My Web

Emmanuel

CONTACT

Tuesday, April 3, 2012

Nassari kumuoa Mdee?






UBUNGE
Jimbo la Arumeru Mashariki umebaki kuwa stori baada ya mgombea wa Chadema, Joshua Nassari kuibuka kidedea, lakini gumzo limebakia je, mheshimiwa huyo mteule atamuoa Halima Mdee (Mbunge wa Kawe-Chadema), kama alivyotamka wakati wa kampeni?

Katika mtifuano wa kuomba kura kwa wananchi ulioanza mwanzoni mwa Machi, mwaka huu, Nassari aliwahi kunogesha kampeni zake kwa kauli ya: “Watu wanasema sijaoa…nikishinda nitamuoa Halima Mdee na hivyo kulifanya jimbo hili kuwa na wabunge wawili.”

Nassari alikuwa akijibu swali la minong’ono kwamba, anaombaje ubunge wakati hana mke tofauti na mpinzani wake wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Sioi Sumari ambaye ana familia yake.
Baada ya mteule huyo wa Arumeru Mashariki kutoa kauli hiyo, gumzo la wakalia mikeka maneno ya watu lilihamia kwenye Mitandao ya Kijamii ya Facebook na Twitter kwamba huenda kijana huyo alimaanisha alichotamka.

Hata hivyo, jitihada za kumpata Nassari ili azungumzie kinagaubaga ‘ahadi’ yake hiyo hazikuzaa matunda kufuatia simu yake ya mkononi kutopatikana hewani.

Kuhusu Halima ambaye naye ni ‘singo’ kitengo chetu cha mawasiliano kilikwama kusikia tamko lake juu ya kionjo kilichotolewa na mbunge wa Arumeru kwamba baada ya kushinda atamfanya kuwa ‘misezi’ wake

No comments:

Post a Comment

New