My Web

Emmanuel

CONTACT

Tuesday, June 26, 2012

Swali la nyongeza la Mh.Zitto Kabwe laleta chereko Bungeni Hii imetokea muda huu Bungeni



Mh.Zitto Kabwe aliuliza swali dogo la nyongeza ''kuwa toka tupate uhuru hajawahi sikia Mkuu wa Majeshi(JWTZ) akitoka upande wa pili wa Muungano Je ni kwanini ?

Waziri wa Ulinzi akamjibu '' kuwa hilo ni suala la wakati kwani hivi sasa kuna majenerali wanne wako makao makuu huenda huko mbele mmojawapo akapata bahati hiyo.

Lakini akaaamsha chereko na makofi kwa wabunge pale aliposema kuwa hata yeye anajiuliza lini ndani ya chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Mwenyekiti wa chama atatoka Kigoma ?

Baada ya hapo kama kawaida ikawa ni kugonga meza kwa furaha na vigelegele Bungeni
hali iliyomfanya Mwenyekiti anaeongoza kikao asubuhi ya leo kuingilia kati.

No comments:

Post a Comment

New