My Web

Emmanuel

CONTACT

Wednesday, May 6, 2020

WHO Considers Madagascar’s Herbal Drink as Possible Treatment for COVID-19


FEATURESTECHNOLOGY

Breaking: WHO Considers Madagascar’s Herbal Drink as Possible Treatment for COVID-19

Dede Ifayemi

May 5, 2020


SWITZERLAND, MAY 05 – Madagascar’s much touted herbal COVID-19 cure may have received some support from the World Health Organization (WHO) after the global health body stated that it welcomes innovations around the world including repurposing drugs, traditional medicines and developing new therapies in the search for potential treatments for COVID-19.

This was contained in a press release issued by the WHO on Monday evening.

“WHO recognizes that traditional, complementary and alternative medicine has many benefits and Africa has a long history of traditional medicine and practitioners that play an important role in providing care to populations. Medicinal plants such as Artemisia annua are being considered as possible treatments for COVID-19 and should be tested for efficacy and adverse side effects.

“Africans deserve to use medicines tested to the same standards as people in the rest of the world. Even if therapies are derived from traditional practice and natural, establishing their efficacy and safety through rigorous clinical trials is critical,” WHO stated in the release.

Today’s Echo understands that Madagascar is building a factory to mass-produce a drink from the extracts of the artimisia annua plant, which is used to treat malaria. The factory will be operational within a month, according to President Andry Rajoelina.

“Our researchers and scientists are doing the necessary to make our coronavirus remedy a drug that meets the standards,” he said on state TV.

Madagascar’s herbal drink has also received a boost from other African countries. The president of Tanzania, John Magufuli, has said he’s sending a plane to Madagascar to fetch the tonic, and Rajoelina said on Twitter that Equatorial Guinea’s vice minister for health had arrived in the country to procure an unknown quantity. Other countries that have shown interest are Senegal, Guinea-Bissau and Comoros, Rajoelina said.

African governments through their Ministers of Health adopted a resolution urging Member States to produce evidence on the safety, efficacy and quality of traditional medicine at the Fiftieth Session of the WHO Regional Committee for Africa in 2000.

Countries also agreed to undertake relevant research and require national medicines regulatory agencies to approve medicines in line with international standards, which include the product following a strict research protocol and undergoing tests and clinical trials. These studies normally involve hundreds of people under the monitoring of the national regulatory authorities and may take quite a few months in an expedited process.

WHO is working with research institutions to select traditional medicine products which can be investigated for clinical efficacy and safety for COVID-19 treatment. In addition, the Organization will continue to support countries as they explore the role of traditional health practitioners in prevention, control, and early detection of the virus as well as case referral to health facilities.

Over the past two decades, WHO has been working with countries to ensure safe and effective traditional medicine development in Africa by providing financial resources and technical support. WHO has supported clinical trials, leading 14 countries to issue marketing authorization for 89 traditional medicine products which have met international and national requirements for registration. Of these, 43 have been included in national essential medicines lists. These products are now part of the arsenal to treat patients with a wide range of diseases including malaria, opportunistic infections related to HIV, diabetes, sickle cell disease and hypertension. Almost all countries in the WHO African region have national traditional medicine policies, following support from WHO.

“As efforts are under way to find treatment for COVID-19, caution must be taken against misinformation, especially on social media, about the effectiveness of certain remedies. Many plants and substances are being proposed without the minimum requirements and evidence of quality, safety and efficacy. The use of products to treat COVID-19, which have not been robustly investigated can put people in danger, giving a false sense of security and distracting them from hand washing and physical distancing which are cardinal in COVID-19 prevention, and may also increase self-medication and the risk to patient safety.

WHO welcomes every opportunity to collaborate with countries and researchers to develop new therapies and encourages such collaboration for the development of effective and safe therapies for Africa and the world.

