KUMBE NDEGE YA DANA AIRLINES ILIYOUA NIGERIA ILIFAHAMIKA KUWA MBOVU IKARUSHWA HIVYOHIVYO,DAH!
Ile ndege ya Dana Air MC Donnell Douglas MD 83, iliyoanguka juzi maeneo  ya Iju-Ishaga, Lagos Jumapili inajulikana kuwa na historia ya Ubovu  hata kabla haijanunuliwa kutoka kampuni ya  Alaska Airlines,ya Marekani  na  Dana Airlines ya Nigeria mnamo February 17, 2009.
 Ndege hii ilinunuliwa na Alaska Airline mnamo November 13, 1990.
Miaka 12 baadae mnamo November 4, 2002,Ndege hii ilipata hitilafu na  ikabidi igeuze njia kwa dharura baada ya kutokea moshi kwenye cabin  area.
August 20, 2006, Ilibidi abiria waondolewe kwa dharura  tena baada ya kutua uwanja wa  Long Beach, California, baada ya  kuonekana Moshhi tena kwenye cabin area,ila watu wakauchuna tu. Baada ya  matatizo haya mfululizo Alaska Airlines mnamo  August 21, waliipaki  ndege hiyo hadi September 11 2008 na wakaipeleka kwa matengenezo. Miezi 5  baadae baada ya matengenezo kumalizika, ndipo walipoiuza ndege hiyo  mnamo February 2009, kwa to Dana Airlines ya Nigeria.
Unaweza kuona  jinsi gani nchi za Africa zinakuwa Dampo la bidhaa chakavu na  Mbovu.Hatujui hili tatizo linatufundisha nini sisi kama Watanzania,maana  Usafiri wetu wa Anga nao uko dhoofuli hali,hatuna uhakika hata hizi  ndege wanazopaka rangi na kusema wamenunua ziko kwenye hali nzuri kiasi  gani kwa Usalama wetu.Mungu tu anatuokoa kwakweli!
Tukio la  karibuni,wiki chache tu nyuma,mnamo May 23,Abiria walilazimika kuchelewa  kuondoka kutoka uwanja wa Ndege wa Lagos baada ya ndege hii kupata  hitilafu tena kwenye mfumo wake wa Hydraullic.
Ila yote hii  haikutosha kutoa WARNING kwa Mamlaka ya hali ya hewa kuzuia ndege hii  kuendelea kutoa huduma za ndege bila matengenezo madhubuti hadi  ilipoanguka juzi na kuua Roho za watu 153 waliokuwa kwenye ndege hiyo.  Inasikitisha kuona picha za waliokufa,wengine wakiwa ni watu wa familia  moja,wakiteketea kwa uzembe huu.Hili liwe fundisho hata kwetu hapa  Tanzania,Usalama wa Ndege uchekiwe kabla hayajatokea maafa makubwa!
Historia inaonyesha ndege hii ilitengenezwa mwaka 1983 na ilirushwa kwa mara ya kwanza December 17, 1984
MABAKI YA NDEGE YA DANA BAADA YA KUANGUKA KWENYE KIJIJI
No comments:
Post a Comment