Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa akiwa na Mkewe, anayefuatia ni Naibu Katibu
Mkuu, Dkt. Asha-Rose Migiro akiwa na Mumewe, Profesa Cleophas Migiro
wakisubiri kusalimiana na wageni waalikwa wakati wa hafla ambayo Ban Ki
Moon aliandaa maalum kwajili ya kumuaga msaidizi wake wa Karibu.
Profesa Migiro akiwa na Bint yake, Chansa- Jasmin wakifuatilia hafla hiyo kwa makini.
Ban
Ki Moon akizungumza wakati wa hafla hiyo ambapo amempogeza na
kushukurusu sana Migiro kwa namna alivyokuwa mshauri wake na mwalimu
wake ambaye a anasema kwa ualimu wake anampa alama ya plus plus plus.
akatumia hafla hiyo kutangaza kwamba anamteua Dkt. Asha- Rose Migiro
kuwa mjumbe wake maalum katika masuala ya ukimwi na ugonjwa wa ukimwi
Barani Afrika. Migiro anaondoka baada ya kuutumikia Umoja wa
Mataifa kwa miaka mitano na nusu.
Dkt.
Asha-Rose Migiro akizungumza wakati wa hafla hiyo, akatoa shukrani
zake kwa Ban ki Moon kwa kumpatia heshima hiyo ya kihistoria ambayo
haita kaa ifutike na kwamba ameupokea uteuzi huo kwa mikoni miwili na
hasa kutokana na kwamba tatizo la ugonjwa wa ukimwi ni tatizo ambalo
analichukulia kwa uzito wa aina yake.
Na
Chiaziiiiiiiiiiiiiiiii iligongeshwa, Katibu Mkuu akitakiana kila la
kheri na Naibu Katibu Mkuu, Dkt. -Asha Rose Migiro, kulia ni Mkurugenzi
wa Ofisi ya Naibu Katibu Mkuu, Bw. Anyanga.
Dkt. Migiro akimtambulisha Mume wake kwa mmoja wa wageni waalikwa.
Bi Amina Mtengeti akinywa kinywaji chake baada ya kigongeshana chiaziiiiii na Katibu Mkuu Ban Ki Moon.
Dkt. Asha- Rose Migiro akiteta jambo na Katibu Mkuu Ban Ki Moon.
Hata
kupiga picha naweza. Naibu Katibu Mkuu akinyaka tukio hili la picha
wakati Katibu Mkuu Ban Ki Moon akizungumza na Bint wa mwisho wa Migiro
Chansa Jasmin.
Sehemu ya wageni waalikwa.
Na Mwandishi Maalum
Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, amemteua Naibu Katibu Mkuu
anayemaliza muda wake, Dkt, Asha-Rose Migiro kuwa mjumbe wake maalum
katika masuala ya ukimwi na ugonjwa wa ukimwi Barani Afrika.
Ban
Ki Moon ametangaza uteuzi huo wakati wa hafla maalum aliyoiandaa
mahsusi kwaajili ya kumuaga Naibu Katibu Mkuu wake,ambaye anahitimisha utumishi wake wa miaka mitano na nusu katika nafasi ya Unaibu katibu Mkuu.
Hafla
hiyo imefanyika siku ya alhamisi katika viunga vya Umoja wa Mataifa,
na kuhudhuriwa na wageni waalikwa mbalimbali wakiwamo mabalozi na wakuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa.
“Ninatangaza rasmi kwamba ninamteua dkt. Asha- Rose Migiro kuwa mjumbe wangu maalum katika masuala ya ukimwi na ugonjwa wa Ukimwi Barani Afrika. Akasema Ban Ki Moon tangazo lililoshangiliwa kwa nguvu na wageni waalikwa.
Akiongea kwa hisia, Ban Ki Moon, ameeleza
kwamba ingawa Migiro alikuwa naibu katibu mkuu wake, lakini amekuwa
mwalimu wake, amejifunza mengi toka kwake na daima ataendelea kuenzi
mchango wake mkubwa.