Tuesday, April 21, 2020

Update of Word

update of Corona
hiyo link ya dunia nzima  unaangalia hali ikoje inabadilika yenyewe kila siku inakupa taarifa sahihi za corona.

http://corona.tuply.co.za

Monday, April 20, 2020

KANISA LA KILUTHERI DAYOSISI YA KARAGWE LASITISHA IBADA> Askofu Benson Bagonza ametangaza kufunga Ibada na mikusanyiko

KANISA LA KILUTHERI DAYOSISI YA KARAGWE LASITISHA IBADA

> Askofu Benson Bagonza ametangaza kufunga Ibada na mikusanyiko ya Dayosisi ya Karagwe kuanzia Aprili 26, 2020 na kuwaasa Viongozi wengine wa Dini nao kusitisha Ibada badala ya kusubiri Serikali iwatake kusitisha 

Maambukizi Duniani ya Covid 19


who yawaasa watu kula mlo kamili


Tanzia


Faida za Ndimu

FAIDA ZA NDIMU KWA AFYA YA MWILI WA BINADAMU.


Fahamu kwanza Ndimu na limao zina utofauti katika virutubisho .. japo baadhi vinafanana.

Faida za Ndimu

1.Ndimu husafisha damu na kuondoa tatizo la homa.

2.Ndimu huondoa gesi tumboni kwa wenye matatizo ya tumbo kujaa gesi.

3.Ndimu husaidia kuondoa sumu mwilini.

4.Ndimu huondoa tatizo la allergy (Mchafuko wa damu).

5.Ndimu ukikamulia kwenye chai ya rangi huzuia sumu ya majani ya viwandani yasikudhuru.

6.Ndimu inaondoa kipara kwa wenye matatizo ya nywele kunyonyoka. Matumizi chukua maji ya ndimu changanya na mafuta ya zaituni kidogo kisha pakaa kichwani kaa muda wa masaa mawili kisha osha kichwa chako kwa maji ya kawaida. Tiba hii itakusaidia kukuza nywele zako kwa wale wenye tatizo la nywele kunyonyoka zitakuwa nyingi fanya hivyo kwa muda wa siku saba(7)

7.Ndimu inatibu kifua na mafua matumizi changanya maji ya ndimu na maji ya vuguvugu... kunywa mara nyingi.

8.Ndimu huondoa harufu mbaya kinywani (mdomoni)
.. kwa sababu inasaidia kuua bakteria wabaya wa mdomoni wanaosababisha mdomo kunuka.  
Matumizi tumia maji ya ndimu kwa kusuktua na kupigia mswaki asubui na jioni kwa muda wa siku 21  tatizo litaisha.

9.Ndimu inapunguza maumivu kama mtu amechomwa na msumari au vitu vyenye ncha kali au kujikata,, Kamua ndimu pakaa sehemu yenye tatizo tiba hii itakusaidia kidonda kipone kwa haraka.

10.Pia Ndimu ni nzuri kuitumia pale umalizapo kunyolewa haina haja ya kutumia spirit.
 Ndimu ni nzuri itakusaidia kuondoa kuondoa Vipele, Mba, na magonjwa yote ya ngozi.

Sunday, April 19, 2020

MUNGU NI MUWEZA WA YOTE

MUNGU WETU ANAWEZA

MAMA mmoja aligunduliwa kuwa na Virus Vya Corona, alichukuliwa hadi kwenye hospital ya wagonjwa wa ugonjwa huo unaendelea kuitesa dunia.
mama huyo baada ya kufikishwa hospital
madaktar walimfanyia vipimo kwa mara nyingine, jambo la kusitikisha ni kwamba, madaktari wale waligundua mama yule hana uwezekano wa kupona, kwani corona ilishamuathiri kwa kiwango kikubwa sana. ana saa4 za kuvuta pumzi,
namaanisha amebakiza masaa 4 apoteze maisha,kwani licha ya kuwa na corona, pia alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kisukari ulimpoteze kinga nyingi za mwili.

mama huyo alianza kulia kwa uchungu, ni baada kuambiwa hana nafasi tena ya kuendelea kutembea juu ya dunia, madaktar walimuacha hawakumpa dawa wala kumuhudumia kwa chochote, walimtelekeza mama huyo na kwenda kuhudumia wagonjwa wengine wenye uwezekano wa kupona huku wakisubiri mama huyo afe waje kutoa mwili wake kitanda alichokalia kiwekwe mgonjwa mwingine, kwani wagonjwa waliokuwa wanaletwa hospital hapo ni wengi mno.

