Zitto akiwasilisha hotuba ya bajeti kivuli.
Katika mjadala unaoendelea Bungeni kuhusu Bajeti, baadhi ya wabunge
wameeleza kwamba Bajeti Kivuli haikuonyesha vyanzo vya mapato na hivyo
kuita ni vyanzo sifuri. Ukweli ni kwamba tumeweka vyanzo vya mapato ya
ndani kwa ujumla bila kuainisha mapato ya kikodi ni ngapi, mapato yasiyo
ya kikodi ni ngapi na mapato ya Halmashauri ni kiasi gani. Hivyo
tunakiri kosa hili na tumechukua hatua ya kuainisha mapato hayo Kama
inavyoonekana kwenye jedwali hili hapa chini.MAPATO |
SHILINGI MILIONI
|
||
A | Mapato ya ndani |
11,889,078
|
|
i)mapato ya kodi (TRA) |
10,232,539
|
||
ii)Mapato yasiyo ya kodi |
1,163,533
|
||
B | Mapato ya Halmashauri |
493,006
|
Ninawatakia mjadala mwema wa Bajeti.
Kabwe Zuberi Zitto,Mb
Waziri wa Fedha na Uchumi Kivuli
19.06.2012
No comments:
Post a Comment