MADA
DAWA YA MBU ALIYEKUAMBUKIZA MALARIA SIO KUMPIGA BUNDUKI,NI EXPEL TU..
HASIRA HASARA
 Idadi ya chuki na hasira unazobeba moyoni mwako kutokana na vile  wapenzi wako wa zamani walivyokufanyia vitu ambavyo unadhani hukustahili  kufanyiwa,aidha kwa kupigwa kibuti bila kutegemea,au mpenzi kuchukua  kipusa kipya na kukutosa kwa kashfa,au kuwa cheated pale ulipopenda  sana,kutakufanya uwe kilema wa kupenda siku za usoni.
 Kamwe usipende kuingia mahusiano mapya bila kusamehe kile kilichotokea  ...kwenye past relationship,ukifanya hivyo,utakuwa kama mtu aliyegongwa  na nyoka,hata akiona mkanda mweusi anashtuka.
 Utajikuta  unaishi kwa dalili,ukiona wingu kidogo unahisi kuna el nino inakuja  kumbe ni watu tu wamechoma takataka nyumba ya Jirani....
  Jifunze kusamehe waliokutekenya moyo na kuuacha unacheka wenyewe,lasivyo  utajikuta unalalamika kwamba huwezi kupenda tena kumbe kosa ni la kwako  umeshindwa kuachilia visasi vya Past.Dawa ya mbu aliyekusababishia  Malaria kamwe sio kumpiga na bunduki kwa hasira,nunua Expel tu kwa Mangi  unampulizia kidogo tu.
 
 
 
          
      
 
  
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
No comments:
Post a Comment