"Sina matumaini ya kuishi Tena, Nakufa Mimi..." alisema yule mama huku akilia. lakini badae mama huyo alijiwa na matumaini ya kuendelea kuwa hai, ni baada ya kukumbuka mbinguni kuna MUNGU asiyeshindwa na lolote lile, Mama Yule Alipiga Magoti Chini Na Kuanza Kumlilia Mungu, akimuomba amponye ugonjwa anaumwa.

"Eee Mola Wangu Ukinichukua Mimi Nani Atakuwa Msaada Kwa Watoto Wangu? Niokoe Na Mauti, Niongezee Muda Wa Kuishi Bado Nahitajika Kwa Wanangu, Usiache Niangamie, Niokoe Mola Wangu, Hakika Mimi Ni ninakutegemea wewe, na Miongoni Mwa Wenye Kukuabudu..." Ni baadhi ya maneno yaliyomo kwenye maombi ya mama huyo, Aliyatamka huku akilia.

Hatimae Saa 4 Alizokuwa amebaki nazo Yule Mama zilifika na zikapita, madaktar walikuja kuchukua maiti lakini walikuta yule mama hajafa bado ni mzima, wakarudi na machela yao ikiwa tupu, kesho yake walikuja na machela yao, wakiamini tayari yule mama amesha kufa, lakin walimkuta bado Ni mzima, tena akionekàna kuwa mchangamfu zaidi ya Jana, Madaktar wale waliangaliana kwa mshangao, hakuna aliyejuwa Siri ya mama yule kuendelea kuwa hai Hadi mda ule, wakati vipimo vyao vilionyesha Mama Hana mda mrefu wa kuishi.
Madaktar walimsogelea mama na kumfanyia vipimo kwa Mara nyingine, hapo ndipo madaktar walizidi kuvishangaa vipimo vyao kwani vilionyesha Mama huyo haumwi Tena Corona wala kisuri.

"Mama umeponaje Hali ya kuwa sisi hatujakupa dawa yoyote?" Aliuliza Daktar mmoja, Mama yule alishinda kujibu swali hilo, Alianza kulia kwa furaha, akawaambia wale madaktar "MUNGU WETU ANAWEZA"
Hatimae Mama huyo aliruhusiwa kurudi nyumbani akiwa mzima wa Afya, watoto walimpokea Mama yao kwa furaha.

Ukiishi kwa kumtegemea Mungu utaishi kwa furaha Sana.
Mungu wetu ni anatupenda, anasikiliza maombi yetu na kuyajibu, Unapomuomba MUNGU na akaona unachelewa kujibiwa maombi yako, usichoke Endelea kuomba ipo siku utajibiwa, Mungu humjibu amtakae na kwa wakati aupendao.

Usisubiri umepatwa na tatizo ndio uanza kumuomba MUNGU akuondolee matatizo, Anza kuomba leo kabla haujapatwa na matatizo, muombe akukinge na matatizo, kwani siku zote kinga Ni Bora kuliko tiba.

Kwa pamoja tunamuomba Mungu muumba mbingu na Ardhi atuondolee Corona, Tanzania na Duniani kwa Ujumla.

Atulinde dhidi ya Magonjwa na Walimwengu wabaya.

NEEMA YA MOLA IWE NAWE DAIMA.

KAMA HAUPO BIZE UNAWEZA KUCOMMENT "AMEN"

Toka kwa Dkt Faustine Ndugulile (Mb)

*UFAFANUZI KUTOKA KWA DR FAUSTINE NDUGULILE, NAIBU WAZIRI WA AFYA KUHUSU BARAKOA NA MATUMIZI YAKE*

Kuna clip inazunguka mitandaoni nikiongelea kuhusu barakoa za kitambaa. Napenda kutoa ufafanuzi ufuatavyo:

1. Barakoa za N95 zinapaswa kutumika na watoa huduma wa afya wanaohudumia wagonjwa wa Covid-19. Barakoa hizi hazipaswi kuvaliwa mitaani, majumbani wala maofisini.

2. Barakoa za upasuaji (surgical masks) hizi zinapaswa kuvaliwa na watumishi wa afya ambao hawana direct contact na wagonjwa. Barakoa hizi pia zinaweza kuvaliwa na jamii kwenye maeneo ya mikusanyiko kwa muda wa masaa 4-6. Barakoa hizi hazipaswi kuvaliwa kutwa nzima na kurudia matumizi (re-use). 