“ Kama
ni kuvaa viatu vyake, naweza kusema ningechekesha sana, kwa ufupi
siwezi kuvaa viatu vya Migiro, amekuwa msaada mkubwa sana kwangu,
ameniwakilisha vema kila mahali nilipomtuma hata katika mazingira magumu na ya hatari, kote ameniwakilisha vema sana, kama mwalimu wangu, na kama profesa wangu anastahili alama ya juu sana” akasema Ban Ki Moon na kushangiliwa.
Akamuelezea Migiro kama kiongozi si tu mwadilifu, lakini mwanadiplomasia aliyebobea, aliyefanya kazi kubwa,ngumu na nzito kwa moyo mkunjufu, uhodari , umakini, na uadilifu wa hali ya juu sana.
“ Siyo rahisi kuelezea yale aliyoyafanya nyuma ya pazia, namna gani alivyochapa kazi kwa nguvu,
yapo mengi makubwa ambayo Migiro ameyafanya na kuyakamilisha kwa
uadilifu wa hali ya juu. Migiro ni mwanadiplomasia aliyebobea lakini ni
mtu wa vitendo, vitendo ambavyo lazima utaona matunda yake” akabainisha
Ban Ki Moon
Na kuongeza “ Migiro amefanya kazi na viongozi wagumu, kiwamo aliyekuwa Rais wa Libya Muammar Quadaff aliyethubutu hata kumrushia katiba ya Umoja wa Mataifa, amezikuna nyonyo za watu wengi wakiwamo watu wanyonge na wenye matatizo mbalimbali. Migoro unaondoka, lakini Umoja wa Mataifa hauta sahau mchango wako. Hapa ni nyumbani kwako, na nitaendelea kuomba msaada wako na ushirikiano wako, bado nitaendelea kukuhitaji” akasisitiza Ban Ki Moon
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, akatumia fursa hiyo kuishukuru
serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kumruhusu Migiro
kwenda kuitumikia jumuia ya kimataifa.
“ Ninapenda kutoa shukrani zangu za pekee kwa jamhuri ya muungano wa Tanzania, kwa kumtoa Migiro katika utumishi wake wa Umma kuja kunisaidia , kwa serikali ya Tanzania na watanzania nasema asanteni sana” akasema Ban Ki Moon..
Kwa
upande wake, Naibu Katibu Mkuu dkt. Asha-Rose Migiro amesema anaupokea
kwa mikono miwili uteuzi wa kuwa mjumbe maalum wa Katibu Mkuu katika
masuala ya Ukimwi.
Akasema masuala ya ukimwi na ugonjwa wa ukimwi, ni eneo ambalo limo ndani ya moyo wake na kwamba anashukuru kuona kwamba Katibu Mkuu anamuamini kwamba anaweza kumsaidia. Akaahidi kwam atalitekeleza jukumu hilo kwa heshima kubwa.
Akamshukuru
Ban Ki Moon, kwa kumuamini kwamba anaweza kumsaidia kama naibu Katibu
Mkuu, na akamshukuru pia kwa ushirikiano mkubwa na uhusiano mkubwa
uliojengeka kati yake na Ban Ki Moon lakini pia kati yake na wasaidizi
wake. Ushirikiano ambao anasema ulichagiza utendaji kazi kufanikisha dira na matarajio ya Katibu Mkuu.
“Katibu Mkuu amenipa heshima ya kihistoria, heshima ya kuwa msadizi wake, ni heshima kubwa kwangu na kwa yeyote
atakayekuja kuandika historia yangu, kwa namna yoyote ile hawezi
kukwepa kumtaja Ban Ki Moon, naomba nikushukuru sana kwa heshima hii
kubwa uliyonipa” akasema Migiro.
Hafla hiyo pia imehudhuriwa na familia ya Naibu Katibu Mkuu ikijumuisha mume wake, Profesa Cleophas Migiro, mdogo wa Naibu Katibu Mkuu, Bi. Amina Mtengeti na mtoto wa mwisho wa Migiro Chansa Jasmin.
Naibu
Katibu Migiro anakuwa mwanamke wa pili kushika wadhifa huo na mwanamke
mwafrika wa kwanza. Lakini pia ni naibu katibu mkuu ambaye amehudumu
katika wadhifa huo kwa miaka mitano na nusu.
No comments:
Post a Comment