My Web

Emmanuel

CONTACT

Saturday, June 30, 2012

MREMBO LISA JENSEN ANYAKUA TAJI LA REDDS MISS WORLD KUWAKILISHA TANZANIA MISS WORLD



Mrembo Lisa Jensen akipunga mkono kwa wapenzi wa masuala ya urembo waliohudhuria katika shindano dogo la Redds Miss World Tanzania lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye jijini Dar es salaam na kushirikisha warembo 10 waliowahi kushiriki mashindano hayo miaka mbalimbali iliyopita, Lisa Jensen ataIwakilisha Tanzania katika shindano la Miss World litakalofanyika nchini Mongolia mwishoni mwa mwaka huu
Miss Tanzania Salha Israel akimvisha taji mrembo Lisa Jensen mara baada ya kutangazwa mshindi katika shindano hilo usiku huu     
Warembo wa Redds Miss World Tanzania wakicheza shoo ya ufunguzi  

Banda la NSSF lang'ara Maonyesho ya Sabasaba


 Banda ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) linavyoonekana katika Viwanja vya Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara nchini (Saba saba.)
Meneja Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume akimuelekeza jambo mmoja wa Wadau wa NSSF alietembelea banda hilo kwenye viwanja vya SabaSaba.
Ofisa Mwandamizi wa Huduma za Wateja kwa Umma, Juma Kintu (kulia) akiwa katika banda la NSSF.

BAN KI MOON AMUAGA RASMI DKT. ASHA-ROSE MIGIRO


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akiwa na Mkewe, anayefuatia ni Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Asha-Rose Migiro akiwa na Mumewe,  Profesa Cleophas Migiro wakisubiri kusalimiana na wageni waalikwa wakati wa hafla ambayo Ban Ki  Moon aliandaa maalum kwajili ya kumuaga msaidizi wake wa Karibu.
Profesa Migiro akiwa na Bint yake, Chansa- Jasmin wakifuatilia hafla hiyo kwa makini.

Matukio mbali mbali hospitali ya Muhimbili


Madaktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam wakimpakia kwenye Gari Daktari Mwenzao aliepatwa na Mkasa wa Kutekwa Nyara na watu wasiojulikana na ambao walimjeruhi vibaya sana,Dk. Steven Ulimboka aliepatwa na mkasa huo usiku wa kuamkia leo huko katika msitu wa Mabwepande,jijini Dar
Wanahabari wakihangaika kupata picha ya Dk. Steven Ulimboka alieinginzwa
kwenye gari hiyo tayari kwa kupelekwa kwenye Taasisi ya Mifupa (MOI) kwa matibabu zaidi.

Friday, June 29, 2012

CHADEMA NA CUF WAMEIKATAA TUME YA KUCHUNGUZA SAKATA LA DR. ULIMBOKA ILIYOUNDWA NA KOVA

Leon Bahati na Aidan Mhando
VYAMA vya siasa vya upinzani vya Chadema na CUF vimesema havina imani na tume iliyoundwa na Serikali kupitia Jeshi la Polisi kuchunguza tukio la kutekwa nyara na kujeruhiwa kwa Mwenyekiti wa  Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Steven Ulimboka.

Badala yake vimetaka iundwe tume huru itakayohusisha vyombo vya dola, madaktari na asasi zisizo za kiserikali.
Taarifa zilizotolewa kwa nyakati tofauti na vyama hivyo viwili, zilisema vyote vinaamini kuwa kwenye tukio hilo la kinyama lina mkono wa Serikali.
Sekretarieti ya Chadema ikiongozwa na Mkurugenzi wa Mafunzo na Oganaizesheni, Benson Kigaila, jana ilitishia  kuunganisha nguvu ya umma katika kuibana Serikali kama tume hiyo haitakuwa tayari kuunda tume huru.Akizungumza na waandishi wa habari, Kigaila waliilaumu Serikali kwa kitendo chake cha kushindwa kutekeleza madai ya madaktari,  wakati ikiruhusu fedha yingi kupotea kwa njia za uzembe na ufisadi.

Dk Ulimboka akiendelea kupata matibabu

Dkt. Ulimboka akiwa katika hali mbaya mara baada ya kuokotwa akiwa hajitambui. Inadaiwa Ulimboka alitekwa jana mida ya saa 6 usiku baada ya kupigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kwa jina la Abeid na alitekwa na watu wawili waliokuwa na silaha. Kufuatia hali hii wafanyakazi wa chumba cha maiti Muhimbili nao wamegoma na mgomo huenda ukawa mkubwa zaidi!





