My Web

Emmanuel

CONTACT

Friday, June 29, 2012

CHADEMA NA CUF WAMEIKATAA TUME YA KUCHUNGUZA SAKATA LA DR. ULIMBOKA ILIYOUNDWA NA KOVA

Leon Bahati na Aidan Mhando
VYAMA vya siasa vya upinzani vya Chadema na CUF vimesema havina imani na tume iliyoundwa na Serikali kupitia Jeshi la Polisi kuchunguza tukio la kutekwa nyara na kujeruhiwa kwa Mwenyekiti wa  Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Steven Ulimboka.

Badala yake vimetaka iundwe tume huru itakayohusisha vyombo vya dola, madaktari na asasi zisizo za kiserikali.
Taarifa zilizotolewa kwa nyakati tofauti na vyama hivyo viwili, zilisema vyote vinaamini kuwa kwenye tukio hilo la kinyama lina mkono wa Serikali.
Sekretarieti ya Chadema ikiongozwa na Mkurugenzi wa Mafunzo na Oganaizesheni, Benson Kigaila, jana ilitishia  kuunganisha nguvu ya umma katika kuibana Serikali kama tume hiyo haitakuwa tayari kuunda tume huru.Akizungumza na waandishi wa habari, Kigaila waliilaumu Serikali kwa kitendo chake cha kushindwa kutekeleza madai ya madaktari,  wakati ikiruhusu fedha yingi kupotea kwa njia za uzembe na ufisadi.


Alisema historia inaonyesha kuwa matukio mengi yaliyochunguzwa na polisi, matokeo yake hayajawekwa hadharani.
Mkurugenzi huyo alisema matukio hayo ni mauaji ya watu wawili yaliyotokea katika chaguzi ndogo za Igunga na Arumeru mashariki.

Hali kadhalika, tukio la kumwagiwa tindikali kwa mwandishi wa habari Seid Kubenea.Taarifa ya Kaimu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Haki za Binadamuna wa CUF, Abdul Kambaya ilisema Serikali inapaswa kuchukua hatua za haraka kwa kuunda tume huru bila kuhusisha Jeshi la Polisi ili uchunguzi wa kina tukio hilo.

No comments:

Post a Comment

New