MAMA mzazi wa beki kisiki wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Zubeda Ally, ameutaka uongozi wa Yanga kumuongezea dau mtoto wake huyo iwapo hautamruhusu kucheza soka la kulipwa.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Zubeda alisema soka ndiyo kazi ya Cannavaro, hivyo iwapo uongozi utamzuia kucheza nje basi ni lazima umuongezee dau.
“Inawezekanaje uongozi uweze kumzuia mchezaji wakati soka ndiyo kazi yake? Wao hawawezi kumzuia kucheza nje kwani anahitaji kupanuka zaidi.
“Kama wao bado wanamhitaji na asitoke nje basi wamuongezee posho au kama hawawezi kumuongezea wamruhusu akacheze soka la kulipwa nje ya nchi,” alisema Zubeda.
Aliongeza kuwa, moja ya maendeleo ya wachezaji hapa nchini ni kufanikiwa kupata nafasi ya kucheza soka la kulipwa nje ya nchi, hivyo kama nafasi inapatikana halafu mchezaji anazuiwa ni kumrudisha nyuma.
Hivi karibuni kulikuwa na taarifa kuwa uongozi wa Yanga ulimzuia beki huyo kwenda kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa nchini Gabon.

No comments:
Post a Comment