Aidha, kumekuwa na sintofahamu kuhusu namna ya uvaaji wa barakoa za upasuaji. Barakoa hizi zinapaswa kuvaliwa kama ifuatavyo:

(a). Upande wenye rangi (blue, kijani, zambarau nk) unapaswa kuwa nje.

(b). Upande wenye chuma unapaswa kuwa juu.

3. Barakoa za kitambaa (cloth masks) *hazina ubora wa kinga kama N-95 au  surgical masks*, lakini *zinaweza kutumika kupunguza uwezekano wa maambukizi toka kwa mtu mmoja kwenda mwingine majumbani na sehemu za mikusanyiko*.  

Mambo ya kuzingatia ni pamoja na:

1. Kutumia vitambaa vya pamba.

2. Kutumia layers zaidi ya mbili katika utengenezaji wa barakoa hizo.

3. Kuwa na  barakoa angalau mbili ili kuruhusu kufanyiwa usafi wa mara kwa mara.

4. Barakoa zifuliwe kwa maji na sabuni na kupigwa pasi.


*NI MUHIMU KUKUMBUKA KUWA BARAKOA SIO MBADALA WA KUNAWA MIKONO NA KUZINGATIA UMBALI KATI YA MTU NA MTU (SOCIAL DISTANCING) BALI NI NYONGEZA YA HATUA HIZI.* 

Aidha, tuhakikishe barakoa zilizotumika hazitupwi ovyo na badala yale zichomwe moto ili kuepuka kuokotwa na kutumiwa 
na watu wengine.

 Vile vile, watu hawapaswi kuazimana barakoa iliyokwisha kutumika. Kila mtu awe na yake.

Mwisho, tuendelee kuzingatia maelekezo yanayotolewa mara kwa mara na Wizara ya Afya kuhusu hatua mbali mbali za kujikinga na ugonjwa huu.

Dkt Faustine Ndugulile (Mb)
19.04.2020

jinsi ya kujikagua kama una Maambikizi ya Covid 19

Maombi ya Asubuhi

Maombi ya asubuhi na faida zake

Ndege na wanyama huamka asubuhi na mapema wakimsifu Mungu. Watumishi wa Mungu wengi Walikua wakiamka asubuhi na kuomba. Baadhi yao ni Ibrahim,Daudi alipenda kuamka asubuhi na kuomba, katika Zaburi 88:13 LAKINI MIMI NIMEKULILIA WEWE, BWANA NA ASUBUHI MAOMBI YANGU YATAKUWASILIA na Zaburi 57:8, AMKA UTUKUFU WANGU, AMKA KINANDA NA KINUBI, NITAAMKA ALFAJIRI, maombi ya asubuhi kwa Daudi yalimfanya kuwa mshindi, Mungu aliupenda moyo wa Daudi.

Yakobo alipopigana na malaika akamwambia sitakuacha mpaka utakaponibariki, ilikua alfajiri na mapema! Matendo 16:25 Paulo na Sila waliomba alfajiri mapema sana, milango ya gereza ikafunguka, Yoshua alipenda kuamka alfajiri, na hata Yesu mwenyewe aliamka asubuhi na kuomba na kuna wakati aliwakuta wanafunzi wake wamelala akawauliza hamkuweza kukesha nami hata saa moja? Pia Mungu alipokua akiwatuma watumishi wake aliwatuma alfajiri na mapema, Yeremia 25:4 NAYE BWANA AMETUMA KWENU WATUMISHI WAKE WOTE, HAO MANABII, AKIAMKA MAPEMA NA KUWATUMA….. na Joshua 6:12 Yoshua akaondoka asubuhi na mapema, nao makuhani wakalichukua sanduku la Bwana.

Unapoanza kuomba asubuhi unamtangizia shetani kwamba mnaanza vita kwamba uko tayari kwa mapambano,unamtangazia adui yako, ugonjwa wako, tatizo lako kwamba kuanzia sasa hakupati maana umejitoa kupanga maombi yako kwa Mungu Zaburi 5:3 BWANA ASUBUHI UTASIKIA SAUTI YANGU, ASUBUHI NITAKUPANGIA DUA YANGU NA KUTAZAMIA.

