Tume
 ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za Kulevya iliyopo chini ya Ofisi ya 
Waziri Mkuu ndio chombo kilichopewa jukumu la kuratibu masuala yote 
yanayohusu dawa haramu za kulevya hapa nchini kupitia mikakati yake 
mikuu miwili ya kuzuia matumizi  na ule wa kuzuia biashara haramu ya dawa za kulevya. 
Ikumbukwe
 kwamba biashara ya dawa za kulevya ndio huchochea matumizi ya dawa hizo
 na kuleta athari kwa mustakabali wa Taifa letu kiafya, kijamii, 
kiuchumi, kisiasa na hata kimazingira.
 Tume
 ikishirikiana na vyombo vya dola hususani Kikosi kazi cha Kupambana na 
Dawa za Kulevya imeshuhudia ongezeko la biashara hiyo haramu kutokana na  kiasi
 kikubwa cha dawa za kulevya kinachokamatwa. Mfano; Takwimu zinaonesha 
kuwa mwaka 2011 kilo 264.3 za dawa ya kulevya aina ya heroin zilikamatwa
 ikilinganishwa na kilo 185.8 zilizokamatwa mwaka 2010 ikiwa ni ongezeko
 la 42% la kiasi cha heroin kilichokamatwa katika kipindi cha mwaka 
mmoja tu. 
![]()  | 
| mtumia madawa ya kulevya | 
Aidha,
 mwaka 2011 kilo 126 za dawa ya kulevya aina ya cocaine zilikamatwa 
ikilinganishwa na kilo 63 zilizokamatwa mwaka 2010, ambalo ni ongezeko 
la 100%. Ongezeko hili kubwa la ukamataji linaashiria kukua kwa biashara
 haramu ya dawa za kulevya kunakorahisisha upatikanaji wa dawa hizo na 
kuchangia kuongezeka kwa idadi ya watumiaji nchini.
Ingawa
 hakuna takwimu sahihi za watumiaji wa dawa za kulevya nchini, 
inakadiriwa takribani watu 150,000 hadi 500,000 wanatumia dawa hizo. 
Aidha, ingawa sehemu ndogo tu ya watumiaji wa dawa za kulevya hufika 
katika vituo vya afya kwa minajili ya kutafuta tiba kumekuwa na ongezeko
 mahitaji ya tiba katika vituo mbalimbali vya afya. 
Hali
 hii inazidi kudhihirisha kuwa pamoja na ongezeko la biashara ya dawa za
 kulevya matumizi ya dawa hizi nayo yameongezeka. Kwa mfano, katika 
kipindi cha mwaka 2011 jumla ya watumiaji 4,684 wa dawa za kulevya walihudumiwa katika vituo vya afya vya manispaa na majiji nchini.
 Halikadhalika,
 takwimu kutoka hospitali ya Mirembe zilionyesha ongezeko la vijana 
waathirika wa dawa za kulevya kutoka 290 mwaka 2000 hadi kufikia 569 
mwaka 2005 sawa na nyongeza ya 96.2%. Katika kukabilina na hali hii 
serikali ya Tanzania ilishirikiana na ile ya Marekani ilianzisha tiba
 ya majaribio kwa wanaojidunga heroin kwa kutumia dawa ya methadone 
mwezi Mei, 2011 ili kuwapunguzia hatari ya maambukizi ya VVU miongoni 
mwao. 
Hadi kufikia mwezi Desemba 2011 wajidunga heroin wapatao 250 walikuwa wakipata tiba hiyo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Matumizi na biashara ya dawa za kulevya huleta huathiri jamii husika kwa namna mbalimbali ikiwemo kiafya, kiuchumi na kisiasa. Athari za kiafya huhusisha uwezekano wa kupata maradhi ya moyo, ini, mapafu, meno, figo, tumbo, ngozi, maradhi ya akili, kansa, ugumba, kuzaa watoto wafu, utegemezi, uteja, kusababisha au kupata ajali na hata vifo. 
Aidha,
 matumizi ya dawa za kulevya huchochea maambukizi ya VVU kutokana na 
kushirikiana sindano kwa wale wanaojidunga na kufanya ngono zisizo 
salama. Kwa wale waliokwisha ambukizwa VVU wanapoendelea kutumia dawa za
 kulevya kinga yao hushuka haraka zaidi ya wale wasiotumia dawa hizi na 
kujiweka katika hatari ya kupata magonjwa nyemelezi kama vile homa ya 
ini, kifua kikuu, kaswende na kisonono. 
Katika
 utafiti uliofanyika mkoani Dar es Salaam mwaka 2006 ulionyesha kuwa 42%
 ya wajidunga walikuwa wamepata maambukizi ya VVU. Utafiti mwingine 
uliofanyika kwa wajidunga wilayani Temeke mwaka 2010 na Asasi ya 
Medicins Du Monde uligundua 34.8% ya wanaojidunga heroin waligundulika na VVU na wengine 27.7% waligundulika na virusi vya homa ya ini.
Kiuchumi,
 matumizi ya dawa za kulevya ambayo huathiri zaidi vijana ambao ndio 
nguvukazi ya Taifa hurudisha nyuma maendeleo ya nchi kwa kuongeza 
wategemezi hivyo kupunguza uzalishaji. Vilevile, serikali inaongezewa 
mzigo kwa kutumia rasilimali ambazo zingeweza kutumika katika sekta 
nyingine za maendeleo katika kukabilina na tatizo hili. 
