Timu
ya England ya soka imeondolewa katika mashindano ya Euro 2012, baada ya
kufungwa na Italia usiku wa Jumapili katika robo fainali, kwa kufungwa
magoli 4-2 ya penalti mjini Kiev, Ukraine, kufuatia muda wa kawaida na
dakika 30 zaidi kumalizika kwa timu hizo mbili kutofungana.
Italia sasa itapambana na Ujerumani katika mechi ya nusu fainali.
Alessandro
Diamanti alifunga bao la kuamua mshindi katika mikwaju hiyo ya penalti,
baada ya Ashley Young na Ashley Cole kukosa kufunga mabao kupitia
mikwaju waliyopiga.
Vijana
wa meneja Roy Hodgson ilikuwa wazi walilemewa katika mchezo mzima,
lakini ni hali ya imani na uvumilivu iliwafanya kuwa na matazamio ya
kuishinda Italia.
Italia iliweza kugonga mwamba, na bao la Antonio Nocerino lilikataliwa baada ya mwamuzi kusema aliotea mpira.
Kadri
mechi ilivyoendelea, ndivyo wachezaji wa England nao walionekana
wachovu, na ikielekea walitazamia bahati zaidi kuliko kujitahidi
kuimarisha kiwango cha mchezo wao, na penalti kwao bila shaka ikawa sio
za kutegemewa tena.
Baada
ya mechi, nahodha Steven Gerrard alisema: "Wachezaji walicheza kadri ya
uwezo wao wote. Nilidhani tungelipata bahati katika mikwaju ya penalti,
lakini mambo hayakuwa hivyo. Ukiongoza katika penalti, unashikilia
matumaini kwamba mambo yatasalia hivyo, lakini Italia ndio waliokuwa na
bahati. Vijana waliokuwa walinzi walifanya kazi nzuri mno, na kuiletea
nchi fahari, lakini tunarudi nyumbani na mioyo ya huzuni, na hili ni
jambo gumu kulikubali."
No comments:
Post a Comment