Wema
Sepetu akizungumza muda mfupi baada ya watu kuchek sehemu ya movie yake
mpya aliyoizindua ya Super Star, ni movie yake ya kwanza na ndani kuna
mastaa kama T.I.D, Mr Blue, Barnaba, Hemed na wengine… baada ya hapa
Wema alitangaza safari ya kwenda kumpokea Omotola.
Wema
Sepetu na friends wakicheza ngoma iliyoandaliwa kwa ajili ya mapokezi
ya Omotola Airport Dar es salaam, ilikua ni saa tisa na dakika ishirini
usiku.
Amesema “mwanzoni tulikua tunataka kumleta Genevieve Nnaj lakini alikua busy na ratiba, tukamtafuta Ritha Dominic lakini gharama zake zilikua juu alikua anataka dola elfu 23 za kimarekani, nikaona itakua ngumu kwetu kwa sababu tunafanya wenyewe bila kuwa na udhamini baada ya kuhangaika ndio tukampata Omotola.
Omotola atakuepo leo pale Girrafe Ocean View kwa ajili ya family day, toka jana alitakiwa kuwa kwenye uzinduzi wa movie lakini kutokana na kupata matatizo kwenye ubalozi wa Tanzania Nigeria alichelewa ndege na kuingia Tanzania usiku sana.
No comments:
Post a Comment