Biashara
 na matumizi ya dawa za kulevya huvuruga mfumo wa maisha katika jamii 
ikiwa ni pamoja na kumomonyoka kwa maadili ikiwemo biashara ya ngono, 
kudharaulika kwa tamaduni za jamii, rushwa, kushuka kwa kiwango cha 
elimu, utoro mashuleni na kazini na migogoro ya kifamilia ambayo 
inachangia kuvunjika kwa ndoa na ongezeko la watoto wa mitaani. 
Kwa
 upande wa kisiasa, biashara ya dawa za kulevya huweza kusababisha 
kuchaguliwa kwa viongozi wanaofanya biashara hiyo hivyo kudhoofisha 
jitihada za serikali za kudhibiti  biashara
 haramu ya dawa za kulevya. Aidha, watumiaji wanaweza kurubuniwa 
kirahisi kuchagua wanasiasa wanaojihusisha na biashara hiyo haramu. 
Kiusalama,
 matumizi na biashara ya dawa za kulevya huhatarisha usalama katika 
jamii kwa kuongeza uvunjifu wa amani ikiwa ni pamoja na ongezeko la 
vitendo vya wizi, utapeli, uporaji, ubakaji na ajali za barabarani. 
Biashara
 ya dawa za kulevya pia huweza kuongeza matukio ya ugaidi, utekaji 
nyara, vita vya wenyewe kwa wenyewe au vita kati ya serikali na magenge 
ya wafanyabiashara wa dawa za kulevya kama inavyotokea hivi sasa katika 
nchi ya Mexico. Vilevile, kuna hatari ya uharibifu wa misitu na kukauka 
kwa vyanzo vya maji iwapo kilimo cha dawa hizi utafanyika kwenye misitu 
au kwenye vyanzo vya maji. 
Mafanikio
Pamoja na changamoto mbalimbali zinazoikabili Tume pamoja na wadau wake imeweza kufanikisha mambo yafuatayo:-
(i)        Kukamatwa kwa kiasi kikubwa cha  dawa za kulevya za heroin na cocaine 
(ii)      Elimu ya dawa za kulevya imeweza kufikia watu wengi zaidi ikiwemo waumini wa dini mbalimbali kupitia viongozi wao;
(iii)    Kukua kwa ushirikiano kati ya vyombo vya dola na Kikosi Kazi kulikosaidia kupambana na biashara ya dawa za kulevya
(iv)    Uanzishaji wa Huduma ya tiba ya majaribio kwa wajidunga wa heroin kwa kutumia dawa ya methadone 
(v)      Kuanzishwa kwa baraza la viongozi wa dini kwa ajili ya kuwahamasisha waumini wao kushiriki katika vita dhidi ya dawa za kulevya.
Changamoto
(i)   Kuendelea kuwepo kwa unyanyapaa katika jamii dhidi ya watumiaji wa dawa za kulevya kunawakosesha fursa ya kupata tiba. 
(ii)  Uelewa mdogo wa masuala ya dawa za kulevya huifanya jamii ione kama  uraibu wa dawa za kulevya ni jambo la kujitakia na si ugonjwa;
(iii) Kushamiri kwa kilimo cha bangi nchini;
(iv) Kuwepo
 kwa mipaka mingi, ukanda mrefu wa pwani (bahari na maziwa), vipenyo 
vingi na njia zisizo rasmi katika mipaka ya nchi yetu hali 
inayorahisisha biashara ya dawa za kulevya;
Mikakati ya Baadaye
(i)           Kuanzisha huduma za makazi ya kupata nafuu (sober houses) kwa watumiaji dawa za kulevya Tanzania bara;
(ii)         Kuendelea
 kuhamasisha watumiaji wa dawa za kulevya na waliopata nafuu kuhudhuria 
mikutano ya kuacha na kutorudia matumizi ya dawa za kulevya (Narcotic 
Anonymous -NA);
(iii)       Kuendelea kutoa elimu kwa umma kwenye matukio maalum ya kitaifa,  semina, makongamano, luninga, redio na machapisho;
(iv)       Kuwawezesha vijana wanaoacha kutumia dawa za kulevya kwa kuwapa stadi za maisha ili waweze kujitegemea;
(v)         Kupanua huduma za kupunguza maambukizi ya VVU miongoni mwa watumiaji;
(vi)       Kuweka sera ya Taifa, kurekebisha sheria na muundo wa chombo cha kudhibiti dawa za kulevya.
Aidha, Tume inaukaribisha umma wa Tanzania kuadhimisha Siku
 ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Ulimwenguni ambayo huadhimishwa tarehe 
26 Juni ya kila mwaka ikiwa ni ishara ya kuungana na mataifa mengine 
duniani yaliyo kwenye harakati za kupambana na matumizi na biashara 
haramu ya dawa za kulevya. 
Mwaka
 huu maadhimisho haya ya kitaifa yatafanyika Mkoani Dar es Salaam, 
Wilaya ya Kinondoni kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Tandale. Kauli 
mbiu ya maadhimisho haya ni“Tujenge Jamii yenye Afya bila Dawa za Kulevya: Tutoe maoni ya Katiba na Kushiriki sensa ya mwaka 2012 


No comments:
Post a Comment