Tuesday, June 26, 2012

Swali la nyongeza la Mh.Zitto Kabwe laleta chereko Bungeni Hii imetokea muda huu Bungeni



Mh.Zitto Kabwe aliuliza swali dogo la nyongeza ''kuwa toka tupate uhuru hajawahi sikia Mkuu wa Majeshi(JWTZ) akitoka upande wa pili wa Muungano Je ni kwanini ?

Waziri wa Ulinzi akamjibu '' kuwa hilo ni suala la wakati kwani hivi sasa kuna majenerali wanne wako makao makuu huenda huko mbele mmojawapo akapata bahati hiyo.

Lakini akaaamsha chereko na makofi kwa wabunge pale aliposema kuwa hata yeye anajiuliza lini ndani ya chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Mwenyekiti wa chama atatoka Kigoma ?

Baada ya hapo kama kawaida ikawa ni kugonga meza kwa furaha na vigelegele Bungeni
hali iliyomfanya Mwenyekiti anaeongoza kikao asubuhi ya leo kuingilia kati.

ONA MASHABIKI WA UINGEREZA WALIVYOFANYA





Taswira zikiwaonyesha mashabiki wawili Waingereza walioamua kushusha bukta kama zilivyonaswa .
Wakati Mchezaji wa Italia Alessandro Diamanti akipiga mkwaju wa mwisho mashabiki wawili waliamua kushusha bukta zao walizovaa ili kumzubaisha mpigaji penati katika hali ya kumzubaisha mpigaji huyo lakini aliweza kutumbukiza kwenye kamba mkwaju huo na kuwaacha hoi Waingereza.

MAHAKAMA YATOA ONYO KWA MADAKTARI

50 CENT APATA AJALI



50 Cent akipelekwa hospitali baada ya ajali hiyo.
Lori lililogonga gari la 50 Cent.

Mkoko wa 50 baada ya ajali.
Mwanamuziki Curtis James Jackson '50 Cent' usiku wa kuamkia leo amepata ajali mbaya baada ya gari lake kugongwa na lori. Baada ya ajali hiyo 50 Cent alikimbizwa katika hospitali ya Queens kwa matibabu. Dereva aliyekuwa anaendesha gari lake naye amelazwa hospitali baada ya ajali hiyo mbaya.
PICHA ZOTE KWA HISANI YA: www.thisis50.com

Monday, June 25, 2012

BUNGENI DODOMA

AJALI YA NDEGE ILIYOTOKEA KATANGA DRC CONGO



hivi vingetakiwa kuwa Dar kutokana na foleni


WEMA SEPETU AZINDUA FILAMU YAKE YA SUPER STAR


Mwigizaji Wema Sepetu akiingia ukumbini wakati wa uzinduzi wa filamu yake ya Super Star aliyoizindua kwenye hoteli ya Hyyat Kilimanjaro jijini Dar es salaam usiku huu, ikihudhuriwa na watu maarufu pamoja na wanamzuziki na waigizaji, picha zaidi za tukio hili zitawajia baada ya muda
Wema Sepetu akipozi kwa picha mara baada ya kukaa kabla ya kuanza kuchezwa kwa Demo ya filamu hiyo usiku huu kwenye hoteli ya Hyyat Kilimanjaro.

WEMA SEPETU JANA USIKU NA JINSI STAA WA NIGERIA OMOTOLA ALIVYOPOKEWA DAR.

Red carpert ya nguvu Kempiski Hotel Dar es salaam.
Red carpert

Mohammed Mursi Aibuka Kidedea Uchaguzi Wa Misri




Mursi ameshinda kura kwa asili mia 51.7% akimshinda mpinzani wake wa karibu Ahmed Shafik kwa mujibu wa tangazo la tume ya uchaguzi wa juu wa Rais.


Mkuu wa jopo la Majaji, Farouq Sultan, amesema kua wamezingatia malalamiko 466 kutoka kwa wagombea, ingawa matokeo ya uchaguzi hayatobalika.


Tangazo hilo lilifuatiwa na shangwe na vigelegele katikakati ya medani ya Tahrir mjini Cairo ambako wafuasi wengi wa Bw.Mursi walikua wamekuanyika.

Waraka Wa Kwanza Wa Mnyika Kwa Wananchi,Ukweli Ni Uhuru






Waraka wa kwanza mwaka 2012 wa Mbunge kwa Wananchi- “Ukweli ni Uhuru”


Waheshimiwa Wananchi wenzangu,
Amani iwe kwenu,
Kwa kipindi cha wiki nzima kumekuwepo na mjadala mkali bungeni, kwenye vyombo vya habari, mitandao ya kijamii na katika taifa kwa ujumla juu ya bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2012/13 sanjari na yaliyojiri kutokana na kauli niliyotoa bungeni juu ya udhaifu wa Rais katika usimamizi wa maandalizi na utekelezaji wa bajeti pamoja na mipango muhimu ya maendeleo. Ukweli ni uhuru!.