Ningependa ufahamu faida za maombi ya alfajiri

1.UTAVIKWA NGUVU ZA MUNGU Kutoka 16:7 Na asubuhi ndipo mtakapouona Utukufu wa Bwana, kwa kuwa yeye asikia manung’uniko yenu mliyomnung’unikia Bwana.

2.HUTAINGILIWA NGUVU ZA GIZA, maana umefunikwa na nguvu za Mungu, mapepo, magonjwa, havina uwezo kuingia kwenye maisha yako, vifungo vyote vya shetani, nira zake, mizigo yake vitaharibiwa na kuwekwa huru Mathayo 11:28 NJOONI KWANGU, NINYI NYOTE MSUMBUKAO NA WENYE KULEMEWA NA MIZIGO NAMI, NAMI NITAWAPUMZISHA. ISAYA 10:27 TENA ITAKUA KATIKA SIKU HIYO MZIGO WAKE UTAONDOKA BEGANI MWAKO, NA NIRA YA SHINGONI MWAKO, NAYO NIRA ITAHARIBIWA, KWA SABABU YA KUTIWA MAFUTA,

3.UTAKUA MBALI NA MAONEVU, SHETANI NA MALAIKA ZAKE, Zaburi 105:14-15 Hakumwacha mtu awaonee, hata wafalme wake aliwakemea kwa ajili yao, akisema, msiwaguse masihi wangu, wala msiwadhuru nabii zangu. Mungu anatuita masihi

4.TUKIAMKA ASUBUHI TUNAVIKWA HAKI ISAYA 54:14-17, Utathibitika katika haki ….kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa, na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utahukumu kuwa mkosa, huu ndio urithi wa watumishi wa Bwana, na Haki yao inayotoka kwangu mimi, Asema BWANA

5.KUINULIWA KUTOKA MAVUMBINI HADI UTUKUFU Zaburi 113:7-9 Humwinua mnyonge kutoka mavumbini, 1 Sam 2:7-8 …..humwinua mnyonge kutoka mavumbuni, humpandisha mhitaji kutoka jaani…

6.UNAKUA NA BIDII KATIKA KAZI ZAKO, mtu anayeomba asubuhi na mapema ana bidii kwa kazi yake, anafanikiwa kimwili na nyumba yake wanafanikiwa. Kuamka asubuhi ni kuwa shahidi mwaminifu wa Yesu Waebrania 10:38 LAKINI MWENYE HAKI WANGU ATAISHI KWA IMANI, NAYE AKISITASITA, ROHO YANGU HAINA FURAHA NAYE, Waebrania 11:6 LAKINI PASIPO IMANI HAIWEZEKANI KUMPENDEZA, KWA MAANA MTU AMWENDEAYE MUNGU LAZIMA AAMINI KWAMBA YEYE YUKO, NA KWAMBA HUWAPA THAWABU WAMTAFUTAO

7.UTAKUA HAI, MWENYE KUKUA KIROHO. Kilicho hai kinaongezeka na kukomaa ili mtu akue anahitaji chakula ndio NENO la Mungu ambapo UNACHANUA, Mark 4:1-20, Hosea 14:5 NITAKUWA KAMA UMANDE WA ISRAELI,NAYE ATACHANUA MAUA KAMA NYIRORO, NA KUIENEZA MIZIZI YAKE KAMA LEBANONI

8.UTAZAA MATUNDA, hivyo hutakatwa na kutupwa motoni John 15:1-6, Luka 3:9 NA SASA HIVI SHOKA LIMEKWISHA KUWEKWA PENYE MASHINA YA MITI; BASI KILA MTI USIOZAA MATUNDA MAZURI HUKATWA NA KUTUPWA MOTONI. Matawi yanayozaa yanasafishwa matawi yasiyozaa yanakatwa, Mtu kama ulikua na tabia haubadiliki, ukiaomba asubuhi, hofu ya Mungu itakaa ndani yako na hutatenda dhambi tena, mfano kama ulikua na tabia ya kutukana kinywa chako kinakamatwa! (haongei lugha chafu) UTUKUFU WA MUNGU UNAKUFUNIKA

*ASUBUHI NJEMA,SIKU NJEMA*

New