SENSA YA WATU NA MAKAZI NI MUHIMU KATIKA MIPANGO 
YA MAENDELEO - “Jiandae Kuhesabiwa 26 Agosti 2012” 
Sensa
 ya kwanza Tanzania ilifanyika mwaka 1910. Sensa nne za Mwisho 
zilifanyika baada ya Uhuru, katika miaka ya 1967, 1978, 1988 na 2002. 
Kulingana na sensa ya mwisho iliyofanyika mwezi Agosti 2002, idadi ya 
watu nchini Tanzania ilikuwa 34,443,603.
Sensa ya majaribio ya watu na makazi 
imefanyika nchini Tanzania katika kaya 5,000. Sensa hiyo imefanyika 
kwenye maeneo 44 ya kuhesabia watu katika mikoa 11.  Waziri Mkuu wa 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alitoa maelezo kwa wananchi kuhusu Sensa
 ya Majaribio ya watu na makazi ya mwaka 2011.
| Tanzania:Matokeo ya Sensa ya Watu 1967-2002 na Makadirio kati ya mwaka 2003-2025 | ||||
| Mwaka | Idadi | Mwaka | Idadi | |
| 1967 | 12,313,469 | 2006 | 38,250,927 | |
| 1978 | 17,512,610 | 2009 | 41,915,880 | |
| 1988 | 23,095,885 | 2010 | 43,187,823 | |
| 2002 | 34,443,603 | 2012 | 45,798,475 | |
| 2003 | 34,859,582 | 2015 | 49,861,768 | |
| 2004 | 35,944,015 | 2020 | 57,102,896 | |
| 2005 | 37,083,346 | 2025 | 65,337,918 | |
Maelezo ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu Sensa ya Majaribio ya Watu na Makazi ya Mwaka 2011. 
 
Maswali yaulizwayo mara kwa mara (Frequently Asked Questions)
Sensa ya Watu na Makazi ni nini?
Sensa ya Watu na Makazi ni utaratibu wa kupata na kurekodi habari kuhusu watu na makazi yao.
Bonyeza hapa kupata maswali na majibu zaidi. 
No comments:
Post a Comment