Aidha, kupitishwa kwa Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa mwaka wa Fedha 2012/2013 na Bajeti ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2012/2013 bila marekebisho yoyote ya msingi pamoja na michango mingi ya wabunge ya kukosoa kumedhihirisha kile nilicho tahadharisha tangu awali kwamba; kwa kuwa udhaifu wa kikatiba umetoa nguvu kubwa kwa Rais juu ya bajeti na uendeshaji wa nchi, udhaifu wa Rais una athiri maisha ya wananchi. Ukweli ni Uhuru!.


Katika mazingira haya, udhaifu wa rais na uzembe wa bunge unapandikiza migogoro kati ya wananchi na serikali kutokana ufisadi na masuala ya maendeleo kutopewa kipaumbele cha kutosha zaidi ya matumizi ya kawaida lakini pia inachochea pia migomo baridi ya watumishi wa umma hususun madaktari, walimu na askari kutokana pia na madai yao ya muda mrefu kutokuzingatiwa kwenye bajeti.
Ukweli ni Uhuru!.
Kadhalika udhaifu wa kanuni za Kudumu za Bunge umefanya wabunge kuwekewa mipaka kwa mujibu wa kanuni 97 (2) ya kuchangia mjadala kuhusu hotuba ya bajeti kwa kuchangia tu mambo ya ujumla yanayohusiana na hali ya uchumi wa nchi na kwamba mbunge yoyote haruhusiwi kupendekeza mabadiliko katika makadirio ya mapato na matumizi ya serikali. Ukweli ni Uhuru!.

Uingereza Yatolewa Euro 2012





Timu ya England ya soka imeondolewa katika mashindano ya Euro 2012, baada ya kufungwa na Italia usiku wa Jumapili katika robo fainali, kwa kufungwa magoli 4-2 ya penalti mjini Kiev, Ukraine, kufuatia muda wa kawaida na dakika 30 zaidi kumalizika kwa timu hizo mbili kutofungana.

Italia sasa itapambana na Ujerumani katika mechi ya nusu fainali.

Alessandro Diamanti alifunga bao la kuamua mshindi katika mikwaju hiyo ya penalti, baada ya Ashley Young na Ashley Cole kukosa kufunga mabao kupitia mikwaju waliyopiga.

Saturday, June 23, 2012

FFU WA NGOMA AFRICA KUBAMIZA AFRO-RUHR FESTIVAL MJINI DORTMUND, UJERUMANI JUMAMOSI 30 JUNI 2012

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA UMOJA WA MATAIFA KUHUSU MAZINGIRA ENDELEVU JIJINI RIO DE JANEIRO-BRAZIL

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili kwenye Viwanja vya Ukumbi wa Mikutano, wakati alipofika kuiwakilisha nchi katikaMkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira Endelevu (Rio+20) jana Juni 21, jijini Rio de Janeiro, nchini Brazil. Mkutano huo ni wa pili kufanyika nchini hapa tangu ulipofanyika kwa mara ya kwanza mwaka 1992. Kushoto kwake ni Balozi wa Tanzania nchini Brazil, Francis Malambugi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira Endelevu (Rio+20) jana Juni 21, jijini Rio de Janeiro, nchini Brazil. Mkutano huo ni wa pili kufanyika nchini hapa tangu ulipofanyika kwa mara ya kwanza mwaka 1992.

TANGAZO- WADAU NA MACHINGA WOTE MNAOMBWA KUHUDHURIA KATIKA MKUTANO/SEMINA TAR 29/06/2012 MACHINA COMPLEX GHOROFA YA 5 ILALA

Kuelekea Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Ulimwenguni



Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za Kulevya iliyopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu ndio chombo kilichopewa jukumu la kuratibu masuala yote yanayohusu dawa haramu za kulevya hapa nchini kupitia mikakati yake mikuu miwili ya kuzuia matumizi  na ule wa kuzuia biashara haramu ya dawa za kulevya. 

Ikumbukwe kwamba biashara ya dawa za kulevya ndio huchochea matumizi ya dawa hizo na kuleta athari kwa mustakabali wa Taifa letu kiafya, kijamii, kiuchumi, kisiasa na hata kimazingira.

MISS DAR INDIAN OCEAN 2012

Mrembo Diana Hussein (kati) amefanikiwa kunyakua taji la Miss Dar Indian Ocean kutoka kwa mwanadada Stella ambaye amemaliza muda wake, mwanadada huyu alifuatiwa na Kudra Lupatu (kulia) na Zulfa Vuai (kushoto). Shindano la Miss Dar Indian Ocean 2012 limefanyika ndani ya Kijiji Cha Makumbusho Dar es Salaam

 Hawa ndiyo warembo wa Tano Bora wakiwa na Miss Dar Indian.
Warembo waliofanikiwa kuingia tano bora.
















