MADA VI FIKIRIA SANA
HATA MUUZA JENEZA HUSALI APATE WATEJA NA KUJIBIWA MAOMBI YAKE:
 Kitu kimoja kuhusu Mungu,hana upendeleo hata kidogo..Unaweza kudhani  kuna watu flani anawapendelea na kuwaonea baadhi,lakini kamwe hayuko  hivyo!
Fikiria,Jambazi kabla halijaenda kuiba linawaza,na  kumuomba Mungu liibe salama lisikamatwe,na linafanikiwa,Mungu  hajalala,ameona kila kitu...Wewe unalalamika kuibiwa mwenzio ameshapata  mkate wa kila siku...Ingawa hukumu yake Mungu anayo mkononi
Lakini umewahi kuwaza hili??
 Una mgonjwa hospitali yuko mahututi,mtu wa muhimu sana maishani  mwako,,,Ni mke/mme,unampenda kweli...Au pengine ni mzazi wako,Mama au  Baba,unaomba na kusali sana kwamba apone na kurejea...
By the  time wewe unasali na kuomba apone,Kuna mtu yuko huko mtaani,ana wiki  nzima hajauza Jeneza hata moja...Ana mke na watoto wa kulipa  ada...Anafunga na kusali sana Mungu amuangazie baraka kwenye biashara  yake...
Kipenzi chako,uliyemuombea sana...Anakufa.....Unakwenda  kwa Muuza Jeneza kununua ili umzike...Kwake yeye ni zaidi ya  Biashara...Mungu amejibu Maombi yake...Amepata hela,ya kula,na kulipa  Ada ya watoto..au hata kulipa kodi with expense ya kifo cha mpenzi  uliyemuombea...
Huyo ndio Mungu,sio tu Athumani,wala sio Sadiki....
 Muuza Jeneza anapiga sala ya Shukrani na anatoa sadaka kanisani kwa  kujibiwa maombi yake kwa muda muafaka,wakati wewe uko Msibani unalia kwa  Majonzi..
Mwacheni Mungu aitwe Mungu..
 
 
 
          
      
 
  
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
No comments:
Post a Comment