za NIT kutuhumiwa kupeperusha bendera za
Tanzania.
Kupitia tamko hili, CHADEMA tunaitaka
serikali kutoa kauli madhubuti juu ya suala hilo ambalo tayari
limechukua sura ya mjadala wa kimataifa usiokuwa na tija yoyote kwa
mustakabali wa Watanzania. Suala la bendera ambayo ni utambulisho wa
taifa letu, haliwezi kuwa suala la mchezo tu, ambapo mawaziri wazima
hawawezi kutoa kauli za kina na kuchukua hatua zinazostahili.
Imetolewa tarehe 2 Julai 2012 na:
Hamad Mussa Yussuf
Naibu Katibu Mkuu Zanzibar
Tanzania
is seriously investigating allegations that it re-flagged Iranian oil
tankers in defiance of sanctions. A US congressman alleged last week
that up to 10 Iranian oil tankers had been re-registered in
Tanzania. But the East African nation's foreign minister said so far
there was no evidence to suggest this was true and he appealed for help
with the probe. The US and the European Union have just tightened
sanctions on Iran over concerns about its nuclear programme.
On Sunday, a complete European Union oil
embargo on Iran came into effect - in response to US legislation, which
sanctions any entity that deals with Iran's Central Bank. Tanzania's
neighbour Kenya on Wednesday said it had cancelled plans to import crude oil from Iran following threats of sanctions.
Flags of convenience
Howard Berman, who chairs the US House of Representative's Committee on Foreign Affairs, wrote to President Jakaya Kikwete last Fridayabout his concerns that Tanzania had allowed National Iranian Tanker Company vessels to re-flag. "If
Tanzania were to allow Iranian vessels to remain under Tanzanian
registry, we in the Congress would have no choice but to consider
whether to continue the range of bilateral US programs with Tanzania,"
the US politician warned.
In a briefing to journalists on
Thursday, Tanzania's Foreign Minister Bernard Membe said that if any
Iranian ships had been re-flagged, they would be removed from Tanzania's
shipping register. But he had received assurances from the Iranian
embassy and a shipping agent in Dubai that no Iranian ships have been
re-flagged. "We're calling on the international community, particularly
the United States and European Union, to determine whether or not the
statements... are correct or not," Mr Membe said. "If it is confirmed
that the ships flying Tanzania's flag are indeed from Iran, we will take
steps to deliberately obliterate the registration."
The BBC's international development
correspondent Mark Doyle says the use of so-called flags of convenience
is common, though controversial, for legitimate trade. But the flags are
also sometimes flown as a way of trying to hide the origin of vessels
and their cargo. On Wednesday, Sierra Leone's government said it would
ban any ships flying its flag from violating international
sanctions. The move came after reports that two ships, using a Sierra
Leonean flag of convenience, had carried Syrian oil products against the
aims of US and European sanctions imposed to try to prevent President
Bashar al-Assad's access to foreign exchange.
No comments:
Post a Comment