Warembo waliofika 10 bora kabla ya kuingia kwenye mchujo wa kutafuta tano bora.
*Keep refreshing the page mambo yote yanakuja...ni Miss Dar Indian Ocean 2012...

HOFU YA MADAKTARI KUGOMA YATANDA

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi

MAHAKAMA YAZUIA,MADAKTARI WABANDIKA MATANGAZO MUHIMBILI KUHAMASISHANA

Na Waandishi Wetu
MTAFARUKU kati ya Serikali na Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) kilichotangaza kuanza mgomo wa nchi nzima leo, umechukua sura mpya baada Mahakama Kuu ya Tanzania Kitengo cha Kazi, jana kutoa amri ya kusitishwa jambo hilo huku wanataaluma hao wa tiba wakisisitiza kushikilia msimamo wao. Mahakama hiyo ilitoa amri kuwataka madaktari hao kuendelea na kazi hadi madai yao msingi katika mgogoro huo, yatakaposikilizwa.

YEAR 2050

BARCA FUTURE IN DANGER :P

Thursday, June 21, 2012

MH: ZITTO AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI KIVULI

 
Zitto akiwasilisha hotuba ya bajeti kivuli.
Katika mjadala unaoendelea Bungeni kuhusu Bajeti, baadhi ya wabunge wameeleza kwamba Bajeti Kivuli haikuonyesha vyanzo vya mapato na hivyo kuita ni vyanzo sifuri. Ukweli ni kwamba tumeweka vyanzo vya mapato ya ndani kwa ujumla bila kuainisha mapato ya kikodi ni ngapi, mapato yasiyo ya kikodi ni ngapi na mapato ya Halmashauri ni kiasi gani. Hivyo tunakiri kosa hili na tumechukua hatua ya kuainisha mapato hayo Kama inavyoonekana kwenye jedwali hili hapa chini.
  MAPATO
SHILINGI MILIONI
A Mapato ya ndani

11,889,078
  i)mapato ya kodi (TRA)
10,232,539
  ii)Mapato yasiyo ya kodi
1,163,533
B Mapato ya Halmashauri
493,006
Mapato haya yamo ndani ya Hotuba ya Bajeti Mbadala lakini kwa makosa ya kihariri hayakuonyeshwa kwenye jedwali na hivyo kuleta usumbufu kwa Wabunge na Watanzania wengine waliopata fursa ya kusoma Hotuba yetu. Tunaomba radhi kwa usumbufu. Nawashukuru walioona tatizo hili na hii inaonyesha kuwa wabunge wanasoma kwa makini Bajeti ya Upinzani.
Ninawatakia mjadala mwema wa Bajeti.
Kabwe Zuberi Zitto,Mb
Waziri wa Fedha na Uchumi Kivuli
19.06.2012

Wednesday, June 20, 2012

TANZANIA BLOG AWARDS Blogs zilizopita katika shindano letu la 2012

Hongera kwa bloggers wote ambao majina yao yalipendekezwa kushiriki katika shindano hili la mwaka 2012.  You are all winners no matter what....

Baada ya kutembelea blogs nyingi tumeona kuwa sio watu wengi wanatumia badges tunazozitengeneza. Hivyo kwa mwaka huu tutaweka ya aina moja tu lakini kama unataka maalumu ya kipengele blog yako iliyopendekezwa basi utuandikie tutakutumia.  Kama kutakua na maombi ya watu wengi basi tutazitengeneza na kuziweka hapa lakini kama ni watu wawili watatu tu basi wengine wale wanaopenda watatumia hii tutakayoiweka ya mwaka huu. Lakini mwisho wa kuomba hizo badges ni Jumatano. Baada ya hapo itakayotumika ni hii moja tu.

Kura zitaanza kupokelewa jumatatu  tarehe 17th June na mwisho wa kupoke ani tarehe 30th June. Ni kwa muda wa wiki mbili tu...
kutaka kupigia kura ingia kwenye: http://www.tanzanianblogawards.com

Majina yaliyoingia mwaka huu katika vipengele vyetu ni  haya :-

USIKU WA NDEGE MNANA

LINAH..BAADA YA ZIARA YAKE KUTOKA MAREKANI..ATAWASHA MOTO JUMAPILI HII 
AKIWA NA LIVE BAND NDANI YA MAISHA CLUB AKISINDIKIZWA NA MASUPERSTAR WENGINE,
MWANA FA,AMINI,DITTO NA COUNTRY BOY....USIKOSE USIKU WA NDEGE MNANA !

New